Edward Lowassa arejea CCM, apokelewa na Uongozi wa juu wa chama

Nshawai kuwaambia humu humu kuwa Kuing,oa ccm madarakani kwa mwenendo huu wa wanasiasa wa Chadema kuhama hama vyama na kukimbilia ccm haitokuja tokea, labda kizazi cha vitukuu wetu hapo ni angalau!!

Katiba imekaririwa kuwa Tanzania imara ni ya chama cha mapindunzi kwahyo someni vifungu na mvielewe!

Asanteni sana

Ndini mtuwatu asiye mwanachama!

wakati ukuta.
 
Eti mihemko yenu! Akina nani hao! Hebu tuachane na huu usutanaji! Good day
Usijifanye wewe ndiye unapata uchungu wa kuachwa hata Ccm nao waliachwa na Lowasa na wakaumia.

Mmeruhusu siasa ziwe sehemu ya maisha yenu acha ziwaendeshe.
 
Usijifanye wewe ndiye unapata uchungu wa kuachwa hata Ccm nao waliachwa na Lowasa na wakaumia.

Mmeruhusu siasa ziwe sehemu ya maisha yenu acha ziwaendeshe.
Aiseee! Nadhani nimemaliza! Kila la kheri! Nilidhani tunajafili sorry wrong bus! Siendi huko unakoelekea
 
Un
Unazungumzia umati??? Hatuzungumzii huo tunazungumzia madhara yatakayotokea kwa watu wanaomwona role model
Ninyi mnamkuza sana huyo Ng'ombe
Ningeweza kuwazuwia jf yote wasingemjadiri kwa lolote,hata maccm yangeleta mjadala mngewachia wajadiri wao. TOKA LINI LOWASA KAWA ROLE MODAL WA WATU? HUYO KISHAJIDHARAULISHA MILELE

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzeee ulko enda umeenda kucover nafas ya nape( 2015) 2020 utatumika, 2021 utawekwa kwenye trash kama walivyo wekwa wenzio saiv
Yangu macho
Mungu atupe maisha marefu
Ameni
We never stop learning
Dhambi ya kuwasaliti wanyonge n kubwa kulko dhambi zote
Malipo n hapa hapa dunian

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1551759212719.png


NB: Makala hii pia nimeiambatanisha chini.

Na. M. M. Mwanakijiji
Kurudi kwa Lowassa CCM kumewagusa watu kwa namna mbalimbali. Wapo ambao wameshtuka na kuumizwa hasa wale ambao walifurahia kuhamia kwake Chadema wakati wa mbio za uchaguzi mkuu wa 2015 na upande mwingine wapo ambao wameshukuru kurudi kwake “nyumbani”. Wapo ambao wanajisikia hasira na kuona kama wamesalitiwa na wapo ambao wanashukuru kwa sababu wanaona kama hakuwa kweli “mwenzao” na sasa ametoka. Yote tisa, kuondoka kwake kumeacha maswali mengi kwa wengi.
Toka juzi nimepokea simu na messages nyingi zikiwa na maswali na mijadala mingi na kutoka na hilo nimeonelea nijaribu kuyajibu maswali haya mbalimbali na yatokenayo nayo katika kuelezea hili na mawazo yangu.

1. Swali: Unachukuliaje kurudi kwa Edward Lowassa CCM?
Mimi: Kurudi kwake hakukunishtua au kwamba sikukutarajia. Toka alivyoondoka CCM baada ya jina lake kufyekwa kule na kutaka kujaribu bahati yake CHADEMA jambo moja lilikuwa wazi; kama angeshindwa kupata Urais angerudi tu CCM. Kitu ambacho kimenishangaza zaidi ni kuwa ameweza kudumu ndani ya upinzani kwa miaka mitatu na nusu hivi. Hili nitalifafanua kidogo baadaye. Lakini niseme tu kuwa Lowassa sasa ana Amani na ni itakuwa makosa kumtukukana au kumkebehi.

