Elimu bure dhidi ya Huduma bora za afya

neno1

Senior Member
Oct 9, 2013
196
141
Nawaza tu kwa maandishi kwamba kati ya Elimu bure kama sera ya awamu ya tano na Huduma bora za afya kipi kingetangulia.

Binafsi nafikiri huduma zetu za afya ni mbovu sana na watanzania wengi wamekuwa wakipoteza maisha sababu ya tatizo hili. Haya yanayofunuliwa sasa ni sehemu tu kuna mengi hatuyajui. Kama umewahi kuguswa na msiba wa ndugu uliodhani shida ni huduma mbovu utanielewa. Hii inachangiwa na ukosefu wa madaktari wa kutosha, vifaa duni na vya kizamani lakini pia elimu isiyotosheleza ya watumishi wa kada hii.

Nadhani hili lingepewa kipaombele cha kwanza kwani ukilinganisha ugonjwa na elimu nadhani mtoto anaweza subiri utafute ada siku mbili au tatu lakini akiugua na bahati mbaya akafariki hata hiyo shule hutakuwa na wakuisoma.
 
Back
Top Bottom