Ee bwana kasi ya mzee wa monduli inatisha....!

Ee bwana kasi ya mzee wa monduli inatisha....!

Olaigwanani lang

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2012
Posts
547
Reaction score
183
wapendwa wana jamvi kwa jinsi E.L anavyokwenda kwa spidi kali namna hii anatisha...mimi najiuliza mbona mtu kama mengi,pinda,jk na wengineo hawaalikwi tena kabisa katika harambee..?
jana tuu nilisikia kachangisha milioni 200 huko karatu...

ni nini hasa tafsiri ya haya anayotenda kwani najiulizaga sipati jibu.....
 
Ni wema wa mtu tu,sio lazima uitwe kwenye haraambee,unajitokeza mwenyewe na kusaidia. Mengi na wengine hawana roho za kutoa.
 
kabla ya kujibu nini tafsiri ya matendo yake, ni vema pia tukatafakari wapi anapata fedha hizo wakati wengine hata nauli ya daladala hawapati. unafikiri PINDA, mtoto wa mkulima anaweza kuwa na jeuri hiyo, au JK mtoto wa kikwere
 
Ni wema wa mtu tu,sio lazima uitwe kwenye haraambee,unajitokeza mwenyewe na kusaidia. Mengi na wengine hawana roho za kutoa.

mbona sijasikia anajitokeza kuchangia mradi wowote katika mikoa ya kusini wakati kapelekewa barua kibao za kumuomba achangie?
 
Acha mumuseme Lowasa fisadi. Lakni ikumbukwe tangu miaka ya 1980s' El, alikuwa na pesa na Mifugo.
Sioni sababu ya el kusemwa kuwa Fisadi. Lakn kama ni Ufisadi mbona anatulipa kwa njia ya harambee?
Kama kuna mwenye data atwambie El aliiba kiasi gani? Na mpaka sasa kwenye Harambee zake tangu aanze ameshachangia jumla kiasi gan?
EL IS JEMBE.
 
mpaka sasa karejesha asilimia 0.002 tu ya alichoiba
 
napenda staili yake ya kujitolea, ni mtazamo wangu
 
naona MACHADEMA kutwa ya leo mmeshinda kumtakasa EL. naona ule mkakati wenu wa kuanzisha Jamhuri ya Kaskazini unaendelea na mmemchagua yeye ili awe rais wenu wa kwanza
 
mpaka sasa karejesha asilimia 0.002 tu ya alichoiba

Mkwele karudisha asilimia ngapi alizoiba? Au anaendelea kuzichota tu za Wajinga na sasa kenda kuwaleta wachina waliosalimisha maisha ya mwanae kuwalipa fadhira kwa mali yetu!
 
wanaoitisha harambee shida yao ni hela tu hawana muda wa kuangalia maadili ya mtu, hela kwanza!
 
wapendwa wana jamvi kwa jinsi E.L anavyokwenda kwa spidi kali namna hii anatisha...mimi najiuliza mbona mtu kama mengi,pinda,jk na wengineo hawaalikwi tena kabisa katika harambee..?
jana tuu nilisikia kachangisha milioni 200 huko karatu...

ni nini hasa tafsiri ya haya anayotenda kwani najiulizaga sipati jibu.....
Hawamualiki yeye ila wanazialika hela zake... Ikitokea akaishia hataalikwa
 
Huyu alikuwa na pesa na mifugo hata kabla ya uwaziri mkuu wanaokumbuka tangu enzi za mwl.akaenguliwa kwa sababu ya utajiri eti ataiuza nchi.Kama sasa anazo za wizi basi kheri ya huyu anayewahurumia na kuwakumbuka aliowaibia kuliko wengine WAIBAO NA KULA NA FAMILIA ZAO TU HATA RAFIKI HUWAGEUKA.ni mawazo yangu tu wakuu.
 
Kule facebook pia mzee yuko active sana, E.L
 
Wana JF, mnyonge mnyongeni lakini haki yake mpeni. Edward N Lowasa alijiuzulu uwaziri mkuu kwa sababu ya kuwajibika tu na wala si kwamba aliiba pesa ya Richmond.

Lowasa ni tajiri tangu zamani sana, na utajiri wake ni wa kupewa na wazazi wake na mwingine ametafuta mwenyewe na kwa njia halali kabisa. Lowasa ni mchapa kazi na pia ana vision nzuri. Kuna kipindi huko nyuma alikuwa si waziri wa wizara yoyote, na muda huo aliutumia kufanya biashara zake halali kabisa na alilipa kodi kama ipasavyo.

Katika hizi harambee anazoitwa si kwamba anatoa mapesa yote hayo, anachofanya ni kwamba anawaomba marafiki zake wa ndani na nje ya Tanzania wachangie harambee hiyo. Juzi kwenye hiyo harambee lowasa na rafiki zake walitoa Tsh 10M tu ambazo hata mimi na wewe tunaweza kuzitoa bila ya kujiuliza mara mbili na hizo nyinginezo zilichangwa na watu wengine.

Kuitwa kwa Lowasa kwenye hizo harambee pia kunatokana na kipaji cha uhamasishaji alichokuwa nacho. (Gift from GOD).
Kuna watu wengi wanaweza kuitwa lakini ukweli ni kwamba jamaa ana kipaji ya kuongea vizuri na watu na anakubalika vyema.

Kama Lowasa atagombea kiti cha uraisi 2015 kwa dhamana ya CCM ,mimi kama Kidatu, nitakuwa mstari wa mbele kabisa kumpigia kampeni ili ashinde kiti hicho, bila malipo yoyote. Lowasa ni mchapa kazi, yuko tayari kufanya maamuzi magumu hata kama yatawaumiza watu kwa lengo lililo bora kwa Taifa letu, ni mkweli, mwadilifu, hana woga, ana mapenzi ya kweli na nchi yake, anawapenda watanzania wote bila kujali dini, umri, rangi na itikadi za kisiasa. Lowasa hana haya ya kuwaonea haya wazembe na wapuuzi.

Ingekuwa ni hekima kumshukuru kwa haya anayoyafanya kwa jamii badala ya kumshutumu na kumsema vibaya.
 
Back
Top Bottom