Ebola: Annan ayakosoa mataifa ya Magharibi

Ebola: Annan ayakosoa mataifa ya Magharibi

RUCCI

JF-Expert Member
Joined
Oct 6, 2011
Posts
1,702
Reaction score
1,716
120716041609_kofi_annan_512x288_afp.jpg
Annan anasema hajaridhishwa na juhudi za mataifa ya magharibi kupambana na Ebola

Katibu mkuu wa zamani wa Umoja wa Mataifa Kofi Annan amekosoa ambavyo mataifa ya magharibi yameshughulikia janga la Ebola.

Bwana Annan ameambia BBC kwamba hajaridhishwa kamwe na hatua za mataifa ya magharibi kupambana na Ebola.

''Ikiwa janga hilo lingekuwa limeathiri eneo lengine , hatua ambazo zingechukuliwa zingekuwa toifauti sana.''

''Hata ukiangalia ambavyo janga hili limekuwa likienenea , mataifa ya magharibi yalichukua hatua tu wakati ambapo ugonjwa huo ulitambuiliwa katika mataifa yao kama vile Marekani na Ulaya.''

Kwiengineko, katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-Moon amezindua kampeini ya kuchagisha mamilioni ya dola kusaidia kwa vita dhidi ya ugonjwa hatari wa Ebola, baada ya kampeini ya awali ya kuchangisha pesa kukosa kufikia malengo yake.

140728145501_ban_ki-moon_512x288_getty_nocredit.jpg
Ban Ki-Moon anaomba ufadhili zaidi katika vita dhidi ya Ebola
Mkuu huyo wa Umoja wa Mataifa amesema kampeini aliyozindua mwezi Septemba kuchangisha pesa imefanikisha tu mchango wa dola 100,000 kufikia sasa.

Ban Ki Moon ni mmoja wa viongozi wa kimataifa wanaokosoa juhudi za kimataifa za kupambana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola akisema ni hafifu mno.

Ugonjwa huo umewaua zaidi ya watu 4,500 kufikia sasa wengi wakiwa katika mataifa ya Liberia, Guinea na Sierra Leone.

Wadhamini wametoa mchango wa karibu dola milioni 400 kwa mashirika mengine ya Umoja wa Mataifa lakini sio kwa kampeini aliyozindua bwana Ban ambayo inapaswa kuwa kama akiba ya pesa zitakazotumiwa kwa vita dhidi ya Ebola pindi zinapohitajika.

Kuna ahadi ya dola milioni 20 katika mchango zitakazotolewa kwa kampeini hiyo.

Kati ya mataifa ambayo yameahidi kutoa mchango wao kwa Ban Ki Moon ni Colom,bia pkeke ambayo tayari imetoa dola laki moja.

Mjumbe maalum wa Umoja huo kuhusu Ebola, David Nabarro, amesema hazina hiyo itakuwa afueni kwa vita dhidi ya Ebola ambavyo kwa sasa limegeuka na kuwa janga la kimataifa.

Bwana Ban amesema ni wakati kwa dunia nzima kuchukua hatua haya mataifa yenye uwezo mkubwa kutoa msaada wa kifedha na uwezo wa kuwafikia wagonjwa na pia kutoa matibabu.

Wito kama huo umetolewa katika siku za hivi karibuni na Rais wa Marekani Barack Obama , waziri mkuu wa Uingereza David Cameron na Rais wa benki ya dunia Jim Yong Kim.

Source:
BBC

http://www.bbc.co.uk/swahili/habari/2014/10/141017_ebola_annan
 
....China ilikuwa inakaribia kuwekeza karibu mataifa yote ya Africa magharibi,kuharibu shughuli za uwekezaji lazima vyikwazo viwekwe kwenye mataifa haya. china ni rafiki wa karibu wa Urusi...mataifa ya A.magharibi yako karibu na US kijiografia. China na Urusi kwa paoja wana urafiki wa mashaka na US na EU. A. magharibi ni sehemu muhimu kama ikiwa launching pad ya "missiles".
....Ili kupata ela za kugharamia vita ya Syria na ukraine na kukabiliana na vikwazo vya Urusi...US na washirka wake hawakuwa na jinsi kuzilazimishi nchi zilizoathitika kukopa kutoka WB na IMF pesa , mnajua waoratibu mienendo ya vyombo hivi vya fedha.

Nawaza tu....!

Annan...alikuwa kwenye payroll ya watu hawa.

Nawaza tu....!
 
mnalialia hamsaidiwi kwani nyie hamna ubongo na mikono!?. mnapewa misaada mnafanya haki yenu!. watu wenyewe ni kama hayawani mwitu hamuaminiki mnaweza kusaidiwa na baadaye mkawageuka wanaowasaidia kama mlivyowafanyia wamarekani mogadishu. omba usaidiwe sio kulia kwanini hausaidiwi, kwani we mtoto. mxiuuuu.
 
Africa haiombi msaada kutoka America au Europe Ni lazima kupewa kiasi cha Mali inayovunwa Na iliyokwisha vunwa kutoka Africa hili sio ombi kwahiyo hakuna msaada nchi za Africa zinapata kutoka developed countries ila Ni surplus ya Mali ya waafrika iliyochukuliwa Na inayoendelea kuchukuliwa na wazungu for the so called colonialism and neo colonialism.Kama wewe Ni msomi utakuwa umenielewa.
 
Mbona theorization hii inakinzana na uhalisia??!!
Hivi neno "kwa msaada wa watu wa. . . . ." lina maana gani tena??!!
DFP number plate nayo ni kuashiria surplus inayorudishwa??!!

Natamani kuelewa zaidi
 
Sijamsikia kusema sana kuhusu viongozi wa Africa na wanavyoongoza nchi zisizo na mifumo ya afya ya kueleweka.
 
