Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 38,537
- 47,994
Habari za awali za helicopter iliyoanguka ikiwa imembeba Rais wa Iran, Ebrahim Raisi maarafu kama "the butcher of Tehran"/mchinjaji wa Tehran huenda imepokewa kwa furaha kubwa na wahanga waliowahi kuguswa naye katika utumishi na uongozi wake mrefu ndani ya Iran.
Huyu bwana alianza kama mwendesha mashitaka na baadaye naibu mwanasheria mkuu katika wa serikali ya Iran, alikuwa mjumbe pia katika kamati za mauaji. Chini yake katika nafasi hizo mbalimbali akifanya kazi kwa ukaribu na mahakama ilishuhudiwa watu zaidi ya 8,000 wakinyongwa na maelfu wengine wakitupwa jela, kupotea au kupata adhabu za utesaji mkuu uliopitiliza kwa sababu za kisiasa na mambo mengine yanayoitwa ya kimaadili.
Wa-Iran wenye uraia wa nchi mbili hasa za magharibi walikumbana na mkono wake katili haswa, alibuni mpango wa kuwatumia kama chambo katika migogoro ya Iran na magharibi kwa kuwavizia na kuwakamata akiwasingiza uhaini kisha kuwatumia kama karata turufu kwenye majadiliano mbalimbali na West.
Huenda wahanga kutoka familia nyingi kwa maelfu ndani na nje ya Iran zilizoathiriwa naye wanaomba helicopter hiyo isipatikane kabisa na hawawezi kulaumiwa kwa hilo.
Ubinadamu kazi.