East Coast Team

East Coast Team

Leo nilikuwa nasikiliza ngoma za early 2000's
Hawa eastcoast team walikuwa wanajua ngoma zao zina hisia flani ambayo naimiss kwenye ngoma za siku hizi mfano
1. Hii leo- Gk ft F.a na AY
2. Kosa langu - Gk ft Pauline Zongo
3. Nitakufaje - GK ft Pauline Zongo
4. Tutakukumbuka - Gk ft TID ( hii ngoma kali kuanzia beat verse mpaka chorus)
5. Mchanga wa macho - AY ft Gk na Complex (RIP)
6. Mabinti damu damu - F.a
7. Tuliza boli - F.a
8. Dirisha la misuko suko - F.a
9. Machoni kama watu - AY ft Lady jaydee
10. Alikufa kwa ngoma - F.a ft Lady jaydee

Mziki wa zaman mtamu sana sio kama wa siku hizi wa shikorobo
Haimaanishi ni mziki Bora kuliko wa Sasa,mziki wazamani unahisia kwasababu tu unakukumbusha mbali.
 
HII LEO LYRICS

Kiitikio:
------------
Hii leo
Crazy GK Mwanafalsafa AY
Weka manyanga chini
Hivi sasa tupo hewani
Twakupa maneno matamu
Na yenye thamani
🎼🎶🎶🎶🎶

Verse 1: AY
-----------
Oya.! Navaa buti
Na full CBM
Nazama street
Ntapiga dili zaidi ya 12
Muda mfupi
I got a Masterplan
Bright town boomerang
AY usijishike sasa nipo hewani

Natoa bunduki
Gharama lukuki kama nyuki
Namwaga miba
Kwa wa fitina wanaozuga
AY sumu kwangu mimi ni ulaghai
Natenda mambo mema
Watu wema wafurahi

Akili ichemke
Tuliza boli mbele tupete
Nikizinyaka ndipo ujivute
Mbele ya GK
Kama domo zege usisogee
Kwangu mi
Kama unavyochonga upotee

Usiridhike
Ndani ya life mshikemshike
Ububujike
Utakachokiona usishtuke
Kwa stahili hii mpaka hawa hii
Nipate kitita siwasubiri
Spidi mshale usinivute

Mambo mazuri tulivu
Hayahitaji kukurupuka
Uvumilivu wahitajika
Wenye mrengo uliyoinuka
Mapande yanapotoka
Napo wanga watakereka
Hadi wazushi watetemeka
Vibarazani kwenye mkeka

🎼🎶🎶🎶🎶

Verse 2: Mwana FA
-------------
Mwana f.a.l.s.a.f.a.
Ukipenda anasa za show-time
Niite Sensei
Watu wanakuja na wanakwenda
Watu wananukia Uturi
Na bado watu wamevunda

Dhamira ikipanda
Hata msuli utafungwa mkanda
Alihitaji mjadala
Aliyedanda treni kwa mbele
Ndiyo anajua mjini shule

Siyo kwamba mimi sipendi
Harufu ya kuku wa Kienyeji
Hapana kwangu nyingi
Naona umuhimu wa kuhoji

Toka mitaa ya Upanga
Iwe Nyong'olo, Ali Khani,
Kilombero au Kalenga
Watu wana-shine
watu watazama
Inakuwa vipi mnapagawa

Ni sawa kwa game
na kwangu game
Haliwepo sawa
Utapofika Usipofika
Bado asubuhi itafika

Ajabu ya walimwengu
Vichwa ngumu ubongo mchungu
Mchana wakiomba Mungu
Usiku ni wanga sugu
Ya walimwengu kwa walimwengu

Sasa wanauliza Steve B
Eti ni DJ au MC
Mi sijiviki Uwakili
Na nakaa MJ
Natega Scratch za Bonny
Zikijazwa mi ni mzigoni
Utajuta kuwa vitani
Au utakoma kuwa mshindani
Clap..Clap.!

🎼🎶🎶🎶🎶

Verse 3: Crazy GK
-------------
Hey yo Nikisema 'One'
Enyi machizi semeni 'Two'
Nikisema 'Three'
Enyi machizi semeni 'O'

Ni King Crazy GK
Nasema wao kwao kivyao
Na sisi kwetu kivyetu
Hiyo ndiyo sheria zetu
Sisi na Upanga yetu

Kwani mpira akili kichwani
Tunatuliza mabutu mabutu
Weka chini toa pasi
Tunacheza tunacheza
Ng'adu kwa ng'adu
MC kwa MC
Prodyuza kwa Prodyuza

Haya sasa sema nao
AY simama na wako
Dunga simama na wako
Nsanga simama na wako
Wapi John Mahundi
Ludigo ni ngoma nzito

Kwani vita kuu ya tatu ya dunia
Imetangazwa na Amiri jeshi mkuu
Crazy GK nipo ndani ya kikosi
Alafu nina Mikosi na nina gozigozi
Kwani dozi zetu ni nzito kama jabali
Kwenye mzani hupimi

Niggas is got back
Kwani MC ntakutia mashakani
Hauwezi kaa pembeni au ingia vitani
Kwani hii fani haitaki utani
Niggas get off the money
And find the honey
We have find the money
Get the money
Spend the money

Na sasa tushika machine gun
Alafu naingia vitani
Hatutaki kuwa na amani
Nakuvalia miwani ya bati
Nakumwaga mavi
Bila kujali wewe ni nani
Kwani wote wanga

Kwa sababu mnanipiga mapanga
Nikiwepo mnajifanya mnanipenda
Nikiwapeni mgongo mnaniponda
Mnaniita bitozi
Kwa sababu navaa ma FUBU
Alafu na drive Bima (BMW)
Lakini ni mipango ya mwenyezi Mungu jama
Any nobody's can refused

Nasasa nakata fuse
Maana machizi wote wamesizi
Na kigugumizi kaka
Ukileta pumba ndo umekwisha
Temeke Rap sasa ndiyo mwisho Kuwakilisha.
Ni wakati wetu
Machizi wa Upanga East tunatisha

Majibaba.
Yenye uwezo
Kwenye Rap na hata kifedha
Hukipendi kama imezidi jinyonge
Chukua kamba ujinyonge
Crazy GK mi sijali
Kwani kwetu vyote ni shega tu.

#Balozi.......✍️
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom