Elibariki Kingu: Kwa hili la RC wa Dar, naomba niwe wa kwanza kufukuzwa CCM

Nilisema Nitanyamaza lakini Nimeshindwa. Nimethibitisha bila mashaka Clouds kuvamiwa na Rc akiwa na ulinzi na askari wenye silaha mpaka kwenye matangazo.

Najua hofu mliyonayo watanzania juu ya huyu Rc.

Ikiwa mamlaka zitaendelea kufumbia macho.Mimi Elibariki Immanuel Kingu mbunge wa CCM nitakuwa wa kwanza kufukuzwa CCM kama kupinga matendo maovu ya Rc huyu itaonekana ni usaliti kwa nchi.

Haiwezekani Rais wetu atukanwe kila kona kwa matendo ya mtu huyu.

Wana CCM ukimya wetu kwenye hili halikubaliki.

Magufuli juzi ametuliza Dodoma kwa kuongea kwa hisia.Idara za usalama kweli mmeamua kuacha tutukanwe?

Naomba sasa niweke kumbukumbu sawa najua mnamchafua kila anayempinga RC huyu kwa matendo yake ambayo yanakiuka utawala bora.

Naomba niwe wa kwanza kufukuzwa CCM kwa kumpinga Rc Makonda

Elibariki Immanuel Kingu
Mbunge.
Tanzania yetu hiii
 
Saa nne za usiku bwana wewee ulienda wapi, saa nnne za usiku daudi wewe ulienda wapi. Kama ni malumba mbona askari, kama kwenye kick mbona na bunduki....HAINA KINGA, HAINA SINDANO WAFYWAAAA...by remmy ongara the rejendari
 
Rais asilalamike achukue hatua ndiyo uungwana.Unapofuga mbwa akawa mwizi anaelaumiwa na majirani ni mwenye mbwa.Mkuu usifumbie macho mambo kama haya,yanayokuabishia serkali yako.Makonda siyo bora kuliko TANZANIA.Sheria inapokuwa na pande mbili eti kisa wengine siyo wa chama chako siyo sawa.Na kwa Makonda usimpe wakati mgumu mkuu wa nchi kaa pembeni ili Rais apate muda wa kufikiria mambo ya msingi siyo sasa anafikiria atakusaidiaje.KUONDOKA SIASA SIYO MWISHO WA MAISHA MAKONDA KAA PEMBENI RAIS WETU APUMUE.
 
Hili Sakata lingekuwa Kenya mwanaharakati kama Okiya Omtata au Boniface Mwangi au mwananchi yeyote angefungua kesi mahakamani kwa challenge uteuzi huo kwa misingi ya tuhuma hizo... Kwa sababu katiba inaruhusu mwananchi yeyote kufungua kesi dhidi ya afisa wa Umma... Mnachotakiwa kufanya kama watanzania ni mmoja wenu kupata ujasiri na kufungua kesi na katika hiyo kesi ofisi ya Mwanasheria mkuu iunganishwe kadhalika Tamisemi na asasi nyingine husika.... Hizi kelele za mitandao ni za chura tu.... Basi nani was kujitolea afungue kesi mbele ya Hakimu Mfawidhi Kisutu???
 
Je, walivyoingia kwenye chumba cha kurushia matangazo walionekana live na viewers?
 
Makonda atatumbuliwa soon ila si kwa tuhuma ambazo sisi tubazikomalia....hii ishu ya kuvamia clouds ni planned ili wapate sababu ya kumtumbua.Hivyo makonda atatumbuliwa kwa kosa la uvamizi na wala si vyeti wala rushwa.Period
 
Nilisema Nitanyamaza lakini Nimeshindwa. Nimethibitisha bila mashaka Clouds kuvamiwa na Rc akiwa na ulinzi na askari wenye silaha mpaka kwenye matangazo.

Najua hofu mliyonayo watanzania juu ya huyu Rc.

Ikiwa mamlaka zitaendelea kufumbia macho.Mimi Elibariki Immanuel Kingu mbunge wa CCM nitakuwa wa kwanza kufukuzwa CCM kama kupinga matendo maovu ya Rc huyu itaonekana ni usaliti kwa nchi.

Haiwezekani Rais wetu atukanwe kila kona kwa matendo ya mtu huyu.

Wana CCM ukimya wetu kwenye hili halikubaliki.

Magufuli juzi ametuliza Dodoma kwa kuongea kwa hisia.Idara za usalama kweli mmeamua kuacha tutukanwe?

Naomba sasa niweke kumbukumbu sawa najua mnamchafua kila anayempinga RC huyu kwa matendo yake ambayo yanakiuka utawala bora.

Naomba niwe wa kwanza kufukuzwa CCM kwa kumpinga Rc Makonda

Elibariki Immanuel Kingu
Mbunge.
Hii kauli yako inatakiwa pia ifatwe na wana CCM wengine hasa mawaziri, wabunge, na nk.. Haiwezekani RC afanye vitendo hivi na wanachama wa CCM wasitoe maoni yao eti utakuwa usaliti. Usaliti na haki ya mwanachama kutoa maoni ni vitu viwili tofauti. CCM wanavyoendelea kukaa kimya kwa vitendo kama hivi kwa kumuogopa rais nchi hii itaelekea pabaya. Swala la kuwaadhibu raia kwa kuwa na maoni tofauti halina nafasi 2017.
 
Huu ni msiiiba,mwenye nyumba inaonyesha ana maslahi na huyu Madereva, mungu wa Dar es Salaam
 
Ipo siku mtoto pendwa atatajitangazia uongozi wa nchi hii studio , kwa mwenendo huu dekezwa. Teh teh teh.
 
Kingu anatafuta Kiki, tekeleza ilani katika Jimbo lako, Makonda yuko Dar, wewe upo Singida mbona hakuna uhusiano.
 
Back
Top Bottom