Ebony FM mmetukosea JamiiForums

D Metakelfin

JF-Expert Member
Mar 23, 2017
3,383
3,642
Wakuu
Leo redio ebony FM ya mjini iringa Wakati wakitangaza kipindi chao(sikijui jina ila kinahusu habari kinakuwa hewani saa 11 jioni).

Walikua wakitangaza kuhusiana na majibizano yaliyotokea Jana baina ya askari polisi pamoja na waziri wa kilimo mstaafu bwana Malima lakini cha kushangaza wameegamia upande mmoja wa kuWalaumu maaskari kwa kutumia nguvu kwa viongozi wastaafu.

Na kubwa zaidi walitumia hoja zilizopo jamii forum huku mtangazaji akimalizia kwa kusema "alinena mchangiaji wa JamiiForums.

Wakuu kuna mambo nimeona hayapo sawa hapo...

MOSI: Tukio la Malima na Nape ni tofauti kabisa, kumbuka Nape alinyooshewa bastola na tukio la Malima risasi ilipigwa juu huku Malima akitumia kilichokuwa cheo cha uwaziri kuvunja sheria.

PILI: Ebony FM imejaribu kuidanganya jamii kuhusiana na maoni yaliyopo ndani ya hii forum kwa kuangalia upande mmoja kitu ambacho si cha kweli kwani kuna misimamo tofauti kuhusiana na suala hilo

Je, wadau mmelichukuliaje hilo suala?
 
Sasa hicho kilichosemwa ni kutokana na maoni ya mchangiaji wa jamiiforums, je kipo au hakipo? Ebony, jf wametukoseaje yani?
 
Nimeona si vyema wala haki kusema kwa mujibu wa jamii forums ilhali jamii forums ina maoni tofautitofauti lakini wao wameegamia upande mmoja
Kwahiyo wewe ulitaka wasome maoni ya wachangiaji wote?

Kweli wewe ni K.
 
nadhan yalikuwa in maoni ya huyo mtangazaji tu...hakuna haja ya kukishutumu kituo
 
Back
Top Bottom