2. Swali: Ina maana basi Lowassa hakuwa mpinzani kweli kweli?
Jibu: Lowassa hakuwa kiongozi wa upinzani kwa maana inayoeleweka. Alikuwa ni “mgombea wa Urais wa upinzani”. Ili kuwa kiongozi wa upinzani ni lazima mtu ajithibitishe kifikra, kiutendaji na kimkakati kuwa anataka kukiondoa chama tawala madarakani. Lowassa aliingia upinzani kwa sababu moja na sababu moja tu – kujaribu kuupata Urais ili kutimiza ndoto yake ya kuwa Rais. Hakuwahi kuonesha kujali yanayotokea upinzani, hakuwa kuunga mkono hoja za upinzani na hajawahi kuwatetea wapinzani muda wote kabla ya kuingia kwake upinzani. Kwa hiyo, kurudi kwake CCM si pigo kubwa au lenye maana sana kwa upinzani wa Tanzania.

3. Swali: Sasa hili linaiacha vipi CHADEMA? Huoni kama CHADEMA imejiweka kwenye wakati mgumu?
Jibu: Kwa kiasi ni lazima wakubali huu wakati mgumu na wakubali kuwa uamuzi wao wa kumchukua Lowassa ulikuwa ni wa mahesabu ambayo mojawapo ya jumla zake ilikuwa ni hatimaye Lowassa kurudi CCM. Kama walidhania kabisa kuwa Lowassa atakuwa mpinzani wa kudumu pamoja nao katika shida na raha basi walijionesha udhaifu mkubwa zaidi kuliko ambayo niliwafikiria. La maana ni kuwa huu si wakati wa kulia; ni wakati kuganga majeraha yao na kusonga mbele.

4. Swali: Huoni kama uongozi uliompokea Lowassa unahitaji kuwajibika?
Jibu: Mojawapo ya udhaifu mkubwa wa upinzani wa Tanzania ni kuwa hauna ujasiri wa kuwajibika. Yaani, watu wanaweza kuvuruga na kuvurugana lakini bado watu wale wale wanataka waendelee kuongoza kwa sababu wanaamini hawatovuruga tena au kwamba hakuna mtu mwingine anayeweza kuchukua nafasi zao. Matokeo yake upinzani wetu bado unaelekea kuangalia kundi la watu unaoweza kuwahesabu kwa vidole kuwa ndio “viongozi wa upinzani” na hawa hawawajibiki, hawawajibishwi na wito wowote wa kutaka wawajibike utaonekana ni kutaka kudhoofisha upinzani.

5. Swali: Sasa ungetaka wawajibike vipi?
Jibu: Kwanza kabisa na kubwa zaidi ningependa kuona Kamati Kuu ya CHADEMA inakaa chini na ikimaliza kikao inakuja na tamko la kukubali makossa na kuwaomba radhi wa Tanzania kwa kuvuruga upinzani mwaka 2015. Hili ni lazima lifanywe. Ni lazima waseme kuwa walikosea; walitaka kutumia njia ya mkato kushinda Urais na walikuwa tayari kusalimu kanuni na misimamo yao ili tu waweze kuingia Ikulu. Waombe radhi.
La pili ni kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA ni lazima ajiuzulu nafasi yake ile kufuatia kurudi kwa Lowassa CCM. Yaani, hawezi, hapaswi, na hatakiwi kabisa kuwa mtu wa kuiongoza CHADEMA kuelekea 2020. Si kwa sababu ni mtu mbaya, si kwa sababu simpendi (nina heshima ya pekee sana kwa Mbowe na mchango wake kwa upinzani) lakini kila jambo lina matokeo; bahati nasibu aliyocheza 2015 sasa imelipa; ameliwa. Kama kiongozi na mwanademokrasia wa kweli ni lazima yeye awajibike kwani ndio kiongozi mkuu wa chama. Anaweza kuendelea na nafasi zake nyingine lakini Chadema mikononi mwake tena haiku salama. Mbowe ni lazima ajiuzulu.

