EAC Crisis: Who’s the catalyst?...Pres. Kagame or Kenyatta?

EAC Crisis: Who’s the catalyst?...Pres. Kagame or Kenyatta?

Mkuu naomba Usibishane na huyu,hawa ndio wabongo halisia,waliojaa madarakani ambao hawana mipango mirefu ya kiuchumi na Nchi Yao,hasa linapokuja suala la mahusiano ya kimataifa,wamekalia kutafuta sifa kwa kuingilia vitu visivyo na manufaa kwa taifa ili jamii ya kimataifa iwasifie,lakini badala ya kisifiwa wanachekwa na kung'ong'wa na wenzao wanappwageuzia migongo,hii uliyotoa ni analysis nzuri sana na ingeweza kusaidia wale wa Foreign affairs kubadilisha Foreign Policies zao,Leo kukiwa na ugomvi Kenya tutakuwa wa kwanza kurukia huo ugomvi ili tuusuruhishe,ila Kama kuna opportunity ya kufanya biashara na Rwanda na Nchi nyingine hakuna atakayefatilia jinsi ya kuwavutia wanyarwanda kufanya biashara na sisi,ni muda sasa umefika wa hizi bongo zetu zilizolala kuamka na kufanya vitu in our NATIONAL'S BEST INTEREST!
Wewe na wezako mnaofikiri hizo joint projects ni kwa ajiri ya kuikomoa TZ au uadui ndio ndio mawazo mafupi na inaonyesha mlivyo watupu huko vichwani mwenu.
 
kitendawili: baba yake alikuwa Rais EAC ya kwanza ilipovunjika, leo yeye ni Rais EAC ya pili inakaribia kuvunjika, ni nani huyo?
 
[TABLE="align: center"]
[TR]
[TH="align: left"]WHERE IS KIKWETE?? Katengwa au hajakaribishwa au kakataa mwaliko au kaona hii sio muhimu?

Eight heads of state for crucial Africa ICT meet
[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD]
1382914105n2.jpg

Nsengimana (C) chats with youths at an ICT hub in Kigali. The New Times/ File.
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Eight African presidents are expected to take part in the Transform Africa Summit, a four-day conference in Kigali that seeks to spearhead broadband connectivity in the continent.

The meeting, taking place six years after Kigali hosted the Connect Africa Summit, will be co-hosted by President Paul Kagame and Dr Hamadoun I. Toure, the secretary-general of the International Telecommunication Union (ITU).

The presidents expected to attend the high-level conference include Yoweri Museveni of Uganda, Uhuru Kenyatta of Kenya, Salva Kiir of South Sudan, Gabon's Ali Bongo Ondimba, Thomas Boni Yayi of Benin and Burkina Faso's Blaise Compaore.

The Summit opens today but the Heads of State and Government session is scheduled for tomorrow.

The broadband factor

More than 15 other African countries will also be taking part in the Summit at Kigali Serena Hotel that organisers said has attracted more than 1,500 delegates.

The Summit, under the theme, "The Future Delivered Today," will devise ways on how Africa can leverage broadband to transform communities, governments and the private sector.

"This conference will partly discuss all possible ways of fast tracking economic development on the African continent through the use of ICTs," the Minister of Youth and ICT, Jean Philbert Nsengiyumva, told The New Times yesterday.

Nsengimana said high-profile and globally-recognised technological corporations are also well represented in the Summit.

The Summit will as well assess the resolutions drawn during the 2007 Connect Africa Summit and offer a platform for dialogue between governments and the private sector on technologies for socio-economic transformation opportunities for Africa.

The conference is also expected to award exemplary individuals and companies that are excelling in using technology to drive socio-economic transformation.

The Summit is expected to feature five key interactive sessions that include leaders' forum, youth innovation extravaganza, exhibition, Smart Africa conference and the awarding ceremony.

The IT stakes

Last year, the United Nations-backed ITU's report ranked Rwanda among top 10 countries in the continent with active mobile-broadband subscriptions per 100 inhabitants.

ITU estimates that 95 per cent broadband penetration will translate into a 10 to 13 per cent boost in Growth Domestic Product growth for Rwanda.

