Ebu Soma Maandalizi ya Hii Semina

Ebu Soma Maandalizi ya Hii Semina

Rutunga M

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2009
Posts
1,769
Reaction score
1,393
Jamani nipo kwenye semina moja katika mkoa mmoja tanzania,leo ni siku ya tatu na mwisho wa semina yetu lakini semina yetu ilkuwa hivi.

Jumatatu tulianza semina saa 3:30 badala ya saa 2 asubuhi kwa kutambulishana na ilipofika saa 4 tukaambia ni muda wa chai hadi saa 5 asubuhi.

tuliporudi kutoka chai tukaambiwa tuingie katika vikundi na kupewa masawali mawili kuwa twende kuyajibu tupite lunch kisha turudi saa 9 alsiri kuwasilisha na baada ya kufanya tukalipwa posho hiyo ni DAY ONE

DAY TWO
tukapewa kazi ya kutembelea sehemu fgulani eti ni field hadi jana jioni

DAY THREE
Tumefika leo na kueleza tulichoona kwenye field kisdha tumelipwa posdho zetu na tunambiwa tmemaliza SEMINA

Hivi hii nchi imefikia hapa kweli?

Lakini kwenye Malipo sikuuliza, nimelipwa hata nauli ya ndege, asubuhi ntakuwa airport huyo makwetuuuuu

Tanzania Nchi yenye Neema tele
 
...Heri yako. Angalau umepata kiduchu cha kipande cha Keki yetu ya Taifa!
 
Ningekuwa mimi nisingepokea hiyo posho yao....kama Slaa alivyokataa mishahara ya Wabunge
 
Hiyo semina ilikuwa ni mpango wa watu-kutafuta sehemu ya kutumia per DM,Ukweli ni kwamba hilo linachangia kurudisha maendeleo nyuma.Raslimali hazitumic ipasavyo-Na hiyo ni sehemu ya ufisadi kwani huelimishwi kama ilivyotakiwa.Ina maana hata ukirudi huwezi kueleza umejifunza nini na utaapply vipi ktk maisha ya kila cku au ktk utendaji wako wa kazi.Inackitisha saaana.

Ndiyo maana watu wanend training nyingi saana,lkn utendaji wa kazi sifuri kwani huishia kutembelea vituo vya utalii tu ktk nchi huck,ila ukisoma aim ya semina au training na kile unachokifanya ni opposite.Fine enough tunaridhika kwa kuwa tumepewa hela-ila ilibidi masuala kama haya tuyakemee kabisa ktk jamii.
 
Wewe peke yako umepunguza hela ya kusomesha watoto 40 wa shule ya Msingi. Ina maana kama mlikuwa kumi ina maana mmedhulumu watoto mia nne, halafu tunasema elimu ya bure haiwezekani. Tanzania ni comedy show isiyo na mwisho.

Kuna siku maafisa kutoka mikoa ya Tanzania walikaa whitesands wiki moja full board kujadili jinsi ya kudeal na gharama za matibabu za wastaafu. Nikauliza kwa nini hizo hela mlizotumia msiwagharimie wastaafu wenyewe kwenye matibabu.

Bongo tambarare bwana
 
....wengine walienda Semina Elekezi Ngurdoto na hakuna kilichobadilika.
 
Halafu tunadanganyana eti tutaweza kuindeleza nchi! Toka lini kuna ufalme umesimama katika mihili ya uongo? Labda wa Bulicheka but not in the real world. Nakupongeza mtoa mada kwa kuona jinsi ambavyo tunaendelea kujidanganya wenyewe. Hatuwezi kufika tunakotaka kufika kaika mafikirio yetu bado ni yale yale ya kupata hela za mtelemko na kutojibidiisha kufanya kazi. It hurts us as individuals and as a nation.
 
....wengine walienda Semina Elekezi Ngurdoto na hakuna kilichobadilika.

tena nakumbuka mpaka washiriki wa miss tourism walipelekwa kumsalimia mzee baada ya kuchoka na semina
 
Ilikuwa ni ya kiserikali? Sishangai ndo namna wanavyotutzfuna. Ila kama ni semina ya CEO's mara nyingi inakuwa kama retreat tu.
 
Nashindwa kucheka au kununa
lakini ndo hivyo tena hela imekwenda hairudi.
bado mzee wangu wa EAC mstaafu hajalipwa mafao yake since ilipovunjika
 
waandalizi wa hiyo semina wamechukua how many tymz ya hizo ulizopewa wewe!!!!!??????
 
Bongo yetu ndy ilivyo, watu wanaandaa seminar kwa ajili ya ulaji tu. Aug nilikuwa sehem kwenye seminar ya siku saba (mm si mfanyakazi wa serikali, tulialikwa tu kama wadau) Jumla ya washiriki walikuwa 40 kati ya 50 walioalikwa, kwa ufukunyuku wangu nikadadisi mpaka nikapata bajeti halisi ya seminar hiyo, kam 285,000,000/= mia mbili themanini na tano millioni! Posho walikuwa wanatoa laki2/day, chakula malazi na nauli jumla haizidi 400,000/= kwa siku kwa kila mshiriki! Hesabu za mwisho nazo nilibahatika kuziona-Hakuna pesa iliyobaki, na idadi ya washiriki waliandika 49 (hakuhudhuria mmoja tu!).....wakati kuna waalimu wanalipwa 210,000/=pm!!!
 
Jamani nipo kwenye semina moja katika mkoa mmoja tanzania,leo ni siku ya tatu na mwisho wa semina yetu lakini semina yetu ilkuwa hivi.

Jumatatu tulianza semina saa 3:30 badala ya saa 2 asubuhi kwa kutambulishana na ilipofika saa 4 tukaambia ni muda wa chai hadi saa 5 asubuhi.

tuliporudi kutoka chai tukaambiwa tuingie katika vikundi na kupewa masawali mawili kuwa twende kuyajibu tupite lunch kisha turudi saa 9 alsiri kuwasilisha na baada ya kufanya tukalipwa posho hiyo ni DAY ONE

DAY TWO
tukapewa kazi ya kutembelea sehemu fgulani eti ni field hadi jana jioni

DAY THREE
Tumefika leo na kueleza tulichoona kwenye field kisdha tumelipwa posdho zetu na tunambiwa tmemaliza SEMINA

Hivi hii nchi imefikia hapa kweli?

Lakini kwenye Malipo sikuuliza, nimelipwa hata nauli ya ndege, asubuhi ntakuwa airport huyo makwetuuuuu

Tanzania Nchi yenye Neema tele

.rutunga: hii ni jf,home of great thinkers. Tueleze kinagaubaga:nani/taasisi gani iliandaa hiyo semina,ilifanyika mkoa gani?hotel/ukumbi gani?. Hii itatusaidia wana jamnvi kujadiri kwa upana zaidi.
 
Mlilipwa kiasi gani? Ivi hizi per diem zikifutwa mnaonaje?
 
.rutunga: hii ni jf,home of great thinkers. Tueleze kinagaubaga:nani/taasisi gani iliandaa hiyo semina,ilifanyika mkoa gani?hotel/ukumbi gani?. Hii itatusaidia wana jamnvi kujadiri kwa upana zaidi.

Mh ????
Isije ikawa wewe ndiye ulikuwa muandaaji,kwani kwenye semina kuna mwezeshaji mmoja alikuwa akiguzia JF kuwa inafichua mambo kama ni wewe basi tambua kuwa hatukuridhika na matumizi mabaya ya fedha za umma.

duh!!!!!! balaaaaaa........ tutafika tu slow slow..... as usual. zaidi ya haya yanafanyika tunayoyajua nimachache sana. tena mwenzetu aliyeona mpaka idadi ya watu na malipo ana bahati. huwa wana bana zile karatasi zina chakaa kwa siku mmoja. tena kwingine huwa tuna sainishwa figure kubwa unambiwa hiyo nyingine utanipa tukitoka......... this kantiri bwana!!!!!!1
 
Back
Top Bottom