wapendwa wana jamvi kwa jinsi E.L anavyokwenda kwa spidi kali namna hii anatisha...mimi najiuliza mbona mtu kama mengi,pinda,jk na wengineo hawaalikwi tena kabisa katika harambee..?
jana tuu nilisikia kachangisha milioni 200 huko karatu...
ni nini hasa tafsiri ya haya anayotenda kwani najiulizaga sipati jibu.....
Huyu alikuwa na pesa na mifugo hata kabla ya uwaziri mkuu wanaokumbuka tangu enzi za mwl.akaenguliwa kwa sababu ya utajiri eti ataiuza nchi.Kama sasa anazo za wizi basi kheri ya huyu anayewahurumia na kuwakumbuka aliowaibia kuliko wengine WAIBAO NA KULA NA FAMILIA ZAO TU HATA RAFIKI HUWAGEUKA.ni mawazo yangu tu wakuu.
Ni wema wa mtu tu,sio lazima uitwe kwenye haraambee,unajitokeza mwenyewe na kusaidia. Mengi na wengine hawana roho za kutoa.
USIPOTAKA JUA NINI TAFSIRI YAKE HUTAWEZA FUMBUA AKILI YAKO...lowasa hajachangia milioni 200 Karatu ila LOWASA amewaza kuhamasisha/kuendesha/kufanikisha hiyo harambee mpaka zikapatikana hizo Ml 200+,kwa hiyo hata mtoto wa mkulima au mfugaji kama anushawishi angeweza itwa na akafanikisha,bahati mbaya hao watu uliowataja hawana uwezo wa kuhamasisha/kuendesha/kufanikisha harambe na wananch/wadau wakachangia kiasi hicho.kabla ya kujibu nini tafsiri ya matendo yake, ni vema pia tukatafakari wapi anapata fedha hizo wakati wengine hata nauli ya daladala hawapati. unafikiri PINDA, mtoto wa mkulima anaweza kuwa na jeuri hiyo, au JK mtoto wa kikwere