Mmakua Mmakonde
Member
- Aug 23, 2016
- 61
- 144
Kwa masikitiko makubwa napenda kutoa dukuduku langu ktk hili suala la elimu bure. Najua hili suala lipo kwa nia njema kabisa la kusaidia upatikanaji wa elimu kwa familia za hali ya chini. Lkn kama ilivyo duniani kote suala la elimu kuwa bure halipo na kinachofanyika ni serikali kugaramia mahitaji muhimu kwa hawa watoto kwa niaba ya wananchi wake. Hivyo ni jambo la msingi serikali ikajipanga na kutathmini changamoto mbalimbali zinazojitokeza ktk hizi stage za kwanza za utekelezaji wa huu mpango.
Naandika haya baada ya kufuatilia maendeleo ya kijana wangu anayesoma ktk shule za serikali kabla na baada ya huu mpango. Hapo kabla nilikuwa nikishuhudia mtoto wangu akifanya mazoezi ya mara kwa mara kila wiki,mwezi, katikati ya muhula ma mwisho wa muhula na nilikuwa napata ripoti za mwalimu wa darasa kuhusu maendeleo yake. Lakini kwa sasa ni mitihani miwili tuu ya kati na mwisho wa mwaka ndio hufanyika hakuna cha weekly,mothly wala midterm test. Haya mazoezi ndio yalikuwa yanawasaidia sana waalimu kujua udhaifu wa watoto na kujua namna ya kuwasaidia. Kila nikimuuliza mtoto wangu kwa nn hamfanyi ananijibu "Elimu bure Baba". Nikaenda shule kuulizia nao wananijibu "Elimu bure Mzazi hatuna fungu la kuratibu hayo matakwa yako ata kama yana faida kwa watoto" . Hapa ndipo nilipoamua kufanya maamuzi magumu ya kumtoa mtoto wangu na kutafuta elimu ya kulipia walau nitimize malengo ya mwanangu. Chonde chonde serikali ni vema kama kuna mapungufu katika kila jambo ni vzr kuyarekebisha haraka maana hakuna jambo ambalo halipaswi kuchezewa kama elimu za watoto wetu maana umri ukiwapita ndio basi tena wataendelea kuburuzwa mpaka kufa kwao huko mbeleni.
Elimu bure iendane na hali halisi ya ufundishaji huko mashuleni na sio kuwakomoa waalimu ambao nao umaliza hasira zao kwa watoto wetu na mwisho wa siku msingi wa hili jambo jema uwa ni kubomoa tofauti na kujenga iliyotarajiwa.