Edward Sokoine, Salim A. Salim & Edward Lowassa

Edward Sokoine, Salim A. Salim & Edward Lowassa

Mwanamageuko

JF-Expert Member
Joined
Oct 31, 2010
Posts
8,596
Reaction score
5,584
Hayati Sokoine alikuwa mbunge wa Monduli na pia Waziri Mkuu. alikuwa na muono wa kuivusha Tanzania kutoka tulipokuwa kwenda kwenye mafanikio, ndio maana akahimiza nguvu kazi na kuwabana watendaji wazembe na wasiowajibika katika kazi zao ndio MAANA WAKAMCHUKIA (mengine ambayo yalisemwa baada ya kufariki kwake siwezi kuyaandika sina ushahidi nayo hata kama ni kweli!) TAIFA LILIHITAJI KIONGOZI AINA YA SOKOINE WAKATI ULE HATA SASA ILI TUTOKE TULIPOKWAMA. ALIGUNDUA TATIZO NI MFUMO, MIPANGO YA OVYO NA MATUMIZI MABAYA SERIKALINI. Akawaaga Dodoma akiwaambia "Tutakutana Dar es Salaam..." hakufika Dar es Salaam mauti yakamfika ndoto tulizokuwa nazo zikafutika. MOLA AMLAZE MAHALA PEMA.

Salim Ahmed Salim, akiwa Waziri Mkuu alienda ziara mikoa ya Kusini na kuwakuta watu wazima hawana nguo wanastiri nyuchi kwa vipande vya magunia na ngozi, hali ilikuwa mbaya bila kujali MFUMO aliondosha amri na kuruhusu MITUMBA iingie nchini ili watanzania wastiri aibu zao. Achilia mbali nini alikifanya akiwa waziri wa ulinzi kwa askari jeshi. Alipotaka kuwa rais (NA NDIYE ALIYEFAA kutokana na kuijua nchi na muono wake) MFUMO ulimpiga chini kwa maslahi ya MFUMO si MASLAHI YA NCHI NA VIZAZI VYAKE. Mengi alizushiwa na kimya akakaa. Pole sana Mzee SAS. JAPO MFUMO UMEKUSAHAU SISI Tunakukumbuka na Mola atakulipa.

Edward Lowassa akiwa waziri mkuu alijua tatizo kubwa ni elimu, utendaji na uwajibikaji kwenye ofisi za umma. Wenyewe watendaji wa ovyo timbwili lake wanalijua. MFUMO ULIPOTENGENEZA KILIMO KWANZA YEYE ALIWAAMBIA ELIMU KWANZA AKIAMINI BILA ELIMU HAKUNA KILIMO. HUU NDIO ULIKUWA MUONO SAHIHI NA HITAJIKA KWA NCHI HII.

Sipendi kusema mengi ni jukumu letu kutafakari nani anatufaa baina ya WENYE MUONO au ambao wanasema HAWATAWAANGUSHA.

KOSA LOLOTE TUTAKALOLIFANYA LITAGHARIMU VIZAZI VYETU KARNE NYINGI KULIKO TUNAVYODHANI.

TANZANIA NDIO NCHI YETU, TUMEKWAMA MIAKA MINGI JE NI NANI ANATUKWAMUA?

NI JUKUMU LETU MIMI, WEWE NA YULE.
 
Mhe. Lowasa ndiye rais. Makufuli anafaa kwa barabara tu. Hana uchungu na taifa lake. Hatujawahi kumsikia akikrmea wizi na ufisadi wa ccm. Huenda naye yupo kwenye mtandao wa waliomweka.
 
Lowasa ndo rais wetu full stop
 
Back
Top Bottom