6. Swali: Huoni kuwa Lowassa alileta mchango mkubwa katika upinzani kuliko ule ambao ungeletwa na Slaa kwa mfano?
Jibu: Miaka mitatu baadaye lazima swali liulizwe mchango gani? Sasa hivi upinzani umepoteza hata majimbo uliyoyapata kwa haki. Sasa hivi haiwezi hata kujivunia kuwa “Lowassa kaongeza majimbo”! Wanaweza kusema walipata kura nyingi za Urais kuliko mgombea yeyote wa upinzani kabla. Lakini kura hizo zimewasaidia vipi? Je, zilikuwa ni sababu ya CHADEMA au sababu ya Lowassa; kama ni za Lowassa kwa kurudi kwake CCM hizo kura bado zimebakia CHADEMA? Ukweli ni kuwa mchango wa Lowassa ulikuwa ni wa kwa uchaguzi tu wa 2015 na si nje ya hapo au zaidi ya hapo. Kurudi kwake kumefuta (negate) mchango wowote wa maana kwa maoni yangu.

7. Swali: Unataka kusema Lowassa hakuwa na mchango wowote?
Jibu: La hasha! Mchango wa Lowassa ulikuwa wa muhimu kwa kiasi tu cha kwamba walikuwepo watu ambao walitaka Lowassa awe Rais mwaka 2015. Hawa ni wale waliokuwa kwenye yale makundi makubwa mawili. Makundi ambayo sasa hivi yako njia panda.

8. Swali: Makundi gani hayo?
Jibu: Kwanza kulikuwa na kundi kubwa la “Ulipo Tupo” ambao ni wale wana CCM ambao walizunguka na Lowassa kutafuta udhamini na ambao walijitokeza kwa maelfu kila alikopita kuunga mkono ugombea wake. Ni kundi la wana CCM ambao hawakuona shida kuimba “Tuna Imani na Lowassa” mbele ya Mkutano Mkuu wa CCM. Kundi la wana CCM walioumizwa na kukatwa kwa jina la Lowassa. Hawa walienda na kumpigia kura alikokuweko na naweza kusema hata angeenda chama cha Wakulima wangemfuata maana walikuwa hawafuati sera bali sura!
Na kundi la pili sasa ni la wazungusha mikono wa “Mabadiliko-Lowassa”. Hili lilikuwa ni kundi la wanachama na viongozi wa upinzani ambao walifikiria wamepata hirizi (amulet) ya kuiengua CCM madarakani. Katika ngazi ya chini kabisa hawa ni wale waliodeki barabara na kutandaza kanga njiani ili “masiha” wao apite kuelekea Yerusalemu! Hawakujali alikuwa nani, alisimamia nini, na alitaka kufanya nini; wao walichotaka ni kumuona anaubeba upinzani mgongoni kwake na kuwahakikishia nafasi mahali pema peponi! Katika ngazi ya juu yake walikuwa viongozi wa juu kabisa wa Chadema ambao walijigeuza na kukubali kuuza kanuni zao, misingi yao na ndoto zao ili Lowassa naye awabebe wao pale wao waliposhindwa. Wote wakajikuta wamebadilisha mabadiliko kuwa ni mtu hata kama mtu huyo ni miongoni mwa watu waliosababisha watake mabadiliko hayo! Inanikumbusha kisa cha mbuzi waliolalamika kuliwa na chui mara kwa mara; wakaandaa maandamano makubwa ya kutaka “mabadiliko”. Siku moja mbuzi na wana mbuzi wakajiunga na maandamano hayo na wao wakaimba “mabadiliko”! Halafu mbuzi wakamchukua chui kuongoza mabadiliko hayo!!

9. Swali: Inaonekana kweli CHADEMA walikutibua sana Mwanakijiji?
Jibu: Hawakunitibua mimi hasa; walitibua yote tuliyokuwa tumeyapigania kwa karibu miaka ishirini. Kilichotokea kinaweza kuitwa “Usaliti Mkuu” wa harakati zote za mabadiliko. Ndio maana hata sasa hivi wanapolalamikia serikali na Magufuli binafsi sijawapa uzito unaostahili; kwa sababu sijui kama wanamaanisha, wanatania au wanatafuta tu mahali pa kusimamia.

