Elimu ambayo Padri hawezi kukupa

Elimu ambayo Padri hawezi kukupa

Ulevi na ulafi ni kunywa na kula kupita kiasi.

Kama tafsiri ya ulevi ni kunywa kinywaji chenye 'alcohol' basi; kila mtu ni mlevi.

Ukipima kiwango cha alcohol kwenye mtindi, sharubati zilizolala(haikuwekwa kwenye jokofu) nk utakuta zinakiwango cha alcohol.
 
Watu wasiokunywa pombe wanaonaga mbinguni ni mali yao tuu yani kama mtu hanywi pombe anajikuta mbele ya Mungu yeye ndiye msafi kumbe wapi wahenga wakasema "wapeni masikini mvivyo wanywe wasahau shida zao....."
 
Shida ya pombe kama ilivyo cocaïne, bangi nk ni matumizi mazuri (moderation). Hata ugali ukila kupindukia ni dhambi, pombe hivyo hivyo, ngono, etc. Everything should be taken in moderation, hata maji ya kunywa!
Sasa hayo unayasema wewe na Kwa mtazamo wako
 
BIBLIA HAIKATAZI POMBE
●Zaburi 104:15
Na divai imfurahishe mtu moyo wake. Aung'aze uso wake kwa mafuta, Na mkate umburudishe mtu moyo wake

Yesu mwenyewe alikuwa stadi wa kutengeneza pombe
●Yohana 2:7–10
7 Yesu akawaambia wale watumishi, “Ijazeni mitungi hiyo maji.” Wakaijaza mpaka juu. 8 Kisha akawaambia, “Sasa choteni maji kidogo mumpelekee mkuu wa sherehe.” Wakachota, wakampelekea. 9 Yule mkuu wa sherehe akayaonja yale maji ambayo yalikuwa yame geuka kuwa divai.



BIBLIA INAKATAZA ULEVI
1. WAKORINTHO 6:10
walevi, wasengenyaji, wanyanganyi, hao wote hawatashiriki ufalme wa Mungu.

●WAEFESO 5:18
Acheni kulewa divai maana hiyo itawaangamiza, bali mjazwe Roho Mtakatifu.
Sidhani kama hayo maelezo yakoyanatetea na kuonyesha kuwa pombe imeruhusiwa katika biblia!
 
Usiwe miongoni mwao wanywao mvinyo; Miongoni mwao walao nyama kwa pupa. Kwa maana mlevi na mlafi huingia umaskini, Na utepetevu humvika mtu nguo mbovu.
................... Mithali 23:20-21 .....................
 
JE, BIBLIA IMERUHUSU POMBE?

Kuna aya tata katika biblia ya kiswahili ambazo walevi wanazitumia kutetea unywaji wa pombe, na wale walio maadui wa Ukristo pia wanatumia aya hizo kuponda Ukristo eti umeruhusu pombe. Jibu ni kwamba biblia haijaruhusu pombe ila kuna watu maarufu katika biblia walikunywa pombe kwa tamaa zao, ambao watu wasio na akili wanatumia udhaifu huo kuhalalisha unywaji pombe.

Kitu cha muhimu kujua kwanza ni lazima tufahamu kuwa Biblia zetu ni tafasiri za lugha zetu za asili yaani kiswahili na kiingereza nk ambazo si lugha ambazo zimeandikiwa Biblia. Lugha ya asili ya Agano la kale ni Kiebrania na kwa sehemu Kiaramu, wakati lugha ya asili ya Agano jipya ni kiyunani na kwa sehemu kiebrania, hizi ni lugha ambazo zina utajiri mkubwa wa maneno na misamiati.

Sasa linapokuja suala la kuhusu pombe, au divai au mvinyo ni lazima tujue kwamba lugha zetu zimeandika neno mvinyo, au divai tu in general na hii ni kwasababu haikuwa na utajiri wa maneno wa kuweka au kutofautisha matumizi ya maneno haya kama ilivyokuwa kwenye kiyunani na kiebrania.

Maneno haya DIVAI au MVINYO katika lugha zetu yameandikwa kawaida tu divai, au mvinyo kiasi huwezi kutofautisha ni divai ipi iliyokuwa ikiongelewa hapo.

Ni sawasawa na kwetu mtu akiongelea neno mbuzi, ni rahisi mtu kujua kuwa hapa anaongelea mnyama au kifaa kwasababu ni lugha yetu na tunajua tofauti zake, lakini Biblia zetu zimeandikwa tu Divai, au mvinyo ni ngumu kwetu kujua alikuwa akimaanisha aina ipi kwasababu hiyo si lugha yetu.

Zabibu zilikuwa zikitengenezwa na kuleta vitu mbalimbali mfano juice, dawa, mikate ya zabibu kavu (ENAB) na kadhalika.


1TIMOTHEO 5:23 inapozungumzia juu ya magonjwa tayari kinachozungumziwa hapo ni mvinyo ambao ni dawa na wala sio mnyinyo ambao ni kilevi.

Jiulize jee, kwa ulimwengu wetu huu leo wanywao pombe wanakunywa kama dawa? Hebu sasa tuangalie majina ya aina kadhaa za divai au mvinyo kwa lugha za asili za Biblia, hii inaweza kutusaidia kidogo kuelewa kuhusu jambo hili.

