Edward Lowassa special thread

Wewe ni kiongozi mwenye mamlaka,wewe ni mkweli na kiongozi mvumilivu sana,wewe ni kiongozi ambaye ana weza kuwajibika......NDANI YA CCM hawataki jamii ambayo sio yenye asili ya sahel hivyo unaweza kuwa rais wa ardhi hii ya babu yako kupitia chama kingine.Hivyo fanya mazungumzo ya kina na UKAWA ili mkomboe nchi hii.Ujio wako ukawa itawaongezea UKAWA nafasi ya kushinda.

Una nyota ya urais ni juu yako kushawishi maadui wako wawe marafiki na kujiaminisha.

Usiende katika chama ambacho ndio unakwenda kukijenga.Angalia hiyo.
 
Ukawa with Lowasa pamoja na wapambe wake imekufa. Walioko ukawa si watafuta vyeo wala maslahi. Ni watu ambao wako tayari kuumia kuona nchi hii inatoka kwenye lindi la umaskini! Lowasa is for power and money. Wapi na Wapi Akishindwa huko ccm basi aende waliko kina Malecela, Msekwa, Msuya na wengine. Huo ndo uungwana!
 
Mimi nasubiri mpango mbadala.wa mh.LOWASA

huwezi kutumia mabilioni ya fedha halafu ukawa huna mpango mbadala.
Tusubiri tuone.
 
Mimi nasubiri mpango mbadala.wa mh.LOWASA

huwezi kutumia mabilioni ya fedha halafu ukawa huna mpango mbadala.
Tusubiri tuone.

Naona wenye timu yao wameukimbia huu uzi aisee, hapo sasa ndio tutajua kama ni mtu wa watu ama vipi maana zile harambee alizokuwa anashiriki kama ni za heri basi ataendelea kushiriki huku akisaidiana na marafiki zake kuleta mabadiliko lakini asipoendelea nadhani timu yake itajua kwamba huo ulikuwa ni mpango maalumu
 
Kiongozi yyt maskini atakaechaguliwa hapo Tz ataiendesha nchi hii kifisadi tu.
Mtu mwenye Njaa ni vigumu sana kumjali masikini mpk ashibe yeye kwanza.

Hamuoni mifano ya nchi za wenzetu? Mchagueni Slaa muone balaa hapa nchini.
 
Kwisha kazi lowasa ata kugombea ubunge tena ni aibu kwake....wampe ubalozi nje akapumzike au aachane na siasa alishaonja nafas ya juu ya uwazir mkuu atulie tu
 
Kiongozi yyt maskini atakaechaguliwa hapo Tz ataiendesha nchi hii kifisadi tu.
Mtu mwenye Njaa ni vigumu sana kumjali masikini mpk ashibe yeye kwanza.

Hamuoni mifano ya nchi za wenzetu? Mchagueni Slaa muone balaa hapa nchini.

Kinyume chake, mafisadi ndio hawashibi. Hata hivyo ndugu yangu, Rais wa kwanza alikuwa maskini, angekuwa na tamaa angeweza kufanya lolote baya. Sifa inayotakiwa hapa ni roho na dhamira safi kwa taifa lako. Mengine yote mlikuwa mnadanganywa tu ili afike ikulu, yeye na maswahiba wakahomole. Tumshukuru Mungu kwa kutuepushia hilo balaa.
 

PIA mshauri akatubu kwanza, halafu atangaze na kuachana na ufisadi pamoja na kwakana maswahiba mafisadi
 
Jonh p m kaoa jirani na kwetu, nijiandae
kuwa usalama wa taifa, hahaaa nishaula
mazee
 

Team EL mmeshinda kwa lipi wakati jamaa ndio kashakosa uraisi hivyo na kwa taarifa ndio kashapotea kwenye system na no room ya yeye kurudi tena in the future.

Sijui ushindi wenu ni kuunga mkono mtia nia mwenza na EL au ilikuwa mnapambana kwa nguvu zote na vurugu za pesa kubwa kuhakikisha El anashinda.

Polee weeeeeeeeeeeeeeeee. Mwenzeni Pombe yuleeeeeeeeeee kama chopa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…