Ehud Olmert jela kwa miaka sita

Ehud Olmert jela kwa miaka sita

mwekundu

JF-Expert Member
Joined
Mar 4, 2013
Posts
22,475
Reaction score
21,046
[h=1]Ehud Olmert jela kwa miaka sita[/h]
120105105947_jp_olmert304x171_nocredit.jpg


Mahakama moja nchini Israel imempa kifungo cha miaka sita jela aliyekuwa waziri mkuu nchini Israel Ehud Olmert kwa kosa la kupokea hongo.
Bwana Olmert alipatikana na hatia mwezi machi katika kile kilichojulikana kama 'swala la eneo takatifu' ambapo hongo ilitolewa ili kuharakisha ujenzi wa majumba ya kifahari mjini Jerusalem.
Kiongozi huyo alikuwa ameondolewa mashitaka katika kesi tofauti zilizokuwa zikimkabili.
Mashitaka yaliomkabili yalitekelezwa wakati Olmert alipokuwa meya wa mji wa Jerusalem na baadaye akiwa waziri wa serikali.
Ehud Olmert alimrithi Ariel Sharon kama waziri mkuu mnamo mwaka 2006 baada ya Sharon kuugua ugonjwa wa kiharusi.
Alijiuzulu mnamo mwaka 2008.

source; Ehud Olmert jela kwa miaka sita - BBC Swahili - Habari
 
Back
Top Bottom