Earlier this year, the 2013 Networked Readiness Index by World Economic Forum (Wef) and European Institute of Business Administration (INSEAD) ranked Rwanda among the top 10 countries in Africa that are in good position to benefit from new ICTs.

Rwanda is set to roll out a high-speed 4G broadband network that delivers download speed of up to 100 Megabytes per second.

The 4G LTE broadband is expected to be launched at this summit.
[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
 
Koba mi nakufahamu wewe unavyomtetea Kagame, sikulaumu coz' it's none of my business lakini katika mada hii hakuna popote Kagame aliposemwa! Hebu msome vizuri Van persie, namnukuu "Nimekusoma na kukuelewa vyema mkuu,adui wa Tanzania katika shirikisho hili si Kagame kama wengi tunavyodhani bali ni Kenyatta.Nakuunga mkono mbandika mada hii,kwamba kenyatta ni kiongozi" BInafsi, wala sifichi na isitoshe nimeshasema kabla kwamba I've problem with Kagame lakini katika hili wala sina tatizo na Kagame zaidi ya kumuunga mkono; kwamba he's right kwani akiwa kama Rais wa Rwanda hana budi kuangalia maslahi ya Rwanda!

Hata hivyo, kuna jambo lingine la msingi ambalo kwa member mkongwe kama wewe ulitakiwa kulifahamu! Kwamba, usipo-quote post yoyote, by default utakuwa unaizungumzia the main post/thread ikiwa uta-comment anything! Tuachane na hayo, tuendelee!

anakupotezea muda mtu mwenyewe anaganga njaa kwa ajira za ajabu huko USA anafikiri tunajadili watu hapa!
 
Wewe na wezako mnaofikiri hizo joint projects ni kwa ajiri ya kuikomoa TZ au uadui ndio ndio mawazo mafupi na inaonyesha mlivyo watupu huko vichwani mwenu.

50% ya wanyarwada wamesoma Tanzania na wamefundishwa na sisi, ukiwemo wewe mwenyewe! Bado miaka 50 ndio mtakapofikia kiwango cha kujilinganisha na Tanzania (Kama tukisimama). Nyie ni watoto wetu kwa lugha nyepesi
 
Unless kama uliwataka hao TZ-CCM wa-participate kwenye movement inayoendelea....kwamba nao wawe ni part and parcel ya harakati ambazo Uganda, Kenya na Rwanda wanafanya! Kwa mtazamo wangu, hadi sasa Tanzania wapo sahihi! Huwezi kushiriki mchakato ambao utatuua wenyewe! Hapa nawaunga mkono kwa 100% isipokuwa wanatakiwa kujipanga ili kukabiliana na threat hiyo na sio kumlaumu Kenyatta wala Kagame. Kagame nae ni lazima aangalie maslahi ya Rwanda yake kabla ya EAC; so kama anaona ni much better kwao kuungana na Kenya na Uganda basi yupo sahihi! Sisi tunatakiwa kufanya vitendo vitakavyo-prove otherwise. Hata kama Kagame atakuwa na chuki zake binafsi kuhusu TZ; tukijizatiti chuki zake atabaki nazo mwenyewe na roho yake!! Hatuna shida na mizigo ya serikali ya Rwanda tuna shida na mizigo ya Rwanda! Akisusa kupitisha mizigo ya serikali, wafanyabiashara wa huko watapitisha tu ikiwa huku kutakuwa mazingira mazingira nafuu kwao kibiashara! Anaweza ku-impose tax ku-discourage lakini Kagame au Museveni hawatakuwa madarakani milele; obvious watakuja viongozi ambao ni rational decision makers.
Mkuu tatizo kuna watu wanapenda kubebwa bebwa bila kufikiria namna ya kujitegemea wenyewe ki-inchi.
Muungano mmoja tu na Zanzibar ni matatizo lukuki, sembuse miungano ambayo haina tija na wa Nyarwanda , Wakenya wanaotaka ardhi, na wengine.
Hili la EA lazima liwe kichocheo kwa waTanzania kujitazama upya kwa nia ya kujitegemea kwa kila hali.
 
