Elimu bure chachu ya ufaulu darasa la saba 2017

Elimu bure chachu ya ufaulu darasa la saba 2017

JINOME

JF-Expert Member
Joined
May 29, 2017
Posts
958
Reaction score
1,427
Matokeo ya Mtihani wa Darasa la Saba uliofanyika Septemba 6 – 7, 2017 yametoka yakiwa naongezeko la asilimia 2.40 ukilinganisha na matokeo ya Darasa la saba ya mwaka jana (2016). Katibu Mtendaji wa Necta Dk. Charles Msonde ameanika hadharani matokeo hayo.

“Watahiniwa 662,035 kati ya 909,950 waliofanya mtihani huo wamefaulu kwa kupata alama 100 au zaidi kati ya alama 250 wanazopaswa kupata. Kati ya waliofaulu, wasichana ni 341,020 ambao ni sawa na asilimia 70.93 na wavulana ni 321,015 sawa na asilimia 74.80. idadi ya watahiniwa waliofaulu ni sawa na asilimia 72.76. Mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa asilimia 70.36, hivyo kuna ongezeko la ufaulu kwa asilimia 2.40” Amesema Katibu Mtendaji wa Necta, Dk Charles Msonde

Tangu Rais Dk. John Pombe Magufuli aingie madarakani mwaka 2015 amekuwa akitoa ELIMU BURE kuanzia Shule ya Msingi (Darasa la Kwanza) hadi Kidato cha Nne. Rais Magufuli ameleta maboresho makubwa kwenye sekta ya Elimu nchini kwa kuhakikisha Serikali yake inagharamikia Tsh. Bilioni 18.77 kila mwezi kutoa Elimu Bure hali iliyopeleka Wanafunzi wengi kuandikishwa Darasa la kwanza, hata bidii ya Wanafunzi kimasomo imeongezeka pia.

Serikali ya Rais Magufuli imepeleka Madawati ya kutosha nchi nzima; Serikali imetumia Tsh. Bilioni 16.9 kununua vifaa vya Maabara kwa shule za Sekondari 1696; Baadhi ya Waalimu wameshaanza kulipwa malimbikizo yao na wengineo wakiboreshewa na kupandishwa madaraja na mishahara.

Hakika kazi inafanyika na matunda yake yanaonekana kwa jamii. Tuendelee kumuunga mkono Rais Magufuli na Serikali yake katika harakati za kupambana na adui “Ujinga” kwa maslahi mapana ya Taifa letu

Shilatu E.J
 
Mdogo wangu amepata A tano

Nasubiri nione atachaguliwa wapi kama vipi nimfanyie transfer kwenda special school hasa hasa Kibaha
 
Mdogo wangu amepata A tano

Nasubiri nione atachaguliwa wapi kama vipi nimfanyie transfer kwenda special school hasa hasa Kibaha
Mi mdogo wangu (ke) amepata A nne na B moja sijui atapangwa shule gani aisee maana usishangae wakamtupa shule ya kata tena day mwanzo mwisho
 
Nimegundua ,he is very geneus,kuna siku,nilmuliza mbona,unachelewa shule?akajibu,mmmmh,baba mbona hata walimu wanachelewaga,nikajua hapa shughuli IPO,sasa hz A_math,science,B_maarifa,B,C_2,Asomo LA mwisho,nimestuka
 
Laiti mngejua Blanda zinazofanywa na walimu huku kwenye halmshauri hasa za wilaya msingejisifia kwa matokeo hayo.

Dogo anapiga A flat masomo matano na hisabati bonge LA banda lakini muulize kanuni ya kutafuta eneo la duara lenye kipenyo kizima hajui (πD^2)/4.

Sasa jiulize kapataje hizo maksi nasemaje kuna blanda nyingi zinafanyika huku kati matokeo hayana uhalisia kilichomo kichwani kwa madogo .
 
Back
Top Bottom