Electro Dance Music (EDM) | Special Thread

Leo'Get To Know° 1 | Robin Schulz

Robin Schulz ni DJ, Programmer, Songwriter, Record Producer na Fashion designer alizaliwa 28 April 1987, Osnabrück, Germany

Robin anafahamika vizuri kutokana na kazi zake zilizoshika chart kubwa kote ulimwenguni, mfano wa kazi hizo ni;

• Speechless wimbo ulioingizwa sauti na dada Erika Sola huku ukiwa umesimamiwa na kusambazwa na "TONSPIEL" - WEPLAY Music na Warner Bros Germany

• Oh Child wimbo ulioshirikisha Piso 21 kutoka Mexico. Ndio wimbo pekee wa Robin uliyotiyarishwa na waandaji 5 kutokea viunga na studio za WEPLAY Music huku ukisimamiwa na Warner Bros Music, Warner Bros Mexico na WEPLAY Music. Wimbo huu uliweza kushika chart za muziki wa dance ya Kielektroniki katika mataifa 37 duniani.

• Mfano wa kazi nyingine ni Waves, Lost, Odum na nyinginezo

Ni moja ya watayarishaji muziki anayetumia 'Intro Live Guitar', Electric Piano na Keyboard pasi ya msaada wa vifaa vya Kielektroniki.

Robin Schulz mwaka 2017 aliweza kuachia filamu inayohusu maisha yake, katika filamu hiyo walijitokeza wasanii kama Axwell and Ingrosso, Micha Moor, Erika, Lost Frequencies, David Guetta na Cheat Codes.

Q/S au "Q/S Designed by Robin Schulz" ni brand ya mavazi na vifaa mbalimbali yaani "Merchs" kutoka kwake Robin Schulz. Brand hii inasambazwa ulimwenguni kote chini ya mwavuli wake mwenyewe na TONSPIEL.

Robin Schulz muda mwingi ambao hatokuwa na 'Music Tour' utamkuta katika jiji la Cologne nchini Ujerumani akichakata kazi zake.

Huyo ndio Robin Schulz kwa ufupi
Mfano wa kazi nyingine ni Waves

Jamaa kautendea haki wimbo wa Mr Probz kwa kuuremix
 
Rudimental - Feel The Love
Rudimental - Waiting All Night
Feint - Shock Wave
Calvin Harris - Feel So Close
Calvin Harris - Sweet Nothing
Calvin Harris - Thinking About You
David Guetta ft Kid Cudi - Memories
David Guetta - Every Chance We Get We Run
Taio Cruz - Higher
Taio Cruz - Take Me Back
mule mule kiongoz
 
Nimedownload mix zao ambazo ziko kuanzia lisaa karibia album nzima
Kuna website moja napenda kudownload nyimbo mbali mbali za EDM

Aisee uzi nimeukubali.

NoCopyrightSounds [NCS] artist wao nao siyo poa kwenye upande wa EDM.

Kuna ngoma moja hivi ya melodic dubstep naikubali sana.

XAIA, RAIN MAN & OLY - BREAKDOWN [NCS]
 
Kugo-logo.png

&
images (1).png
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom