Elewa kwamba; Ni Tanzania Pekee ndiyo Tuna mambo haya!

dmkali

JF-Expert Member
Nov 17, 2014
11,284
21,397
Ukitaka kujua mafanikio hufichwa ndani ya akili "Tambua hili"
  • Ni Tanzania pekee Mtoto akitiwa mimba mzazi atahusishwa kuwajibishwa.
  • Ni Tanzania pekee bidhaa za ndani zina bei kubwa au sawa na za kutoka nje.
  • Ni Tanzania pekee wenye kusikilizwa ni sampuli ya watu kama Lemutuz
  • Ni Tanzania pekee ukiwa kiongozi unajua kila kitu , siasa usikilizwe wewe, misiba wewe, ujenzi wewe, michezo wewe, usalama wewe n.k
  • Ni Tanzania pekee profesa hadi anafikia kustaafu anajiona yuko jalalani wakati huo anafundisha vijana namna ya kujiajiri
  • Ni Tanzania pekee Timu ikifungwa anaelaumiwa ni kocha peke yake, na ikifunga anapongezwa mchezaji.( naomba kufafanua hapa)
    • Inakuwaje unamlaumu kocha kwa matokeo mabovu ukamsahau waziri wa michezo? Waziri wa michezo ndiye Mwenye dhamana ya michezo, ikiwemo na kusaka na kuibua vipaji kokote vilipo
    • inakuwaje unamlaumu kocha peke yake ukamsahau waziri wa elimu anaeshindwa kuibua vipaji mashuleni kwa umitashimta
Ni Tanzania pekee kwelikweli!!
 
Back
Top Bottom