10. Swali: Huoni kuwa labda upinzani ulilazimika kumchukua Lowassa kwa vile hawakuwa na namna nyingine ya kuweza kushinda uchaguzi?
Jibu: Hapa ndio mgongano mkubwa tuliokuwa nao. Chadema na washirika wake waliamua kutafuta njia ya mkato kushinda uchaguzi. Walitaka kufanya kile ambacho hakijawahi kufanywa na chama kingine cha upinzani duniani – wiki chache kabla ya uchaguzi mkuu kumchukua kiongozi toka chama tawala mwenye tuhuma za ufisadi kuwa mgombea wake wa Urais. Ni kweli walitaka kushinda lakini si kwa gharama hiyo! Na kurudi kwake CCM ndio kunathibitisha ni kwa kiasi gani ule ulikuwa ni uamuzi mbaya sana. Maisha ya watu wengi sana yaliharibiwa, ndoto za wapinzani wengi zilivurugwa, matarajio ya wale waliopigwa na polisi, waliouawa, waliojeruhiwa kwa kutaka mabadiliko. Yaani, hili ni zaidi ya Lowassa na Slaa, hili ni zaidi ya CHADEMA na CCM; lilihusu maisha ya watu. Kuna watu kurudi kwa Lowassa CCM kumewaumiza zaidi kuliko kuingia kwake CHADEMA! Kwamba, baada ya kejeli zote zilizorushwa dhidi yao kwa kumkataa Lowassa leo amerudi kule kule alikokuwa na kuiacha Chadema kwenye mataa yaliyozimika!

11. Swali: Vipi kuhusu CCM na wao kumpokea Lowassa mtu ambaye walimnanga na kulikata jina lake kama kuchinja kibudu; huoni kuwa wao sasa ndio wanaonekana wamekumbatia “mafisadi” kweli kweli?
Jibu: Kwanza kabisa ieleweke kuwa CCM kwa kumpokea Lowassa hawakupoteza kitu. Lowassa kwa kwenda CHADEMA alipoteza kila kitu. Kurudi kwake CCM basi ni bora zaidi kwa Lowassa kuliko hata kwa CCM. Lakini, kama alivyosema yeye mwenyewe kuwa amerudi “nyumbani” na ni kweli amerudi nyumbani. Sasa kama alikuacha nyumbani kubovu na amerudi amekukuta kubovu tatizo siyo yeye bali ni wale walioachiwa nyumbani. Na kama atarudi na kuendelea na nyumba mbovu kwa vile wengine hawataki itengenezwe hilo litakuwa la kwake na wenzake.

12. Swali: Vipi kuhusu ufisadi naona unazungumza kwa misemo tu; CCM wamekumbatia mafisadi?
Jibu: CCM kama chama hakijabadilika. Mojawapo ya vitu ambavyo nimekuwa nivikirudia rudia toka kuchaguliwa kwa Rais Magufuli ni kuwa CCM ni “ile ile”. Ninaposema hili nina maana ya kuwa sera zake hazijabadilika, mtazamo wake kuhusu kutawala haujabadilika, na linapokuja suala la ufisadi katika mfumo wa kiutawala bado makubwa hayajafanyika.

13. Swali: Makubwa gani unafikiri hayajafanyika hadi hivi sasa?
Jibu: Nikianza kuyaorodhesha naweza kuandika kitabu. Kwa ufupi ni kuwa matatizo ya kimfumo bado yapo. Lakini matatizo ya kimfumo yanatoka na matatizo ya kisheria na matatizo ya kisheria yanatokana na matatizo ya kisera. Sera hutangulia mabadiliko ya sheria, na sheria hutangulia mabadiliko ya mifumo na mifumo ndio hutangulia mabadiliko ya jinsi watu wanafanya kazi. Hadi hivi sasa hakujatokea mabadiliko ya kisera ambao ndio msingi wa mabadiliko yote mengine. Na ndio maana nasema CCM ni ile ile.

