Efatha wamjibu kinana..

Efatha wamjibu kinana..

hp4510

JF-Expert Member
Joined
Jan 16, 2012
Posts
8,244
Reaction score
8,533
Bodi ya wadhamini ya huduma ya Efatha, ambao ni wamiliki wa shamba la Efatha, imemjibu katibu mkuu wa CCM, Abdulrahamn Kinana kutokana na kauli yake kuwa atahakikisha Serikali inanyang'anya shamba hilo na kulirejesha kwa wananchi.

Katika taarifa yake kwa umma, bodi hiyo imesema mbali na kuwa hawakubaliani na uamuzi huo, wanahoji kama mpango ni kuwapa wananchi shamba hilo, ni lini wao (Efatha) wamekoma kuwa wananchi wa Tanzania.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa baadhi ya waumini wa Efatha ni wanachama wa CCM na wengine ni wafanyakazi wa Serikali iliyopo madarakani,hivyo nao ni wananchi wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Efatha, shamba hilo la Malonje lenye ukubwa wa hekta 15,000 lilikuwa linamilikiwa na Shirika la Maendeleo ya Mifugo (DAFCO) na kwa mujibu wa sera ya ubinafsishaji iliyopitishwa na Serikali lilikabidhiwa kwa PSRC ili waliuze.

Baada ya kutotokea mnunuzi, PSRC waliamua kutenga sehemu iliyokuwa na miundombinu,lakini bado hakutokea mnunuzi ndipo walipoamua kulikabidhi shamba hilo kwa Wizara ya Maendeleo na Mifugo na Maji mwaka 2003.

Inaongeza taarifa hiyo kuwa mwaka 2004 wizara ililikabidhi shamba hilo kwa Mamlaka ya Mkoa wa Rukwa ili kuligawa katika vipande vidogo ambavyo vingeuzika jambo ambalo pia lilishindikana.

Inazidi kufafanua mwaka 2007, Serikali iliitisha kongamano la wawekezaji na Efatha walipata mwaliko na fursa ya kuomba kununua hekta 10,000 za shamba hilo kwa ajili ya kilimo na mifugo, ombi lililokubaliwa kwa kununua shamba hilo kwa bei ya Sh600 milioni.

Wiki iliyopita akiwa ziarani mkoani Rukwa,Kinana alisema atahakikisha shamba la Efatha alilodai limepokonywa kwa nguvu, linarejeshwa kwa wananchi kwa madai kuwa Rais Kikwete alishatoa agizo la kupatiwa hekta 8,000.
 
Sasa na wao wanapoteza muda kujibishana na huyu. Kwa zile mashine za kufulia nguo za hospitali yetu ziko wapi?
 
Bodi ya wadhamini ya huduma ya Efatha, ambao ni wamiliki wa shamba la Efatha, imemjibu katibu mkuu wa CCM, Abdulrahamn Kinana kutokana na kauli yake kuwa atahakikisha Serikali inanyang'anya shamba hilo na kulirejesha kwa wananchi.
Katika taarifa yake kwa umma, bodi hiyo imesema mbali na kuwa hawakubaliani na uamuzi huo, wanahoji kama mpango ni kuwapa wananchi shamba hilo, ni lini wao (Efatha) wamekoma kuwa wananchi wa Tanzania.
Taarifa hiyo imeeleza kuwa baadhi ya waumini wa Efatha ni wanachama wa CCM na wengine ni wafanyakazi wa Serikali iliyopo madarakani, hivyo nao ni wananchi wa Tanzania. Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Efatha, shamba hilo la Malonje lenye ukubwa wa hekta 15,000 lilikuwa linamilikiwa na Shirika la Maendeleo ya Mifugo (DAFCO) na kwa mujibu wa sera ya ubinafsishaji iliyopitishwa na Serikali
lilikabidhiwa kwa PSRC ili waliuze. Baada ya kutotokea mnunuzi, PSRC waliamua kutenga sehemu iliyokuwa na miundombinu, lakini bado hakutokea mnunuzi ndipo walipoamua kulikabidhi shamba hilo kwa Wizara ya Maendeleo na Mifugo na Maji mwaka 2003.
Inaongeza taarifa hiyo kuwa mwaka 2004 wizara ililikabidhi shamba hilo kwa Mamlaka ya Mkoa wa Rukwa ili kuligawa katika vipande vidogo ambavyo vingeuzika jambo ambalo pia lilishindikana.
Inazidi kufafanua mwaka 2007, Serikali iliitisha kongamano la wawekezaji na Efatha walipata mwaliko na fursa ya kuomba kununua hekta 10,000 za shamba hilo kwa ajili ya kilimo na mifugo, ombi lililokubaliwa kwa kununua shamba hilo kwa bei ya Sh600 milioni.
Wiki iliyopita akiwa ziarani mkoani Rukwa, Kinana alisema atahakikisha shamba la Efatha alilodai limepokonywa kwa nguvu, linarejeshwa kwa wananchi kwa madai kuwa Rais Kikwete
alishatoa agizo la kupatiwa hekta 8,000.
 
hao efatha ndio wanakata wananchi maskio?? Shamba lazima ligawe kwa wananchi, ardhi ikae bure kwa babu zip??

kwa sababu hao Efatha sio wanainchi?
 
Utendaji wa Kinana hauna tofauti na utendaji wa wapinzani.Kile ambacho kinatakiwa kifanywe na wapinzani yeye ndiye anacho kifanya.Anafanya Kazi ya kuipinga serekali utafikili kilichofanyika hakijafanywa na serekali yake.Kinana atakuwa ana kiandaa chama chake ili kitakapo kuwa chama pinzani kisipate shida ya kuipinga serekali itakayo kuwa madarakani kipindi hicho.
 
Bodi ya wadhamini ya huduma ya Efatha, ambao ni wamiliki wa shamba la Efatha, imemjibu katibu mkuu wa CCM, Abdulrahamn Kinana kutokana na kauli yake kuwa atahakikisha Serikali inanyang'anya shamba hilo na kulirejesha kwa wananchi.

Katika taarifa yake kwa umma, bodi hiyo imesema mbali na kuwa hawakubaliani na uamuzi huo, wanahoji kama mpango ni kuwapa wananchi shamba hilo, ni lini wao (Efatha) wamekoma kuwa wananchi wa Tanzania.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa baadhi ya waumini wa Efatha ni wanachama wa CCM na wengine ni wafanyakazi wa Serikali iliyopo madarakani,hivyo nao ni wananchi wa Tanzania.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo ya Efatha, shamba hilo la Malonje lenye ukubwa wa hekta 15,000 lilikuwa linamilikiwa na Shirika la Maendeleo ya Mifugo (DAFCO) na kwa mujibu wa sera ya ubinafsishaji iliyopitishwa na Serikali lilikabidhiwa kwa PSRC ili waliuze.

Baada ya kutotokea mnunuzi, PSRC waliamua kutenga sehemu iliyokuwa na miundombinu,lakini bado hakutokea mnunuzi ndipo walipoamua kulikabidhi shamba hilo kwa Wizara ya Maendeleo na Mifugo na Maji mwaka 2003.

Inaongeza taarifa hiyo kuwa mwaka 2004 wizara ililikabidhi shamba hilo kwa Mamlaka ya Mkoa wa Rukwa ili kuligawa katika vipande vidogo ambavyo vingeuzika jambo ambalo pia lilishindikana.

Inazidi kufafanua mwaka 2007, Serikali iliitisha kongamano la wawekezaji na Efatha walipata mwaliko na fursa ya kuomba kununua hekta 10,000 za shamba hilo kwa ajili ya kilimo na mifugo, ombi lililokubaliwa kwa kununua shamba hilo kwa bei ya Sh600 milioni.

Wiki iliyopita akiwa ziarani mkoani Rukwa,Kinana alisema atahakikisha shamba la Efatha alilodai limepokonywa kwa nguvu, linarejeshwa kwa wananchi kwa madai kuwa Rais Kikwete alishatoa agizo la kupatiwa hekta 8,000.

Huyu Mwingira anafahamika na serikali sijui kama Kinana ameona hii kitu
Mtume na Nabii Josephat Mwingira asaidia maendeleo mkoa wa Rukwa

30/05/2009 by Strictly Gospel
22
mwingira.jpg

Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kiongozi wa kanisa la Efatha nchini, Mtume na Nabii, Josephat Mwingira katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Rukwa iliyoongozwa na Rais kwenye hoteli ya Kilimanjaro- Kempinski jijini Dar May 27, 2009. Zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zilichangwa,Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
Ahsante mkuu kwa picha ... kinana arudi kwa JK. Akajipange upya.
 
Huyu Mwingira anafahamika na serikali sijui kama Kinana ameona hii kitu
Mtume na Nabii Josephat Mwingira asaidia maendeleo mkoa wa Rukwa

30/05/2009 by Strictly Gospel
22
mwingira.jpg

Rais Jakaya Kikwete akipokea mchango wa shilingi milioni 10 kutoka kwa kiongozi wa kanisa la Efatha nchini, Mtume na Nabii, Josephat Mwingira katika harambee ya kuchangia Mfuko wa Maendeleo wa Mkoa wa Rukwa iliyoongozwa na Rais kwenye hoteli ya Kilimanjaro- Kempinski jijini Dar May 27, 2009. Zaidi ya shilingi bilioni 1.4 zilichangwa,Katikati ni Waziri Mkuu, Mizengo Pinda.

(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Kama kuna mtu ana account ya Kinena ya FB au Twitter mtumpieni hii picha.

Kinena hajawahi kuongea pointi hata siku moja!
Kinena ni mtu aliyelewa na madaraka na Fedha za kifisadi zinazotokana na uuzaji wa Pembe za ndovu. Efatha wanatakiwa kumpuuza!
 
mwingira ni mjasiriamali wa kidini.

kwani sheria inasemaje? tatizo hawaongi? viongozi wa ccm rukwa wanataka kula. kama ni kukata watu masikio kwani kwa nini haichukui mkondo wake? tatizo jingine ni chadema tangu tuanze kuwasikia viongozi wetu wanasumbuka sana na kufikia hata kula hadharani. natamani chadema ifilie mbali.
 
hao efatha ndio wanakata wananchi maskio?? Shamba lazima ligawe kwa wananchi, ardhi ikae bure kwa babu zip??
Kulingana na taarifa yao wamenunua eneo hilo kwa shillingi 600,000,000/- iwapo watanyang'anywa hizo fedha atazirudisha nani?
 
Sasa anajibu hoja za wananchi kama nani kwenye serikali hii huyo kinana??
 
Back
Top Bottom