Kipindi hicho wanafunzi walikuwa wangapi? Tena miaka hiyo huenda walikuwa wanapikiwa msosi kama sekondari. Wanafunzi wote walikuwa wanapata accommodation vyuo, sasa hali ni tofauti. Nafikiri kuna assignment kubwa ya kufanya kabla hatujaifikia.
Ulipaswa kwenda zaidi ya kuangalia idadi ya wanafunzi tu. Ni vyema ukaangalia population nzima na uwiano wake k umuri.
Ccm imekuwa zero katika matumizi sahihi ya raslimali kwa mustakabalisahihi wa maendeleo ya nchi na hivyo kuendup kuwa na idle resources and man power kubwa, ama uzalishaji usio na tia kwa taifa.
Mchakato wa kutoa elimu bure haukai kisiwani peke yake ni interrelated mpango unaotegemeana sana kwa karibu na mipango mingine kwa ujumla yake ikiwemo kuongeza uzalishaji wenye tija, ukusanyaji sahihi wa mapato na matumizi bora ya raslimali zote ikiwemo watu, na magawanyo sahihi wa mapato ya serikali.
Suala la elimu bure haliwezi kuwa halisi bila kupunguza mianya ya ukwepaji kodi iliyolelewa na serikali ya ccm.
Ni vigumu kuongeza mapato bila kuwekeza kwenye uzalishaji bora na masoko kwa ngazi zote likwemo swala la kufufua sector ya viwanda ambayo ccm imeua na kuzika, kuimarisha uzalishaji kilimo kitu ambacho kimekuwa midomoni na si mioyoni mwa ccm na elimu ambayo ndiyo mwanga katika kila hatua.
Lakini ni jambo lisiloeleweka mtu aseme anaboresha viwanda bila kujua wala kuzingatia upatikanaji wa nishati. Viwanda vinahitaji nishati. Nishati hiyo ya kufanikisha viwanda inatoka wapi ikiwa ccm wanampango wa kuzima hata hivi vimuli muli vya tanesco vya sasa? Hawana hata habari kama viwanda vinamahitaji yake. Ccm wamebaki kunakili kwa juujuu mipango ya UKaWA.
Yako mengi sana ambayo yanahitaji akili nyingine na SIYO CCM ambayo imeyatengeneza eti ijiadai kuyamaliza. Huu utakuwa wehu.
Mfano. UKAWA vipaumbele vyao ni elimu, elimu , elimu katika maeneo yote ya raslimali watu, matumizi na hifadhi ya ardhi yetu na vyote vilivyomo, siasa safi wakianzia na muundo wa katiba mpya ya nchi kwa ajili ya Watanzania na Tanzania yao waitakayo, uongozi bora na matumizi halali, sanifu na sahihi ya nyenzo hizi juu kwa kusukuma mbele ustawi wa taifa la Tanzania katika nyanja zote.
HATUTEGEMEI KUPATA TAFSIRI SAHIHI YA MKAKATI HUU KUTOKA CCM KWA KUWA SI MAONO WALA NIA YAO NA UWEZO HAWANA WA KUBORESHA KITU ZAIDI YA KULINDA MASLAHI YAO TU. KUIGA KOTE HUKU KUTOKA UKAWA NI KUKOSA DIRA, KUTOKUKUBALIKA NA KUTOKUWA NA DHAMIRA SAFI KWA CCM JUU YA TAIFA.
Ninaomba, unapokuwa na swala usilolielewa, kitu ambacho si dhambi, badala ya kujifanya unajua na kutoa hitimisho kwa kuwa hufahamu, jaribu kuuliza kwa kuwa hakuna mtu anajua vyote na huwezi kutoa jibu kwa kitu kiko moyoni kwa mwingine.
MABADILIKO YA TANZANIA NI UKAWA TU NA WALA SI CCM AMBAYO IMESHINDWA MIAKA YOTE NA BADO HAINA MAJIBU, UWEZO WALA NIA YA KUFANYA LOLOTE LA KUIPELEKA TANZANIA KATIKANJIA SAHIHI.
CCM IKAE PEMBENI IONE WENGINE WANAFANYAJE KATIKA KULIONGOZA TAIFA BADALA YA KUJIFNAYA WANAJUA WAKATI WAMESHINDWA.