Wee ----- usiharibu hii topic ingawaje umeileta mwenyewe na kila mtu anaweza kuandika upuuzi ujue so don't be a smartazz,msome van Persie anaongelea uadui ambao naona ndio longolongo tuu...anyway move on!!!

najengaga taswira ya kichaa nikisoma post zako...
 
Tanzania imejiloga yenyewe. Hivi kwa uvivu na uzembe huu tulionao wao Kenya, Uganda na Rwanda wakae watusubiri. Kweli? Saa haimngoji mzembe. Sikiliza hii. Diplomasia hujengwa na kubomolewa na ulimi na kalamu. Watu wetu wanapayuka badala ya hoja kupata ukweli juu ya hali hii. Hata mlalamike vipi, mbunge mzima huwezi kuwaita viongozi wa nchi jirani ati "wa ovyo ovyo". Hivi spika hana mwongozo iwapo mbunge ataropoka juu ya masuala yahusuyo nchi nyingine, mwongozo upo kwa wabunge wa upinzani tu? Rais wa nchi jirani, ambaye mnaunda umoja naye, umwite wa ovyo ovyo tena bungeni? Ni kutojua hata abc ya diplomasia!
 
Mzee hapo umenena!Dah kwakweli ww ni mchumi.Badala ya kujiondoa ni kutengeneza coridor ya pili na kweli jamaa lazima watatupigia magoti.(hao wanaotutenga)
 
Unless kama uliwataka hao TZ-CCM wa-participate kwenye movement inayoendelea....kwamba nao wawe ni part and parcel ya harakati ambazo Uganda, Kenya na Rwanda wanafanya! Kwa mtazamo wangu, hadi sasa Tanzania wapo sahihi! Huwezi kushiriki mchakato ambao utatuua wenyewe! Hapa nawaunga mkono kwa 100% isipokuwa wanatakiwa kujipanga ili kukabiliana na threat hiyo na sio kumlaumu Kenyatta wala Kagame. Kagame nae ni lazima aangalie maslahi ya Rwanda yake kabla ya EAC; so kama anaona ni much better kwao kuungana na Kenya na Uganda basi yupo sahihi! Sisi tunatakiwa kufanya vitendo vitakavyo-prove otherwise. Hata kama Kagame atakuwa na chuki zake binafsi kuhusu TZ; tukijizatiti chuki zake atabaki nazo mwenyewe na roho yake!! Hatuna shida na mizigo ya serikali ya Rwanda tuna shida na mizigo ya Rwanda! Akisusa kupitisha mizigo ya serikali, wafanyabiashara wa huko watapitisha tu ikiwa huku kutakuwa mazingira mazingira nafuu kwao kibiashara! Anaweza ku-impose tax ku-discourage lakini Kagame au Museveni hawatakuwa madarakani milele; obvious watakuja viongozi ambao ni rational decision makers.
Ni tatizo kuweka emotions kwenye maamuzi yanayohusu nchi, labda wakija viongozi wengine wanaweza ona tofauti na hawa waliopo, but as far as it is bado tupo sahihi kabisa
 
