Electronics (PC, Phones, TVs ....) easy fixes... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Electronics (PC, Phones, TVs ....) easy fixes...

Discussion in 'Tech, Gadgets & Science Forum' started by Lizzy, Sep 9, 2011.

 1. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #1
  Sep 9, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Juzi nilimwagia laptop yangu kinywaji kidogo ikaniletea mizengwe haswa.

  Ilijizima alafu kila nikijaribu kuwasha inawaka kwa sekunde kadhaa alafu inajizima yenyewe...sikujua kama inahusiana na kile kinywaji maana nlishafuta juu juu sikujua kama kiliingia mpaka ndani.
  Nikafikiria kuomba ushauri hapa ila nikajua inaweza kuchukua muda mpaka mtu anaelielewa tatizo hilo ajitokeze kwahiyo nikazamia Google. Took a while kupata majibu ila nilifanikiwa.

  Sasa nikapata idea...kwanini nisifungue thread ambayo itakua maalum kupeana utaalam wa haraka haraka ambao mtu mwenyewe anaweza kuutumia kurekebisha simu, tv, pc na vikorokoro vingine bila kupeleka kwa fundi.
  Mtu akisoma hii thread anaweza kujifunza vitu alafu siku ikitokea akahitaji moja ya hayo maujanja anakua tayari anajua au angalau anafahamu wapi pa kuyapata kirahisi na kwa lugha rahisi maana sio wote tunaoelewa kiingereza vizuri .

  Kwahiyo mi ntaanza na chache.

  1.Ukimwagia kifaa chochote cha umeme DON'T KEEP IT ON.
  Kitu cha kwanza kizime, toa kwenye umeme kama umechomekwa alafu toa betri kabla ya kuangalia hicho kimiminika kimeingia mpaka ndani au la. Baada ya hapo futa kile unachokiona kwa macho ...ukimaliza kama una feni itumie kupuliza kifaa chako kukisaidia kukauka, au weka kwenye jua, na uache kwa muda kabla ya kurudisha betri na kuangalia kama umefanikiwa au la.

  2.Computer yako ikiacha kutoa sauti ghafla/ microphone ikiacha kufanya kazi angalia sounds setting kuhakikisha kwamba kila kitu kipo kama kinavyotakiwa. Yaweza kua ulibadilisha settings bila kujua...
  Ukiona kwamba kila kitu kiko sawa na bado inasumbua basi inawezekana SOUND CARD yako ina matatizo hivyo install nyingine.Zimejaa tele online ni kiasi tu cha kusearch SOUND CARD free download inayoendana na program unayotumia.

  3.Laptop yako ikikataa kucharge ...unplug the charger...toa betri alafu plug charger.Then izime...rudisha betri..washa uangalie kama kunamabadiliko. Kama bado inakataa tafuta betri nyingine ujaribu maana tatizo laweza kuwa kwenye betri.

  4.PC ikiwa slow sana angalia kama umejaza sana vitu uisafishe (delete usivyohitaji..hamisha unavyohitaji).

  6. Ukidownload movie ikakubali kucheza ila ikakwambia kwamba hutoweza kupata AUDIO kwasababu ''The file contains a track in the Dolby AC3 Audio code 8192'' ingia online tafuta AC3 FILTER FREE DOWNLOAD and you are good to go.

  7. ..............
   
Loading...