Mbona theorization hii inakinzana na uhalisia??!!
Hivi neno "kwa msaada wa watu wa. . . . ." lina maana gani tena??!!
DFP number plate nayo ni kuashiria surplus inayorudishwa??!!

Natamani kuelewa zaidi
uhalizi

Uhalisia upi bro Africa imeendelea kuwa masikini kwa miaka mingapi sasa? Unakumbuka structural adjustment programs ambao wali introduce the western? Globalization it's like we are kept in the ring the heavy weight and feather weight unategemea nini Apo?
 
Sijamsikia kusema sana kuhusu viongozi wa Africa na wanavyoongoza nchi zisizo na mifumo ya afya ya kueleweka.

Viongozi WA Africa wataongea nini mbele ya Barack Obama? Juzi hapa si waliitwa kama wanafunzi wote waliitwa Na kuelekezwa mambo ya kutekeleza. Everything relies on power brother
 
Viongozi WA Africa wataongea nini mbele ya Barack Obama? Juzi hapa si waliitwa kama wanafunzi wote waliitwa Na kuelekezwa mambo ya kutekeleza. Everything relies on power brother

Totally beside the question.

Nimeuliza kwa nini Annan hawasemi viongozi wa Afrika kuboronga?

Wewe unaniambia viongozi wa Afrika hawawezi kusema mbele ya Obama.

Habari niliyouliza ni tofauti na uliyojibu.
 
Nimekujibu ila umeshindwa kuelewa nikwamba viongozi Si Kama wanaboronga Kama ulivyosema lakini mfumo uliopo wa uendeshaji wa masuala ya kisiasa Na kiuchumi duniani upo centralized Na great powers so Ni vigumu Sana kujifanya kichwa ngumu labda uwe Kama Mugabe.sijui Kama umenielewa Apo bro
 
You are an apologist of mediocrity. Viongozi wa Africa wanaboronga criminally. Gaddafi mtu aliyekuwa anapata two billion USD every week from oil kaishia kujidunga cocaine, kuwa pedophile, kubaka wake za majenerali wake na mawaziri wake na watoto mpaka wananchi wake wamemuua.

Utasema hajaboronga huyu?

Huyo ndo wamemtawadha "King of Kings of Africa".

Of course superpowers watataka ku centralize power.

Viongozi wa Africa kushindwa kuvunja hiyo habari ya superpowers kama unavyoisema ndio kuboronga kwenyewe.

Kwa nini Annan asiwaseme viongozi maboya?

Where is Africa's CDC?

Why shouldn't Africa develop it's own cures and vaccines?
 
Whete is Africa's CDC?

Why shouldn't Africa develop it's own cures and vaccines?

Ha ha ha ha feather weight in the same ring with the heavy weight that's too difficult brother.
 
Africa haiombi msaada kutoka America au Europe Ni lazima kupewa kiasi cha Mali inayovunwa Na iliyokwisha vunwa kutoka Africa hili sio ombi kwahiyo hakuna msaada nchi za Africa zinapata kutoka developed countries ila Ni surplus ya Mali ya waafrika iliyochukuliwa Na inayoendelea kuchukuliwa na wazungu for the so called colonialism and neo colonialism.Kama wewe Ni msomi utakuwa umenielewa.
ukisema tuanze kulipana dunia haitatosha . wajapan wawalipe wakorea na wachina, wafaransa wawalipe ulaya kwa matendo ya napoleon, wajerumani walipe kwa matendo ya hitler, waturuki nao walipe, waroma nao walipe.......... mali ya wazungu ni product ya ubongo na mikono yao (hata kama ilikuwa ni kupora waafrika). waafrika tunalalama utafikiri sisi ndiyo watu wa kwanza kutawaliwa toka dunia ianze.
 
Libya is the very best country to leave in ghadafi's era more than ever.
 
ukisema tuanze kulipana dunia haitatosha . wajapan wawalipe wakorea na wachina, wafaransa wawalipe ulaya kwa matendo ya napoleon, wajerumani walipe kwa matendo ya hitler, waturuki nao walipe, waroma nao walipe.......... mali ya wazungu ni product ya ubongo na mikono yao (hata kama ilikuwa ni kupora waafrika). waafrika tunalalama utafikiri sisi ndiyo watu wa kwanza kutawaliwa toka dunia ianze.

You look for sympathy brother the world knows how Europe underdevelop Africa Na mpaka sasa hao wote uliowataja some of them continue to benefit from our resources.Wao wanaendelea kutawaliwa na nani?
 
....
Utasema hajaboronga huyu?

Huyo ndo wamemtawadha "King of Kings of Africa".

Of course superpowers watataka ku centralize power.
.....
We know all of your tricks now and ill motive towards Africans......!!!

globalresearch.ca said:
Dr. Cyril Broderick, A Liberian scientist and a former professor of Plant Pathology at the University of Liberia's College of Agriculture and Forestry says the West, particularly the U.S. is responsible for the Ebola outbreak in West Africa. Dr. Broderick claims the following in an exclusive article published in the Daily Observer based in Monrovia, Liberia. He wrote the following:
The US Department of Defense (DoD) is funding Ebola trials on humans, trials which started just weeks before the Ebola outbreak in Guinea and Sierra Leone. The reports continue and state that the DoD gave a contract worth $140 million dollars to Tekmira, a Canadian pharmaceutical company, to conduct Ebola research. This research work involved injecting and infusing healthy humans with the deadly Ebola virus. Hence, the DoD is listed as a collaborator in a "First in Human" Ebola clinical trial (NCT02041715, which started in January 2014 shortly before an Ebola epidemic was declared in West Africa in March.​
 
Back
Top Bottom