Electrical technician natafuta kazi

CHIN

Member
Sep 20, 2017
28
45
Wakuu namatumaini yangu mu wazima wa afya.

Nisiwachoshe sana kichwa cha habari kinajieleza,nimemaliza masomo yang ya elimu ya kati katika fani ya uhandisi umeme kutoka DIT,naomba mwenye chanel yoyote ya kazi hata kwa muda anisaidie tafadhari.

Naomba kuwasirisha.
 
Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
22,338
2,000
Wakuu namatumaini yangu mu wazima wa afya.
Nisiwachosha sana kichwa cha habar kinajieleza,nimemaliza masomo yang ya elimu ya kati katika fani ya uhandisi umeme kutoka DIT,naomba mwenye chanel yoyote ya kazi hata ya muda anisaidie tafadhari.
Naomba kuwasirisha.
Ungesema kwa uwazi...

FTC, ADE au BSc. Eng...

Elimu ya kati ndo ipi?
 
vvm

JF-Expert Member
Jul 18, 2014
3,947
2,000
Wakuu namatumaini yangu mu wazima wa afya.
Nisiwachosha sana kichwa cha habar kinajieleza,nimemaliza masomo yang ya elimu ya kati katika fani ya uhandisi umeme kutoka DIT,naomba mwenye chanel yoyote ya kazi hata kwa muda anisaidie tafadhari.
Naomba kuwasirisha.
Endelea kutafuta mkuu mi sijasoma hii kitu lakini ndio kazi yangu kudeal na proteus
 
JUAN MANUEL

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
2,833
2,000
Wakuu namatumaini yangu mu wazima wa afya.
Nisiwachosha sana kichwa cha habar kinajieleza,nimemaliza masomo yang ya elimu ya kati katika fani ya uhandisi umeme kutoka DIT,naomba mwenye chanel yoyote ya kazi hata kwa muda anisaidie tafadhari.
Naomba kuwasirisha.
Tembelea makampuni ambayo yanafanya Power maintainance ya telecom towers,huko kazi huwa ni nyingi,jaribu NETIS wapo mwanza,Camusat wanaofisi dar ila shughuri zao nyingi zipo mbeya,Reime wapo dar,shughuri zao zipo mtwara.Maktech.Pivotech.NEWL

Hayo makampuni yana ofisi dar,ila shughuri zao nyingi zipo mikoani.
Ni muhimu kuwa na leseni ya udereva.

Haya makampuni,ni Mara chache kutangaza kazi,inabidi uwe unatembelea ofisi zao,unaacha document zako.usitume kupitia emails.

Fika mwenyewe kwenye ofisi zao,ulizia HR,au unampa barua hata mlinzi,aipeleke kwa HR.
 
Shukrani mkuu
 
TAREO TANZANIA

New Member
Oct 9, 2020
1
20
Wakuu namatumaini yangu mu wazima wa afya.
Nisiwachosha sana kichwa cha habar kinajieleza,nimemaliza masomo yang ya elimu ya kati katika fani ya uhandisi umeme kutoka DIT,naomba mwenye chanel yoyote ya kazi hata kwa muda anisaidie tafadhari.
Naomba kuwasirisha.
TANGAZO LA NAFASI YA KAZI:
CHUO CHA UFUNDI KIDT KINAHITAJI MWALIMU/MKUFUNZI WA FANI YA UMEME NA UJENZI:
SIFA: AWE NA DIPLOMA AU UZOEFU NA UWEZO WA KUFUNDISHA VIJANA WA LEVEL 1 HADI 3
ELIMU: MWENYE EIMU YA DIPLOMA KATIKA FANI YA UMEME NA UJENZI AU INYO ENDANA
MASOMO ATAKAYO FUNDISHA NA KAZI ATAKAZO KUWA ANAFANYA.
1. Masomo ya umeme /ujenzi.
2.Kusimamia na kufundisha
3.Kusimamia na kufundisha masomo ya ziadaikiwa ni Eng maths. Technical drawing....
Mwenye usoefu na anaye weza kufanya kazi hizi anaweza kuwasiliana na mkuu wa chuo
MAWASILIANO : 0717157640 /0754469894
TUSAIDIE KUFIKISHA UJUMBE HUU KWA WADAU WOTE.
KARIBU KIDT VTC TUJENGE AJIRA KWA VIJANA WOTE
 
Kumbo El Capitanol

JF-Expert Member
Jun 16, 2016
285
250
Naombeni kuuliza..level II ni diploma au cheti??kwa upande wa umeme
Yes ni cheti mkuu! kwenye hizi kozi za Engineering kwa level ya Diploma kuna mfumo wa kuanzia NTA level 4 (Basic Technician certificate) kwa mwaka wa kwanza ,NTA level 5 (Full Technician certificate) mwaka wa pili na NTA level 6 (Ordinary Diploma certificate) mwaka wa tatu .
 
mwanaNjilo

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
281
250
Naombeni kuuliza..level II ni diploma au cheti??kwa upande wa umeme
Vocational Technical Award (VTA) Level ll haiwezi ikawa astashahada (cheti) au stashahada (diploma). Hiyo ni category tofaut ya Academic award. Ukimaliza VTA level l, ll na lll (ambazo zinakua accredited na VETA) unaweza ku apply ukasome ngazi ya astashahada (yaani Cheti/ NTA Level 4).

