Ebola: Damu ya waliopona kutibu ugonjwa

Ebola: Damu ya waliopona kutibu ugonjwa

figganigga

Platinum Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
27,943
Reaction score
63,717
Ebola😀amu ya waliopona kutibu ugonjwa
140905205847_who_ebola_marie_kieny_afp_624x351_afp.jpg

Mkutano wa WHO kuhusu Ebola mjini Geneva

Shirika la afya duniani WHO limesema kuwa damu ya watu ambao wameponea ugonjwa wa Ebola inaweza kutumiwa kuwauguza wagonjwa wengine.

Katika mkutano mjini Geneva, wataalam wa shirika hilo walikubaliana kwamba hii itakuwa njia ya haraka na ilio salama dhidi ya ugonjwa wa Ebola,sababu kuu ikiwa kwamba kinga ya mwili katika damu ya mtu aliyepona inaweza kukabiliana na virusi hivyo.

Wataalam hao pia wanataka matibabu mengine kuharakishwa ikiwemo dawa ya Zmapp pamoja na chanjo zengine mbili.
Idadi ya watu wanaodaiwa kufariki kutokana na ugonjwa wa Ebola imepita elfu mbili.

Zaidi ya watu elfu nne wameambukizwa ugonjwa huo huku tiba yake ikiwa bado haijajulikana.

Chanzo:BBC
 
Back
Top Bottom