Edward Lowassa na Mbowe acheni ubinafsi

mmbangaya

JF-Expert Member
Jan 16, 2015
997
1,763
Habari Jf,

Naomba kabla ya kutoa hoja yangu nideclare interest kwamba mimi ni mwana Ukawa damu.

Baada ya uchaguzi mkuu kumalizika viongozi wa ukawa wakiongozwa na Lowassa na Mbowe walituambia kwamba CCM wameiba kura na hawajashinda kihalali.

Wakatuambia kwamba haki yao haiwezi kupotea wanaenda kuishtaki serikali ya CCM kwenye mahakama za kimataifa ikiwepo ICC na CCJ.

Cha kushangaza baada ya hapo hawajarudi kwa watanzania tuliokuwa tunaunga mkono sera zao kutupa feedback.
Instead wamekaa kimya kama hawapo.

Hii inapelekea watanzania kuamini yale maneno ya wapinzani wenu kwamba baadhi ya viongozi wa UKAWA ni wachumia tumbo. Inamaana nyie siyo aina ya viongozi mnaowajibika kwa waliowatuma.

Je, kura zetu zingetosha mngerudi hata kutushukuru? Au mnadhani 2020 ni mbali sana?

Imani yetu kwenu inaenda kuyeyuka kabisa sasa.
 
Habari Jf,
Naomba kabla ya kutoa hoja yangu nideclare interest kwamba mimi ni mwana Ukawa damu.
Baada ya uchaguzi mkuu kumalizika viongozi wa ukawa wakiongozwa na Lowasa na Mbowe walituambia kwamba ccm wameiba kura na hawajashinda kihalali.
Wakatuambia kwamba haki yao haiwezi kupotea wanaenda kuishtaki serikali ya ccm kwenye mahakama za kimataifa ikiwepo icc na ccj.
Cha kushangaza baada ya hapo hawajarudi kwa watz tuliokuwa tunaunga mkono sera zao kutupa feedback. Instead wamekaa kimya kama hawapo.
Hii inapelekea watanzania kuamini yale maneno ya wapinzani wenu kwamba baadhi ya viongozi wa ukawa ni wachumia tumbo. inamaana nyie siyo aina ya viongozi mnaowajibika kwa waliowatuma.
Je kura zetu zingetosha mngarudi hata kutushukuru? Au mnadhani 2020 ni mbali sana?
Imani yetu kwenu inaenda kuyeyuka kabisa sasa.

Nadhani umekurupuka au umekurupushwa, hivi hujui waliandaa mkutano tr8 ambao ulipigwa marufuku? any way nenda Arusha Leo wanamkutano
 
Nadhani umekurupuka au umekurupushwa, hivi hujui waliandaa mkutano tr8 ambao ulipigwa marufuku? any way nenda Arusha Leo wanamkutano

afadhali mkuu umemwambia kidogo niwengi wa aina yake wapo.
maana wengi ni kulalamika tuu lkn hawafuatilii mambo kiundani.kiukweli ni kuwa mikutano ya kampen kwenye majimbo yanayofanya uchaguzi sasa yatatoa majibu ya Yale waliyotaka kuyasema jangwani
 
Mimi nafikiri tusubiri hao viongozi watafakari kwanza na siyo kulazimisha waseme cha msingi ni amani tuliyonayo, au ulitaka aseme tuandamane?
 
Mimi nafikiri tusubiri hao viongozi watafakari kwanza na siyo kulazimisha waseme cha msingi ni amani tuliyonayo, au ulitaka aseme tuandamane?

Acha kuwapa watu nguvu ambayo hawana, fisadi Lowasa na Mbowe hawana uwezo wa kuvunja Amani TanZania kama wangekuwa nawo kwa jinsi fisadi Lowasa alivyokuwa na uchu wa madaraka angeshautumia tayari kuifanya nchi isitawalike!
Hivyo huwo uwezo hawana ila wanachofanya ni kuwadaganya manyumbu yao kwamba hawataki kuvuruga Amani wakati ukweli ni kwamba hawana uwezo wa kuvuruga Amani TanZania!
 
kuweza kushika dola ni mpango mkakati ambao unahitaji muda wa kutosha kuufanikisha. Usidhani kwa aina hii ya kukurupuka na kutaka kupata urais itawezekana.
The point is watu wanahitaji feedback na way forward ya kupata mabadiliko ya kweli.
kama siyo tamaa tuu ya kutaka urais unadhani kama mtu unapenda mabadiliko ya kweli ukiokosa urais unatulia tuu unasubiri after five years unakuja na slogan mpya?
Unadhani kutoa feedback lazima maandamano au mikutano ya hadhara kwamba press conference nazo zimezuiliwa?
Kwa namna hii ya zima moto ikulu mtakuja kupasikia tuu ukawa. mafanikio yoyote yanahitaji investment ya time and money.
Need some change of your mind people
 
Back
Top Bottom