14. Swali: Unataka kusema kuwa Magufuli hajafanya kitu chochote cha kubadilisha nchi?
Jibu: La hasha! Mabadiliko yote ambayo tunayaona sasa hivi ni kwa sababu ya Magufuli. Ni yeye mwenyewe; ndio maana wakati anawaapisha mawaziri hawa wapya juzi anahoji mambo yanayofanywa na Polisi na usishange siku mbili au tatu baadaye Polisi wanakuja na kitu. Tumeliona hili kwenye mambo ya bandari, TRA, Magereza n.k. Watendaji wanasubiri kuumbuliwa hadharani na Rais, Makamu wa Rais au Waziri Mkuu. Na tumeona hata baadhi ya mawaziri hawajui au hawaoneshi kama wanajua nini wanatakiwa kufanya kiasi cha Rais Magufuli kuwatengua! Sasa haya ni mabadiliko ya Magufuli; lakini kwa vile yanategemea mtu yanatumia nguvu kubwa zaidi. Ni sawasawa na mtu ambaye ameamua kusukuma gari ambalo amelitoa kwenye matope lakini badala ya kuliwasha liende anaamua kuendelea kulisukuma. Litakwenda lakini halitakwenda kama inavyopaswa kwenda kama likiwa limewashwa. Magufuli anajitahidi kusukuma gari na kwenye mteremko linaweza kufikia spidi nzuri tu; lakini lazima ifike mahali gari liwashwe na liende kwa kufuata kanuni za kimekaniki (mechanical laws).

15. Swali: Vipi kuhusu Dkt. Slaa ambaye alirudi CCM na sasa Lowassa ameenda huko huko CCM. Siyo kwamba aliondoka CDM kwa sababu ya Lowassa?
Jibu: Nisiwe mzungumzaji wa Dkt. Slaa kwani anaweza kujisemea mwenyewe. Lakini kwa vile ni rafiki yangu na ninamheshimu labda kuliko mwanasiasa mwingine yeyote Tanzania kwa hivi sasa naweza kusema mambo mawili. Kwanza, Dkt. Slaa hakurudi CCM; aliamua kuachana na “siasa za vyama” kama alivyoelezea katika hotuba yake pale Selena Hoteli. La pili ni kuwa kinyume na watu wengine wanavyochukulia utumishi katika serikali ya Tanzania – ukiondoa nafasi zinazotokana na kuchaguliwa haulazimishi mtu kuwa mwana CCM.

16. Swali: Unafikiri Magufuli anaweza kuteua mtu ambaye si mwana CCM kuwa Balozi?
Jibu: Siyo tu anaweza amefanya hivyo tayari. Na amethubutu kufanya yale ambayo siyo Mkapa wala Kikwete waliwahi kukifanya kwa kiasi hiki nacho ni kuteua watu kutoka upinzani kushika nafasi kubwa za kiuongozi. Kuteuliwa kwa Kitila na kwa Anna Mgwira ni mifano tu. Na siwezi kushangaa au kushtuka akiteuliwa mtu kutoka upinzani kuwa Mkuu wa Mkoa au hata Waziri. Kati ya vitu vingi ambavyo nimevielewa ni kuwa anataka mtu anayeweza kutekeleza kile ambacho Rais anakitarajia.

17. Swali: Lakini Dkt. Slaa hajawahi kurudishi kadi ya CCM na bado anaimilikia na hivyo yeye bado ni mwanachama, sivyo?
Wenye kutoa hoja hii wameamua tu kujitoa ufahamu. Katiba ya CCM (kama zilivyo katiba nyingine za vyama) imeelezea namna gani uanachama wake unakoma. Ibara ya 13:1 ya Katiba hiyo imelieleza hili. Kwa hiyo isipokuwa kama kuna mtu atakuwa ana uthibitisho kuwa a. Dkt. Slaa ameendelea kulipia ada ya chama na kutimiza masharti ya uanachama au b. alipoteuliwa kuwa balozi aliomba uanachama wa CCM tena. Nje ya hapo; kwa kadiri nijuavyo Dkt. Slaa hajarudi kuwa mwanachama wa CCM. Na kwa kadiri ninavyomjua kama ikitokea anataka kurudi CCM atafanya hivyo wazi na akianisha sababu zake za kufanya hivyo. Kujiunga na chama cha siasa ni haki ya kila Mtanzania isipokuwa wale ambao hawaruhusiwi kisheria.

18. Swali: Siwezi kukuachilia bila kukuuliza kuhusu mtu mwingine; Rostam Aziz. Tumemuona Rostam akijitokeza mara mbili hizi tena na Magufuli unachukuliaje hilo hasa kwa vile Rostam alihusishwa sana na ufisadi CCM na pia kuwa karibu sana na Lowassa?
Jibu: Nilisubiri uniulize hili. Kuna mambo kadhaa ambayo yanahitaji kuwekwa vizuri na sijui kama nitakuwa na muda wa kutosha kufafanua kila moja. Kwanza, kama Lowassa alikuwa arudi CCM asingeweza kurudi bila kuungwa mkono na Rostam Aziz. Lakini pia jambo moja kubwa ambalo kutoka na vyanzo vya kuaminika sana ni kuwa Lowassa kweli kabisa hakutaka kurudi CCM. Miezi michache tu nyuma Lowassa alikuwa amejiridhisha kumalizia siasa zake upinzani. Lakini Rostam au RA kama baadhi yetu tunavyomuita amethibitisha kitu kimoja ambacho kinahitaji kufikiria – bado ana nguvu ya ushawishi. Kuna vitu (factors) ambazo vimemfanya Lowassa aamue kurudi CCM – soma jibu langu la mwisho kudokeza mojawapo ya mambo yanayoweza kuwa yamemsababisha Lowassa kurudi CCM kwa ushawishi wa rafiki yake.
Jambo la pili ni kuwa Rostam ana nguvu na ushawishi wa kuweza a. kwenda Ikulu baada ya ndugu yake kuwekwa pingu akatoka huko alikokuwa na b. yeye naye alikuwa ametangaza kuachana na siasa za “majitaka” na akavua vyeo vyake vyote ndani ya CCM. Hivyo, kuonekana kwake hivi juzi kuna tuma ujumbe mmoja mkubwa – kwamba bado anaweza kupiga mluzi na watu wakaitika. Hili ni wazo la kutisha sana.

19. Swali: Unataka kusema RA amemuweka Magufuli almaarufu kama “jiwe” mkononi?
Jibu: Kuna watu wanaweza kuona hivyo na yeye mwenyewe anaweza kufikiria hivyo au kuwafanya watu waamini hivyo. Lakini nitakuambia kitu kimoja kuhusu Magufuli na hili nina uhakika nalo wa asilimia 100; Magufuli si mtu wa kuweza kufikirika amewekwa mkononi; umdharau kwa maangamizi yako mwenyewe. Kuna sababu kwanini Magufuli amemleta karibu Lowassa na Rostam na wengine wameshasahau – na Apson Mwang’onda vile vile. Hawa watatu kuja upande wa Magufuli ni kufanya kile ambacho msemo wa Kiingereza unakielezea – keep your friends close, but your enemies closer yaani weka marafiki zako karibu lakini maadui zako karibu zaidi! Lakini pia nafikiri kuna kitu Magufuli anakitaka kutoka kwa hawa watatu na nadhani naweza kukisia ni kitu gani hasa na wengine wanaweza kuwa tayari wamekikisia.

20. Swali: Ni kitu gani unafikiri Magufuli anakitaka kutoka kwa hawa?
Jibu: Siwezi kulisema kwa sasa.

21. Swali: Unaonaje sasa katika mazingira ya sasa kuelekea 2020 hasa baada ya kurudi kwa Lowassa?

Jibu: Lowassa kwa kweli siyo tishio kuelekea 2020. Angeendelea kubakia upinzani na kuendelea na hoja za upinzani angeweza kuwa ni ‘credible’ figure; yaani mtu wa kuaminika. Sauti yake ingekuwa na nguvu sana. Kwa sasa sioni kama kura za CCM zinaweza kugawanyika jinsi ambavyo zingegawanyika 2015. Hii ina maana kibarua kikubwa mwakani hakitakuwa kwa CCM bali kwa upinzani.