Tanzania imejiloga yenyewe. Hivi kwa uvivu na uzembe huu tulionao wao Kenya, Uganda na Rwanda wakae watusubiri. Kweli? Saa haimngoji mzembe. Sikiliza hii. Diplomasia hujengwa na kubomolewa na ulimi na kalamu. Watu wetu wanapayuka badala ya hoja kupata ukweli juu ya hali hii. Hata mlalamike vipi, mbunge mzima huwezi kuwaita viongozi wa nchi jirani ati "wa ovyo ovyo". Hivi spika hana mwongozo iwapo mbunge ataropoka juu ya masuala yahusuyo nchi nyingine, mwongozo upo kwa wabunge wa upinzani tu? Rais wa nchi jirani, ambaye mnaunda umoja naye, umwite wa ovyo ovyo tena bungeni? Ni kutojua hata abc ya diplomasia!
Hivi haya mawazo kwamba Watanzania ni watu goi goi na wa hovyo kabisa mnayatoa wapi? Hivi mnapata wapi uthubutu wa kuwa-label Watanzania kwamba ni watu wazembe, wavivu na goi goi wakati shughuli nyingi za kila siku hapa tunazifanya sisi wenyewe? Yale mashamba ya mahindi kule Rukwa, Ruvuma, Mbeya, Iringa and the like yanlimwa na Wakenya? Yanalimwa na Wanyarwanda? Yanalimwa na Waganda? Zile korosho kule kusini zinalimwa na Wakenya? Zinalimwa na Wanyarwanda? Je, na mazao mengine kama hayo yanalimwa na wageni kule vijijini? Tatizo lenu watu kama nyinyi mnakariri, au labda mnapoona familia zenu ni wavivu basi ndo mnadhani kila mmoja ni mvivu! Maelezo yenu hayana tafakuri za kiuchumi na ndio maana mnaishia kuropoka kwamba Watanzania ni wavivu!! Kusini kwa mfano, walikuwa wakulima wazuri wa korosho lakini uzalishaji ukashuka vibaya mno! Watu kama nyinyi ndo mnaishia kukurupuka kwamba imetokana na uvivu kumbe mkulima hawezi kufanya shughuli ambayo haina tija kwake....kama mwaka uliopita alizalisha mazao lakini akashindwa kuyauza usimtarajie kwamba atalima tena kwa spirit ile ile; huo si uvivu!!! Kwa mfano unakuta watu wengine wanaweza kuwaona watu wanaoishi kando kando ya bahari/pwani kwamba ni wavivu kwavile tu hawalimi lakini wanasahau kwamba jamii ndivyo ilivyo!! Jamii nyingi zinafanya shughuli zake kulingana na mazingira yake! Huwezi kumuita Mmasai au Mmang'ati kwamba mvivu kwavile tu hana shamba la mahindi; huyu kwa asili ni mfugaji!! Ikiwa Mmasai anaweza kuitwa mvivu kwavile hana shamba basi hata Mhaya mwenye ekari kadhaa za kahawa nae ni mvivu ikiwa hana mifugo!! Hivi hao Wakenya ambao mnawaona majembe wana tofauti gani na Tanzania? Mara ngapi Kenya inaingia Tanzania kununua mahindi? Mara ngapi mahindi ya Tanzania yanaenda kuuzwa Kenya? Sasa tangu lini mvivu akalima kiasi cha kuwa na akiba ya kuuza na yule asiye mvivu akakosa akiba ya chakula?

Kisha unadai kwamba diplomasia inajengwa na kalamu na kwamba Watanzania wanapayuka hovyo hovyo kwa kigezo cha Komba kuwaita "marais wa hovyo hovyo!" Ikiwa unaona ni bonge la unjifu wa diplomasi kwa mbunge kuwaita marais wa nchi jirani kwamba marais wa hovyo hovyo what about Rais wa nchi moja (kagame) na foreign minister wake kumuita Rais wa nchi nyingine jirani (JK) kwamba ni mjinga asiye na ufahamu wowote kuhusu Rwanda? Ni diplomasia ya wapi hiyo? Sasa ikiwa marais wa nchi wanafanya mambo kinyume na makubaliano ni jina gani hasa linawastshili kama si watu wa hovyo hovyo?
 
50% ya wanyarwada wamesoma Tanzania
!
!
kwa hiyo 50% ya population yao wamesomea tanzania,tujumlishe na 30% kwa kuashume wamesomea kwao huko huko,hii itamaanisha kwamba 80% ya wanyarwanda wamesoma.
vipi tanzania hali ikoje na division five zetu
 
