ebay inagoma kufanya manunuzi, tatizo nini?

poposindege

JF-Expert Member
Nov 22, 2010
453
175
Habari wadau!
Naomba msaada kwa ambao washawahi kufanya manunuzi kwenye mtandao wa ebay.com
Kwani nimefanya manunuzi kwa mara kadhaa lakini napata majibu ambayo siyaelewi na ninachokusudia kununua nakikosa.

Nimekuwa nikinunua vitu kupitia mtandao wa aliexpress.com mara nyingi na nafanikiwa.
Nina akaunti ya paypal na kadi yangu ya benki inaruhusu kununua bidhaa online.

Na salio lililokuwepo kwenye akaunti yangu ni kubwa na la kutosha kufanya manunuzi ya bidhaa ninayokikusudia. Naomba msaada kwa wenye ujuzi zaidi kuhusu kufanya manunuzi ebay.

ebay.JPG
 
Chagua hapo unataka kulipia hiyo bidhaa kwa njia ipi kama ni paypal au credit card maana naona ndio tatizo lililopo hapo kwenye hiyo screenshot mpaka kushindwa kulipa.
 
Kuna tatizo kwenye kadi yangu ya benki.
Kuna salio kubwa ambalo lipo lakini halifanyi kazi.
Nimeshawasiliana na Benki husika wanalifanyia kazi.
Ahsante kwa wote mliojaribu kunisaidia.
 
Back
Top Bottom