22. Swali: Utamuunga mkono Magufuli kama ulivyofanya 2015 na hasa Lowassa akiwa CCM?
Jibu: Hadi hivi sasa sijaona kwa kiasi kikubwa sababu ya kutokumuunga mkono Magufuli. Tatizo kubwa la CCM bado lipo na hivyo ni namna gani kutafuta uwiano wa mambo haya mawili. Sijui ni kwa kiasi gani Magufuli anaweza kuibadilisha CCM kwa sababu CCM ni ngumu sana; na kama watu wanafikiria kuwa Magufuli ameidhibiti CCM subirini muone wakati utakapofika kumaliza muhula wake wa pili. Mnyukano utakaotokea CCM utakuwa ni wa kukumbukwa! Isipokuwa tu kama kutatokea kitu kikubwa sana 2020.

23. Swali: Una maana gani?
Jibu: Nilisema mwanzoni kuwa ndogo za Lowassa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania zimekufa. Nimesema hapo juu kuwa ujio wa Rostam Aziz sasa hivi na kumrudisha rafiki yake CCM una maana yake. Kumbuka mwanzoni mwa miaka ya 2000 RA alijulikana sana kama “the King Maker” yaani mtu anayewapatia watu “mfalme”. Vipi kama ndogo ya Lowassa kugombea Urais itakuwa ni kama ya viongozi wale waliokuwa tayari kutawala kwa mhula mmoja tu; vipi kama wanaweza kufanya kama kilichofanywa Urusi? Na yakatokea mabadiliko ambayo ndio wameyapigia mahesabu; vipi kama ndogo ya Lowassa kuwa mgombea wa Urais ni ya 2020? Magufuli amekuwa akilalamikia sana ugumu wa kazi ya Urais na ni jinsi gani umekuwa mzigo mkubwa sana kwake kiasi kwamba niliwahi kuandika Makala kuwa kama kweli anaona ni mgumu hivyo Katiba imeweka njia za yeye kuutua; vipi kama tayari ameanza kufikiria kuutua mzigo huo mara moja kwa sababu unakuja na lawama nyingi sana? Hili wazo ukiliendeleza kwa mbali zaidi unaweza kushtuka sana. Labda ndoto ya Lowassa haijazimika kabisa.

24. Swali: Hapa unaenda kuzua mijadala mingine. Vipi kuhusu nafasi ya Lissu maana hatujazungumza lolote kuhusu Lissu na yaliyotokea na nafasi yake kuelekea 2020?
Jibu: Sasa hapa tutaanza mjadala mwingine; hili niulize tena wakati mwingine nina majibu mengine ya kufikirisha. Jambo hili halijaweza kuangaliwa vizuri sana linaangaliwa kishabiki, kihamasa na kihisia zaidi. Kuna mambo mengi.
MWISHO
 

Attachments

  • KURUDI KWA LOWASSA.docx
    125.3 KB · Views: 30
Kwamba RA anaweza kutinga ilkula na ndugu yake akatoka selo.....kunaonesha udhaifu mkubwa sana kwenye utawala wa sheria katika nchi yetu na kwa kweli Jiwe mwenyewe. Kunasema mengi sana kuhusu matumizi mabaya ya madaraka na mfumo wetu wa mahakama. Kesi nyingi dhidi ya upinzani, ni wazi zaidi sasa zina mikono ya wanasiasa.
 
Kwa Eddo:
Kwa uwazi wa nafsi,Eddo ni mtu wangu,jamaa yangu na mtu nayemuheshimu kutokana na aina ya siasa zake enzi zake ndani ya CCM.

Na kwa asili Eddo sio "fisadi",Eddo tabia yake imekuzwa sana na RA,maana miaka hiyo ya 1990's RA alikuwa anatafuta "Political affiliation" ili mambo yake yaende sawa,akawatengeneza Eddo na Check bob,ili mmoja wapo iwe karata yake.

Eddo hakutaka kabisa kabisaaa kurudi CCM,na hajapenda kurudi,AMERUDI TU KWA SABABU YA USHAWISHI WA KINGMAKER...Ni habari ndefu,inayohitaji kupata za chini ya kapeti kwa uhakika kabla ya kuziweka hapa,Eddo kurudi CCM kuna watu maisha yao na biashara zao zimepona!