TIROSH

Tirosh, properly "must," translated "wine" _divai "Hii ni juice iliyokamuliwa kutokana na zabibu/divai mpya MITHALI 3:10. Sehemu nyingi MUNGU anawaambia watu walete sadaka ya divai. Matumizi ya divai ukiangalia katika lugha za asili neno lililotumika ni TYROSH, likimaanisha si kilevi bali ni juice. Ona mifano michache hapa
ISAYA 65:8 – Tyrosh ni divai mpya ambayo wakulima waliita Baraka, KUMBU2 12:17 – Dhaka ya divai (Kumb 28:51); "new wine" divai (Mithali 3:10 "sweet wine").

Sidhani kama katika maandiko hayo MUNGU alikuwa akiagiza aletewe kilevi. Among the blessings promised to Esau Genesis 27:28 mention is made of "plenty of corn and tirosh." Canaan is called "a land of corn and tirosh" Kumb 33:28 ; Compare Isaiah 36:17 ) Kanaan iliitwa nchi ya ngano na divai(tirosh). Najaribu tuu kuwaza na sioni kama MUNGU angeita kilevi baraka. hahaahaa

YAYIN

Huu ni mvinyo/divai iliyochachuka, ni neno la ujumla wake lakini ili kujua tofauti, mahali popote ambapo MUNGU aliagiza sadaka ya mvinyo au kuagiza mtu atumie mvinyo hajatumia neno YAYIN bali ametumia neno TIYROSH. Hutumika pia kwa jina la MESEKH a properly a mixture of wine and water with spices that increase its stimulating properties. Mifano ya maandiko yanayoongelea YAYIN kama kilevi Isaya 5:22 "The wine [yayin] is red; it is full of mixture [mesekh];" MITHALI 23:29-30 , "mixed wine;" Icho ni kilevi kilichotokana na zabibu na mazao mengine. Na Mungu ameweka marufuku.

Pia Yayin kabla haijachacha kuwa kilevi ilitumika kama juice, ile siku inapokamuliwa toka ktk shinikizo la zabibu(yaani mashine ya kuproces zabibu kuwa divai) ilikuwa ni kijengo cha chini kilichotengenezwa kwajili kuziponda au kuziganyaga zabibu mpk zinakuwa ujiuji na kukamuliwa divai. Ilikuwa ni kazi kubwa kutengeneza divai mpk iwe nzuri na yenye ladha kinywani. Ndo maana Yesu alivyotengeneza divai ktk harusi ya Kana kwa kutumia maji, ilikuwa mujiza na ikawa yenye ladha tamu na nzuri kwa wanywaji. Kwaiyo Yesu hakutengeneza kilevi.

SHEKAR

Hii imetajwa kama kileo chenye nguvu, kilikuwa ni kileo chenye kutengenezwa kwa mchanganyiko mbalimbali, na hii pia ni pombe by origin meaning. Rejea

MUHUBIRI 2:3
ISAYA 5:22
MAMBO YA WALAWI 10:9 , "Do not drink wine [yayin] nor strong drink [shekar];"
HESABU 6:3 ;
WAAMUZI 13:4 - 7
ISAYA 28:7 (in all these places rendered "strong drink").
ISAYA 5:11 ; 24:9 ; 29:9 ; 56:11-12 lees
Mithali 20:1

Mafungu yote hayo yanaonesha divai ya kileo(strong drink) ambayo Mungu alipiga marufuku(Isaya 5:22, Waefeso 5:18). Ole wao walio hodari kunywa kileo chenye nguvu....(Isaya 5:22) Msilewa kwa mvinyo ambao ndani yake kuna ufisadi(Waefeso 5:18)

ASHISHAH

Huu ulijulikana kama mkate wa zabivu, Soma ( 2 Samuel 6:19 ; 1 Nyakati 16:3 ; Hosea 3:1 ), which, however, rather denotes a solid cake of pressed grapes, or, a cake of raisins

UTAJUAJE KUWA HII NI SAHIHI AU SI SAHIHI?

Hata kama huna uhakika wa jambo kama ni sahihi au siyo sahihi basi angalia matunda/matokeo ya jambo lile ndipo utajua kama ni sahihi au siyo sahihi kunywa pombe. Rejea
MITHALI 23:29-35
MATHAYO 7:17-18

Je matokeo ya kunywa pombe ni nini?

Rejea

MWANZO 9:20-23 Nuhu pombe ilimfanya kuvua nguo na kuwa uchi kiasi cha kulaani familia yake.

MWANZO 19:30-36 Lutu pombe ilimfanya kulala na binti zake kiasi cha kuwapa mimba.

MATHAYO 24:45-51/1WAKORINTHO 6:10 Wanywao pombe wataangamia ajapo Yesu.

Nje ya katazo la biblia pombe ni hatari kwa afya yako, na inaleta umaskini na zinaa na uharibu wa jamii na familia. Hosea 4:11

Unaweza kuwa unywi pombe ila unawanunulia wengine pombe, basi tambua una hatari ""imeandikwa "ole wake yeye ampaye jirani yake kileo....Habakuki 2:15

Mtu apendaye anasa atakuwa maskini; Apendaye "mvinyo" na mafuta hatakuwa tajiri. Mithali 11:17. 18 Tena msilewe kwa mvinyo, ambamo mna ufisadi; bali mjazwe Roho; Waefeso 5:18. Ole wao walio hodari kunywa kileo...Isaya 5:22

Amani ya Bwana iwe nawe.
hayo ni ya agano jpya au la kale?
 
Back
Top Bottom