EL,AC na RA Fanyeni Haya | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

EL,AC na RA Fanyeni Haya

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by eedoh05, Jun 17, 2011.

 1. e

  eedoh05 JF-Expert Member

  #1
  Jun 17, 2011
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 633
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 45
  Mh. Edward Lowassa, Andrew Chenge na Rostam Aziz, sikilizeni ushauri wangu. Inawezekana mmeshapata ushauri mwingi na toka kwa watu mbali mbali. Mimi ninawashauri hivi, (kwa kuwa naamini mliyoyafanya/ au hamkufanya kwa ajili yenu tu, bali kwa ajili ya wenzenu-CCM):
  1. Jitokezeni hadharani, semeni ukweli wenu wote, msimung'unye maneno. Semeni jinsi mlivyohusika, na nani mlihusiana nao. Kweli milele humweka mtu huru.
  2. Mtubu mbele za Mungu wa Mbinguni na mbele ya watanzania kwa yote yaliyosemwa na yanayosemwa juu yenu.
  3. Mnapojitokeza kusema yote ,msiseme haya mengine ni nyeti (ni kwa usalama wa taifa). Taifa haliwezi kuwa salama, uovu, uongo, kulindana kunapozidi. Uvumi na manung'uniko yanapozidi. Hadi sasa usalama wa nchi uko mashakani. Lolote laweza kutokea muda wowote kweli isiposimama mahali pake..
  Mkifanya hayo, mtu yeyote atakayeinuka kuwasema atakuwa kioja. Msiiogope CCM,kwani ccm sio mlango wa kuingia mbinguni. Kumbuka, kama yanayosemwa juu yenu yote ni kweli, hamkuyafanya kwa ajili yenu, bali mliyafanya kwa ajili ya ccm au viongozi wa ccm. Sasa ni kwa nini ccm imewageuka kiasi hicho?

  Fedha za EPA kwenda Kagoda inasemwa ndizo zilimwezesha JK na ccm kushinda uchaguzi wa mwaka 2005 na kwa sehemu fedha hizo hizo (mtaji huo huo) umewarejesha JK na ccm madarakani katika uchaguzi wa 2010. Ushindi huo wa mara mbili (2005/2010) wa CCM ulichangiwa na juhudi zenu binafsi. KIMANTIKI, KILA MWANA CCM ''wana-magamba' ALIYESHANGILIA NA ANAYESHANGILIA USHINDI HUO NA KULINGA NA KUTEMBEA KIFUA MBELE ANASHANGILIA FAULO MLIYOFANYA, NA ANATAMBA NA KUJISIFU KWA UOVU HUO.

  SASA, INAKUWAJE ZIGO LOTE LA LAWAMA MTUPIWE NINYI WATATU TU? MIPANGO YOTE YA USHINDI NA MIKAKATI YA KUSHINDA ILIFANYIKA NA CC YA CCM ILIYAPA BARAKA. HILO ZIGO LA KUCHAFULIWA NI LAO WOTE
  WANAOJIJUA KUWA NI WANA CCM.

  Ninyi tubuni, hao wengine wabaki na zigo lao. Kisha mwone Mungu aliyehai akitenda katika maisha yenu yote. Kumbuka kisa cha Zakayo mtoza ushuru katika Biblia Takatifu.
   
Loading...