Katika kitu kilichompa wakati mgumu Eddo ndani ya miezi hii baada ya RA na Jasusi Mkuu mstaafu kuonekana Ikulu,basi nu hili la kurudi CCM.Ninadhani,ni wakati ambao Eddo ameweza kutoa chozi kwa kuitamka ile kauli ya "Nitarudi,ila sitaki mbwembwe nyingi za kunipokea".

Eddo ameisaliti nafsi yake kwa kukumbuka fadhila za marafiki zake waliobanwa na kuminywa kwa ajili ya yeye kurudi nyumbani.

Kwa Mbowe:
Ni moja kati ya maamuzi atakayojutia sana katika historia ya siasa za Tanzania za kimageuzi,hakufikiria mbali zaidi ya kuingia Ikulu kwa njia ya mkato,hata hii ya kulala gerezani ni malipo ya aina ya upinzani alioutengeneza baada ya uchaguzi wa 2015.Kesi za Mbowe na aina ya upinzani baada ya 2015 ni matokeo ya uamuzi wa kumchukua Eddo na kumbandika cheo cha ugombea.Imepoteza ajenda,itikadi,imani na falsafa ya upinzani.Kuelekea 2020,Upinzani watakuwa na ugumu wa kuzungumza ajenda zao kuliko CCM.Siasa haichezwi kwa kubahatisha,wala hakuna kanuni ya siasa inayoakisi kanuni ya kibiashara,kwamba the more the higher capital with risk,the more the higher return with profits.Kumchukua Lowassa ilikuwa ni "risk" ambayo ilianza tu kuwatesa CHADEMA toka siku wamemkumbatia hadi siku ile kamati kuu yote itakapokuwa imeondoka kwenye siasa na vijana wapya kuchukua hatamu.

Kwa Dr Slaa:
Mtu ninayemuheshimu mpaka kifo kitakapotutenganisha,mwanamageuzi wa kweli,mwanafalsafa wa siasa za Tanzania,muadilifu na mjenzi wa hoja huru.Ni pigo la harakati si tu za kuiondoa CCM madarakani,bali kuifanya Tanzania yenye muamko wa kisiasa na elimu ya Uraia.Hawa ndio wale "Majasiri Waongoza Njia katika Siasa".Uamuzi wake pia wa kupokea Ubalozi na utetezi kuwa unaweza kuwa balozi na usiwe mwana CCM ni utetezi dhaifu.Kwa nchi na mifumo ya nchi kama zetu zenye kihoro cha ujamaa,kutenganisha nafasi ya ubalozi na CCM ni kujidanganya.Labda ni sababu ya hasira na kutemwa kwenye urais 2015,lakini Dr alipaswa kuiacha legacy ya uongozi wake ndani ya upinzani kwa kufia upinzani.Huyu na Eddo kuna mahali hawachekani,na kuna vitu wakikaa na kutulia wanajutia maamuzi yao ya pili.

Kwa RA:
Huyu hazuiliki,hashikiki...ni amesharudi uwanjani kuendeleza ufalme wake,huyu ana akili kuliko wanavyomdhania,na kuelekea 2020,sabb kasharudi rasmi,basi nusu ya wabunge wa CCM itakuwa ni matokeo ya kazi ya mikono yake.Huyu ni mwamba...kwanza kuonekana tu Ikulu na oale Lumumba akiwa amesimama na Rais,basi washirika wake kibiashara nje na ndani ya nchi wamerudisha imani kwake 100%.Alimtaka mtu wake 2015 ikashindakana,sasa ameitwa bila yeye kuita.Kwa kweli huyu namkubali kwa fitina zake za kufanikisha mipango yake bila kumkanyaga mtu.Uwepo wake tu pale Lumumba,kama angekuwa ndio yeye ni Tsh iliyokuwa imeshuka kwa 10% dhidi ya dola,basi pale ingepanda kwa 90%.
 
Back
Top Bottom