Ebu pita wewe mama ata baba itakuhusu

Ebu pita wewe mama ata baba itakuhusu

Jurrasic Park

JF-Expert Member
Joined
Sep 13, 2013
Posts
3,833
Reaction score
6,889
Habari wana MMU

Nifuraha yangu nikutane na nyie hapa kushirikiana changamoto za maisha ya kila siku huku duniani.Ni miezi miwili tangu niingie mjini hapa Dar es salaam kwa kazi niliyoomba huku. Maisha yanaenda pamoja na ugumu wa maisha lakini inshalahh nitayaweza.

Siku moja katika pitapita zangu huku mjini nikakutana na mama mmoja aliyekuaga jirani yangu kule kanda ya kaskazini. Story iko hivi huyu mama aliolewa na mwanaume mmoja ambaye alikuwa mpiganaji wa maisha.

Huyu mwanaume alipata kujenga nyumba ya kisasa na club ya kuuza mbege. Katika mihangaiko ya maisha huyu mwanaume alipata ajali akafariki kwa ajali ya gari. Huyu mama baada ya ya taratibu za mazishi kuisha huyu mama alipata mwanaume mwingine.

Huyo mwanaume aliyempata katika kuishi naye akataka kupata mkopo wa hela benki. Benki kwenda kupata mkopo, wakanunua gari ya kutembelea hizi za bei mbaya. Sasa miaka ikasonga wakiwa na huyu mwanaume.

Kuna kipindi nilishuhudia yule mama alitaka kujenga nyumba nyingine wakati nyumba ilipofikia kuwekewa kioo aligoma kumlipa fundi, fundi akatembelea juu ya kioo (mlio jenga mnajua maana yake )Ilipofika muda wa kulipa mkopo huyu Mama akamshirikisha yule mwanaume akafanya namna nyumba aliyoweka rehani na mali zingine benki ikachukua zote.

Mwanaume kuona vile akasepa akamwachia mama ule msala. Mama akabaki na asset moja ya club ya mbege pale kanda ya kaskazini. Sasa mama pale kilabuni alikorofishana na yule muuzaji ambaye mume aliyemwachia sasa muuzaji akasepa kimoja. Kutokana na kauli mbaya za yule mama wanunuzi wakasepa kimoja(wanunuzi wanaweza wasimpende tajiri wakampenda muuzaji) sasa ile asset moja nayo ikafilisika.

Mama wa watu akakimbia kule kaskazini leo nimemkuta huku dar anakaa na mashemeji. Namuonea huruma sana kwa sababu alikuaga tajiri leo ndo ivyo tena. Mwanaume yule aliyekuwa naye sasa aonekani. Siamini kabisaa huyu mama ndo kafika hapa tunagombea daladala hapa mjini kama hatuna akili, leo ndo ivyo tena sijui ata nimsaidieje

Nimeileta hapa jukwaani ili iwe fundisho kwa wadada na wamama walioko huku jamani huwezi pendwa na wanaume wawili

Asante@gobe
 
kumbe tunapendwa mara moja na mmoja tu kwa hiyo akifa basi tena .. nimejifunza jambo hapa
 
kaskazini na mbege

Ni kama msondo na ngurumo
 
Huyo.mwanamke kajitakia....


Yaani unaweka nyumba rehani ili ununue gari??? Akili za wapi hizo...

Halafu utakubalije mali zako ziwekwe rehani kisa mwanaume anataka gari? Mahaba niue gani haya???

Pole yake lakini
 
Huyo.mwanamke kajitakia....


Yaani unaweka nyumba rehani ili ununue gari??? Akili za wapi hizo...

Halafu utakubalije mali zako ziwekwe rehani kisa mwanaume anataka gari? Mahaba niue gani haya???

Pole yake lakini

mahaba nirushe nikatue kwa BADILI TABIA
 
Last edited by a moderator:
ulikuwa mawazoni mwangu
Huyo.mwanamke kajitakia....


Yaani unaweka nyumba rehani ili ununue gari??? Akili za wapi hizo...

Halafu utakubalije mali zako ziwekwe rehani kisa mwanaume anataka gari? Mahaba niue gani haya???

Pole yake lakini
 
Maelezo sijasikia kama alishazaa watoto na marehem,, je alizaa nae?
Kama ndio basi mwanamke ni mpumbav badala ya kuwaza kuilea familia na kwamba ndo umebaki mwenyewe kama mama na ndo kama baba ye anaanza mambo ya ngono lazima maisha yaporomoke kwasababu ameingia kwenye mapenz mapya na ulimbukeni wa aliyempata ambae hawaz kuchakalika kama marehemu,,.

Pili kama hakuzaa nae basi si kosa lake huyo mama, kuna kitu alikuwa anakitafta either watoto sa marehem akafa mapema akajikita kwa mtu ambae ni mzigo yaan wakulelewa tu na hana future za kama marehemu maana dunian tumetofautiana, na mwanaume ni kichwa cha nyumba sa kikiwa kibov na mambo yote mabov,, mwanamke ni wa kuongozwa jaman.
 
Si kila mara mtu huona lijalo mbele hasa pale kitu kiitwacho mapenzi kinapoingia katikati,pole yake.
 
Back
Top Bottom