I stand to be corrected!
 
senegro orgenes

Senior Member
Apr 26, 2017
196

Inamana wanavyosema ajira za electrical technician!!means hata wa level II wa veta anaweza kuomba iyo kazi??
 
mwanaNjilo

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
281
250
Inamana wanavyosema ajira za electrical technician!!means hata wa level II wa veta anaweza kuomba iyo kazi??
VTA Level ll huezi ukawa electrical technician ndugu. Unahitaji qualifications zaidi ili uwe techniacian. Taasisi kama Tanesco wana ajiri Electrical Technician kwa qualifications za Bachelor's degree. Kuna waliopata bahati miaka hiyo ya nyuma wakaajiriwa katika kada hiyo akiwa na Diploma.

Mark hivi vitu: VTA & NTA. Hizo ni level tofauti za award. Kama una hold VTAs (Level l, ll, lll) ni tofauti na holder wa NTAs (Level lV, V, VI, VII, VIII, IX).

I stand to be corrected!
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
5,780
2,000
You are very correct
Vocational Technical Award (VTA) Level ll haiwezi ikawa astashahada (cheti) au stashahada (diploma). Hiyo ni category tofaut ya Academic award. Ukimaliza VTA level l, ll na lll (ambazo zinakua accredited na VETA) unaweza ku apply ukasome ngazi ya astashahada (yaani Cheti/ NTA Level 4).

I stand to be corrected!
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
5,780
2,000
VTA Level ll huezi ukawa electrical technician ndugu. Unahitaji qualifications zaidi ili uwe techniacian. Taasisi kama Tanesco wana ajiri Electrical Technician kwa qualifications za Bachelor's degree. Kuna waliopata bahati miaka hiyo ya nyuma wakaajiriwa katika kada hiyo akiwa na Diploma.

Mark hivi vitu: VTA & NTA. Hizo ni level tofauti za award. Kama una hold VTAs (Level l, ll, lll) ni tofauti na holder wa NTAs (Level lV, V, VI, VII, VIII, IX).

I stand to be corrected!
Hapa upo sahihi kiasi fulani ila kuna mahali umekosea.
Hapo uliposema Tanesco wanaajiri Technicians kwa level ya Bachelor degree ni uongo na hakuna kitu kama hicho.
Wanaajiri Technician kwa level ya Diploma na Engineer kwa level ya Bachelor degree miaka yote.
 
mwanaNjilo

JF-Expert Member
Aug 30, 2018
281
250
Hapa upo sahihi kiasi fulani ila kuna mahali umekosea.
Hapo uliposema Tanesco wanaajiri Technicians kwa level ya Bachelor degree ni uongo na hakuna kitu kama hicho.
Wanaajiri Technician kwa level ya Diploma na Engineer kwa level ya Bachelor degree miaka yote.
Sawa. Ndomana nikasema: I stand a correction!

Swali moja kwako: Techician na Engineer ni kada moja au tofauti? Ukinipa jibu, naomba niambatanishe swali jingne: Nikweli Engineer na Technician waajiriwa kwa qualification moja wapo kati ya Diploma na B. Degree (kama ulivosema)?
 
mbu wa dengue

JF-Expert Member
Jun 2, 2014
5,780
2,000
Sawa. Ndomana nikasema: I stand a correction!

Swali moja kwako: Techician na Engineer ni kada moja au tofauti? Ukinipa jibu, naomba niambatanishe swali jingne: Nikweli Engineer na Technician waajiriwa kwa qualification moja wapo kati ya Diploma na B. Degree (kama ulivosema)?
Japo swali lako halipo clear na sijakuelewa umelenga kitu gani ila nitajitahidi kulijibu kama ifuatavyo.
Ukisikia mtu ni Engineer means ana Bachelor degree in Engineering.
Ukisikia mtu ni Technician means ana Diploma in Engineering ingawa siku hizi kuna fani zingine kama pharmacy pia wanatumia hili neno Technician wakimaanisha ni mtu mwenye Diploma ya pharmacy.
Artisan ni yule fundi mwenye cheti cha Veta.
Hizi ndio common definitions za kidunia.
Lakini ukija kwenye mambo ya ajira kwenye makampuni kila kampuni ina mpangilio wake.
Usishangae siku ukiona tangazo la kazi linamuhitaji Engineer lakini elimu yake iwe ya Diploma au Wakasema wanamtaka Technician lakini elimu yake iwe Bachelors Degree,Au wakasema wanamtaka Technician lakini elimu yake iwe cheti cha veta.
Hiyo isikuchanganye ni makampuni binafsi huamua kufanya hvyo kutokana na kukwepa maslahi fulani.
 
senegro orgenes

Senior Member
Apr 26, 2017
196
250
Duuu sasa mdogo wangu ata ajiriwa wapi??maana nimemwambia mpaka level II???
Je na hawa ARTISAN??ndio level gani
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom