Ebola yaathiri siku kuu ya Eid

Ebola yaathiri siku kuu ya Eid

MK254

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
33,574
Reaction score
53,613
090921105611_kenya.jpg

Eid adhaaRipoti kutoka Magharibi mwa Afrika zinasema kuwa sherehe za Eid Ul Adhaa zimeathiriwa vibaya na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.
Nchini Guinea maeneo ya uma ambapo watu hukongamana ili kufanya ibada yalikuwa bila watu.
Nchini Sierra Leone Muungano wa baraza la maimamu uliwaonya waislamu kutoamkuana kwa kushikana mikono wala kukumbatiana.
Madaktari nchini Ujerumani wanasema kuwa mwanasayansi aliyeambukizwa ugonjwa wa ebola wakati alipokuwa akilifanyia kazi shirika la afya duniani ameponea.
Vilevile Muunguzi wa Ufaransa aliyeambukizwa ugonjwa huo alipokuwa akijitolea katika shirika la madaktari wasio kuwa na mipaka MSF nchini Liberia pia ameponea.
Takriban watu 3400 wamefariki kutokana na maambukizi ya ugonjwa huo.

Ebola yaathiri siku kuu ya Eid - BBC Swahili

 
Hili gonjwa linatisha sana, Mungu atusaidie usihamie Afrika ya Mashariki. Yule Mliberia mgonjwa wa Ebola kule US (Dallas, Texas) yuko mahututi sijui kama atapona. Sijui kama hata anatibiwa sawa sawa.
 
Back
Top Bottom