Elimu bure imefukuzisha walinzi wa shule

Elimu bure imefukuzisha walinzi wa shule

U

Ukishaingia u ccm na uchadema mambo yanaharibika utaifa unafutika, uzalendo unayeyuka! Rais Magufuli ameingia madarakani akiwa na nia ya kutaka kurekebisha mambo mengi yaliyoharibika ikiwemo Elimu. Ninaamini kwamba kama zingekuwepo fedha za kutosha asingesita kuagiza zielekezwe sehemu zilizo na upungufu. Pia, waziri wa Elimu Watanzania wengi wanamkubali kwamba anao uwezo wa kusimamia mageuzi katika elimu nchini. Inasikitisha kuona ndani ya miezi mitatu tu ya awamu ya 5 watu wanataka mambo yabadilike. Magufuli ameonyesha nia njema, jukumu letu in kumpa muda na ushirikiano ili juhudi zake za kutuletea maendeleo zizae mtunda.
Watoto wako shule ndugu hawawezi subiri. JPM mwenyewe hakusubiri akutane na wadau waelimu ili ajue nini changamoto za elimu na ni njia ipi ifanyike ili elimu bure iwezekane. Yeye alikurupuka bila hata kuwa na waziri wa elimu. hakujipa hata muda, sasa kwanini unataka sisi wananchi tunaoumia tumpe muda? Mbona hakuwapa muda hao aliowasimamisha kazi na kuwafukuza? Rais aache kukurupuka asiongoze nchi kama shule.
 
Kabla ya hapo ulikua unatoa sh ngapi?, weka hapa tujue kama kipato cha shule kimepanda au kimeshuka

Shule za msingi zinaingiziwa ruzuku ya Elimu Bure kila mwezi,katika ruzuku hiyo Kuna mgawanyo wa vifungu tano navyo ni utawala,ukarabati,mitihani,michezo na vifaa.Katika shule anayosoma mwanangu shule imepewa jumla ya sh 280000 shule hiyo inajumla ya wanafunzi 535.Chakushangaza serikali imeshindwa kabisa kutenga pesa kwa ajili ya kumlipa mlinzi,kutoa lishe(uji) shuleni.
Hata pesa zilizotolewa kwa ajili ya mitihani hazitoshi kabisa.Elimu Bure imeleta shida zaidi shuleni
 
Mi ya mwanangu ina watoto 246 ilipata tsh 146000 nkamuuliza ticha mbona zinaishia kwenye chaki tu na red pen? Andalio mmenunua na nin? Akaanguka akazimia

Hiyo fedha inatosha sana kununua vifaa vya kufundishia madarasa 7 kwa miezi 3. Box 7 za chaki 35,000. Box 2 za red pen (kalamu 100) 40,000. Andalio sh ngapi bhana acha majungu
 
Pesa zinatumwa kila mwezi wala msipate shida magufuli anaona mbali.
 
Acheni kusambaza ujinga. Mion

Michango yote hata kama wazazi wameridhia imezuiwa, labda kama wazazi watachangishana bila kumshirikisha mkuu wa shule, haujasikia mkurugenzi kaondolewa kisa michango?[/QUOTE]
ndivyo hivyo watu wakiamka wala hajatafiti angalau kidogo kazi kumlaumu magufuli, muongozo wa michango sio kupitia mwalimu mkuu tena. Mwalimu mkuu ni mjumbe katika vikao vya serikali ya kijiji au mtaa shule ilipo. Matatizo yote ya shule kama mlinzi, uji, vyoo, madarasa anayatoa kule then serikali ya kijiji inachangisha. Tatizo viongozi sijui kwa nini hawafafanui kwa wananchi, na wananchi wamepata uchochoro wa kukimbia michango. Hili natamani Magufuli mwenyewe ahutubie taifa ku clarify masuala yanayopotoshwa. Inafikia wapotoshaji wanaanza kuaminika. Go Magufuli,go!
 
Mimi kama mwalimu wa michezo nauliza hivi hata michango ya sherehe ya kuhitimu kidato cha nne nayo imezuiliwa? Je michango ya field trips nayo vipi?
 
Iko haja ya Wakuu wa shule kurudisha miradi kama vile ile ya EK yaani Elimu ya Kujitegemea. Hii inaweza ikawaongezea kipato cha shule ikiwa ni pamoja na kuipunguzia serikali mzigo wa gharama za uendeshaji.
 
Back
Top Bottom