Ecuador: Mfanyabiashara Daniel Noboa ashinda nafasi ya Urais

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,502
9,282
Daniel Naboa.jpg

Daniel Naboa

Mfanyabiashara huyo wa chama cha mrengo wa kati-kulia, mwenye umri wa miaka 35, atakuwa rais wa kwanza mwenye umri mdogo zaidi Ecuador. Lakini anakabiliwa na changamoto kubwa.

Baada ya asilimia 93 ya kura kuhesabiwa, Noboa alikuwa mbele kwa asilimia 52 huku Gonzalez akiwa wa pili kwa asilimia 48.

Gonzalez amekubali kushindwa na amempongeza Noboa kwa ushindi wake mnamo wakati akipanga kumpigia simu. Amesema hayo alipokuwa akizungumza na wafuasi wake mjini Quito.

Wagombea hao wawili walishiriki kura ya marudio baada ya kuchukua nafasi ya kwanza na pili mbele ya wagombea wengine sita katika duru ya kwanza ya uchaguziwa Agosti 22.

Masuala makuu ambayo yanawapa wapiga kura changamoto nchini humo ni pamoja na uchumi ambao umetatizika tangu kutokea kwa janga la COVID-19, ongezeko la uhalifu ikiwemo mauaji na ghasia za magerezani.

Uchaguzi huo wa Jumapili ulifanyika bila ya matatizo makubwa.

"Leo Equador imeshinda, demokrasia imeshinda,” alisema Diana Atamint ambaye ni rais wa Baraza la Taifa la Uchaguzi nchini humo.

Uchaguzi huo wa mapema uliitishwa baada ya rais kuvunja bunge mwezi Mei.

Uchaguzi wa Equador ulifanyika mapema baada ya Rais Guillermo Lasso kuvunja bunge mnamo mwezi Mei, ili kuepusha kura ya kutokuwa na imani dhidi yake, miaka miwili tu baada ya kuchaguliwa kwake.

Noboa ataongoza kwa muda wa mwaka mmoja na nusu au hadi 2025, kipindi kilichobakia cha muhula ambao wake Lasso

Upigaji kura ni jambo la lazima kwa raia wote wa kati ya umri wa miaka 18 hadi 64. Jumla ya watu milioni 13 nchini humo wanastahiki kupiga kura. Wale ambao hawafuati sheria hiyo hupigwa faini ya takriban dola 45.

Luisa Gonzalez mwenye umri wa miaka 45, wa chama cha mrengo wa kushoto ‘Citizen Revolution' alichaguliwa na Rais Rafael Correa kuwania urais

Wakati wa utawala wa Rais Rafael Correa, Gonzalez alishikilia nyadhifa mbalimbali serikalini, na alikuwa mbunge hadi Mei, 2023.

Mwanzoni mwa kampeni, alisema Correa atakuwa mshauri wake, lakini hivi karibuni amekuwa ajijaribu kujitenga na Correa huku akiwasogelea karibu wafuasi wanaompinga rais huyo wa zamani.

DW
 
Back
Top Bottom