Edward Lowassa mwenye nyota ya mfalme

Edward Lowassa mwenye nyota ya mfalme

Ng'wanangwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2010
Posts
10,827
Reaction score
4,184
Edward Ngoyai Lowassa mwenye nyota ya mfalme ndiye Rais wa Jamhuri ajaye.

Akiwa mwenye haiba yenye mvuto usiomithilika, Edward amedhihirisha kuwa yeye ni mwamba wenye imara. Amewabadilisha wengi nikiwemo mimi. Ninampenda mno na hakika ndiye mtu sahihi tuliyepewa na Mungu kuinasuwa Tanzania kutoka katika makucha ya kikundi cha wanyonyaji kilichojificha katika mwavuli wa chama kinachoitwa ccm. Lazima nimpigie kura inyeshe isinyeshe kura yangu ni kwa Edward.

Mwenye maneno machache
Edward hana porojo. Anajuwa watanzania tumeshadanganywa sana na sasa inatosha. Haihitaji kutumia dakika 30 au saa nzima kutamka watanzania wanapaswa sasa kupata elimu bure kuanzia darasa la kwanza hata chuo kikuu. Kwa nini isiwezekane katika nchi yenye madini kila namna? Nchi yenye vivutio vya utalii unaoingiza mabilioni ya shilongi? Nchi yenye hazina ya gesi na urani? Inawezekana. Edward anajuwa anagombea nafasi ya juu kabisa katika uongozi wa nchi na imempasa kutoa ahadi ambazo ana uhakika zinatekelezeka. Tarehe 25 nenda ukampigie kura Edward tuondoe utawala wa kipuuzi wa chama cha mapinduzi.

Makini...
Hana papara Edward. Ametulia tuli kimwili lakini akili yake ikifanya kazi mithili ya mifumo ya computer maarufu kama server. Mifumo ya namna hii huwa haizimwi na hakika Edward hazimiki...yupo nasi tupo naye maana yake Alipo Tupo. Tutampigia kura.

Mcha Mungu...
Edwardd ameyaishi maisha ya mateso ya mwenye haki. Akiwa raia wa Tanzania na Waziri Mkuu wa Zamani, Edward amepita katika tanuru la moto akichezewa rafu na watu wa chama cha ccm. Wakijiaminisha kuwa hawezi kuwa Rais wa Jamhuri kwa kuwa wao tu wanamchukia. Yeye aliita 'chuki iliyokithiri juu yangu'. Hakika haya ni mateso na ccm walijuwa walikuwa wakimtesa na kudhani wamemmaliza. Walichokuwa wamepotoka ni kushindwa kujuwa kuwa Edward anayo haki tena ya kikatiba ya kugombea nafasi ya urais. Ndiyo kusema mateso yake yamekuqa mateso ya mwenye haki na hakika mateso ya mwenye haki huponywa na Mungu. Edward atashinda Urais Oktoba 25 kwa sababu Mungu yupo upande wake. Siku zote Mungu husimama na mwenye haki. Kampigie kura Edward tarehe 25.

Kama alivowahi kusema Jakaya: Tanzania bila Ukimwi inawezekana, nasi tuseme Tanzania bila ccm inawezekana.

Na kama wanavyosema malaria haikubaliki tushirikiane kuitokomeza basi imetupasa kusema tukijiamini Ccm haikubaliki tushirikiane kuitokomeza.

Kwa Mungu ninakuombea Edward uwe Rais wangu wa Awamu ya Tano.
 
Safi sana Mkuu. Andiko limetulia sana na umemwelezea Lowassa vyema sana
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom