Haya yalikuwa ni matangazo ya moja kwa moja kutoka Uwanja wa taifa mjini Dar es salaam kupitia redio Tanzania Dar es Salaam,"Mpira unatoka katika lango la timu ya Dar Yanga Afrikans kuelekea katika lango la timu ya Simba "Taifa Kubwa", Golikipa wa Yanga Steven Nemes anaupiga mpira vizuri kabisa hukuuuuu anauchukua Said Mwamba Kizotaa Kizotaa anampasia Method Mogella Mogella pembeni kabisaaaa anampelekeaaa kwakeeee Salum Kabunda Kabundaa Kabunda kwakeee Constatine Kimanda Kimandaaa anapeleka mpira kwa Ken Mkapa Ken Mkapa Mkapa Mkapa anatoa pasi ndeeeefuuuuu kwake Lunyamila Lunyaamiilaaaaaa Lunyamilaaaa chenga ya kwanza chenga ya piliii Lunyamila bado Lunyamilaaaa Lunyamilaaaa hatari katika lango ya timu ya Simba lalalalalalalal gooo lalaa goooo alalalalal Gooooooooooooooooooooooooo!!!
one of the greatest player this country has ever produced. naamini kwa upande wa left wing, hakuna kama lunyamila ktk historia ya tanzania. inasikitisha aliishia hapa hapa na kuishia kupata visenti vya akina gulamali. ndo matatizo ya kuzaliwa at a wrong time au wrong place! wanamsifu Giggs, lakini Giggs kwa Lunyamila wala haoni ndani...
siku hizi ni fundi gereji pale mwembechai BIHONYI AUTO GARAGE kajaa tele anakula spana
Hivi huyu jamaa yuko wapi kwa sasa na anafanya nini?
Alitaga ksbb alipokuwa Form IV alikuwa ameitwa kwenye team ya Taifa ya Tanzania Bara kwenye mashindano fulani ya Challenge,kwahiyo alikuwa anatoka Shy anakuja kupigania Taifa lake wakati wenzake wanaendelea kusoma na kujiandaa na mitihani,na ndo mashindano yale yaliyoibua kipaji chake...unafikiri kwa mazingira ya namna hiyo kwanini asizungushe hata kama angekuwa ndetichia angetaga tu,hata Masuke.....kwanza mimi nachelea kusema Kijana alikuwa bright sana basi tu soka lilimnyima fursa ya kuthibitisha hilo na ndo maana alifaulu Darasa la VII peke yake katika shule aliyokuwa anasoma huko Shinyanga VijijiniAlisoma shy bush kama sikosei.nakumbuka matokeo yake yalipotoka wapenzi wa simba walifurahia sana maana alitaga yai
Mkuu tabia gani hii ya kuniombea mimi nitage? si angefanya kama mwenzake Akilimali kwenye mtihani wa form four mwaka 1999, siku moja kabla ya mtihani alipanga dawati lake safi lakini cha ajabu kesho yake hakuonekana sijui alikuwa amekula dili na headmaster ila baadaye ilibidi arudie form four na akamaliza 2000 matokeo yake siyakumbuki. Halafu jamaa ni jirani yangu huko Mbezi kwa Yusuf.Alitaga ksbb alipokuwa Form IV alikuwa ameitwa kwenye team ya Taifa ya Tanzania Bara kwenye mashindano fulani ya Challenge,kwahiyo alikuwa anatoka Shy anakuja kupigania Taifa lake wakati wenzake wanaendelea kusoma na kujiandaa na mitihani,na ndo mashindano yale yaliyoibua kipaji chake...unafikiri kwa mazingira ya namna hiyo kwanini asizungushe hata kama angekuwa ndetichia angetaga tu,hata Masuke.....kwanza mimi nachelea kusema Kijana alikuwa bright sana basi tu soka lilimnyima fursa ya kuthibitisha hilo na ndo maana alifaulu Darasa la VII peke yake katika shule aliyokuwa anasoma huko Shinyanga Vijijini
Nakumbuka alienda Ujerumani kufanya trials za kujiunga bundesliga huku nyuma bongo kukawa na mechi ya Simba na Yanga pale ccm kirumba. Wanazi wa Yanga wakamtumia ujumbe arudi haraka naye akakubali. Alifika Airport ijumaa na kuunganisha ndege siku hiyo hiyo kwenda Mwanza. Kesho yake Jumamosi alicheza mpira mkubwa mno Simba akafungwa 2-0, goli moja alifunga yeye. Huo ndio ukawa mwisho wa Lunya kucheza ulaya. Huyu jamaa hata Nonda Shaban aliyechezea yanga na UEFA Champions League alikuwa anaomba usiku na mchana acheze kama Lunya. Ila siku hizi yupo Mbezi ya kimara na bado ni mnazi wa Yanga. TheLunyamila alikuwa na kipaji cha aina yake. Jamaa namfagilia. Inasikitisha mno hakupata chance ya kwenda kucheza soka ughaibuni kunakoeleweka sio umangani. Nakumbuka aliwahi kupata chance ya kufanya trials na FC Koln kule Bundesliga sasa sijui ilikuwaje
Tuko Naye huku mbez mwisho darHivi huyu jamaa yuko wapi kwa sasa na anafanya nini?
Umenikumbusha hayo magoli yalifungwa na Bakari Malima (Jembe ulaya) yote kwa kichwaNakumbuka alienda Ujerumani kufanya trials za kujiunga bundesliga huku nyuma bongo kukawa na mechi ya Simba na Yanga pale ccm kirumba. Wanazi wa Yanga wakamtumia ujumbe arudi haraka naye akakubali. Alifika Airport ijumaa na kuunganisha ndege siku hiyo hiyo kwenda Mwanza. Kesho yake Jumamosi alicheza mpira mkubwa mno Simba akafungwa 2-0, goli moja alifunga yeye. Huo ndio ukawa mwisho wa Lunya kucheza ulaya. Huyu jamaa hata Nonda Shaban aliyechezea yanga na UEFA Champions League alikuwa anaomba usiku na mchana acheze kama Lunya. Ila siku hizi yupo Mbezi ya kimara na bado ni mnazi wa Yanga. The
Nilimuona Dodoma uwanja wa Jamhuri mechi na CDA kipindi hicho aisee alifunga goli 1 ambalo alimpiga mlinzi darizi na golikeeper alikuwa katoka kidogo nae akachop ule mpira. Ilikuwa hatari sana.nilimwona lunyamila pale mtwara wakati yanga ikicheza na bandari mtwara alifunga goli ambalo wachezaji wa bandari walishangilia pamoja na mashabiki waliokuja kutoka wilaya zote kuja kumwona LUNYAMILAAAAAA
Anafanya nini kwa sasa?Tuko Naye huku mbez mwisho dar