Si ajabu wengi wetu hatufahamu yale ambayo yalisababisha kuvunjika kwa EAC ya awali; sana sana tunafahamu hayo kupitia maandiko tu. Pamoja na hayo, wengi wetu hapa tunafahamu juu ya kufufuliwa upya kwa jumuiya hiyo. Kwa kurejea tu ni kwamba, EAC ilianza kufufuliwa kipindi ambacho Rais Daniel Arap Moi alishakuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Hali kadhalika, hata Rais Museveni nae alishakuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi vile vile. Kwa upande mwingine, Rais wa Tanzania enzi hizo, Mheshimiwa Benjamini Mkapa alikuwa hajatimiza hata miaka mitano madarakani! Na kama kumbukumbu zangu zipo sawa, ni kwamba harakati za kufufuliwa EAC zilianza ama zilipamba moto miaka michache tu tangu Mkapa aingie madarakani. Hii maana yake ni nini? Akili ya kawaida katika hili inashawishi kwamba, kuna kila dalili kwamba Benjamin Mkapa alikuwa ndie CATALYST ya ufufuliwaji upya wa EAC. Wana Habari na wale watu wa serikalini tangu zamani labda wanaweza kulieleza vizuri jambo hili vinginevyo niatendelea kushawishika kwamba Mkapa ndie ali-push kufufuliwa EAC coz’ Museveni na Moi walishakuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi lakini hapakutokea kitu kama hicho!

Hayo yote kwa sasa ni historia lakini ni muhimu katika kutafuta marejeo. Historia ni mwalimu mzuri. TUENDELEE.
Hivi sasa mtu hahitaji kuwa na shahada ya uhusiano wa kimataifa kufahamu kwamba jumuiya ya Afrika Mashariki ipo mashakani! Wengi wa Watanzania, hususani wana Jamii Forums tumekuwa tukimshutumu sana Kagame kwamba ndie chanzo cha yote haya! Humu jukwaani tumemshambulia sana Kagame kwa lugha mbalimbali; za kiungwana na hata zile za kinyume chake! Niseme wazi, mimi ni miongoni mwa wale ambao nimetupa makombora mazito mazito kwa Kagame! Nimepata kumuita Kagame kwa majina mbalimbali kama vile muuaji na mpenda vita! Nitamke tu kwamba, kwa kawaida akili yangu huwa inakwenda likizo ninapoona kiumbe chochote kinaingilia maslahi ya nchi hii!
Hata hivyo, hatimae akili ikarudi kutoka vacation! Hapo tena nikajiuliza; hivi CATALYST ni KAGAME kweli? Mbona ni kama akili iliyorejea kutoka vacation inanishawishi kwamba CATALYST sio Kagame bali ni KENYATTA?

Kwanza tuwekane sawa, hususani kwa wale ambao walikuwa wanalikimbia somo la Chemistry. WHAT’S A CATALYST?
Kwa kifupi ni kwamba, A Catalyst is a substance which ALTERS the rate of chemical reaction! Ikiwa kumbukumbu zangu zipo sawa, nadhani tafsiri yake inamalizia kwa kusema “but remains unchanged at the end of reaction.”
Ku-alter manake ni kwamba ama ita-speed up the rate of chemical reaction au ita-slow down. Kwa kiswahili chepesi, A Catalyst is like KICHOCHEO! Sasa ni nani basi kati ya Kagame na Kenyatta tunaeweza kumuita a CATALYST/KICHOCHEO? Kama ni Kagame, mbona haya hayakutokea zamani wakati Kagame alishakuwa madarakani tangu enzi hizo? Ni kwanini haya yametokea miezi michache tu tangu Kenyatta aingie madarakani? Is it Kagame or Kenyatta?

Kama mtu atanitaka niwaelezee kwa sentensi fupi sana watu hawa ni kwamba Kagame ni one of the most ambitious leader ever happened in EA history! He’s also The War Monger, hili halina mjadala! Huyo ni Kagame! Lakini kwa upande mwingine, Kenyatta ni one of the Capitalist Leader ever happened in EA history! While Kagame is so ambitious politically and political power, Kenyatta is so ambitious economically and economical power! Kenyatta ni bebari kwa tafsiri zozote zile! Kwa hulka zao, watu wa aina hii wana expansionism motives; however, economical expansionism.
Turudi kwa EAC crisis. Hivi ni nini hasa kinachotafutwa pale kwa hivi sasa? Is it political/power or economical motive? Watu wanazungumzia kuziunganisha nchi zao kwa reli, barabara, bandari and so on! Wanazungumzia ku-speed up suala la kuwa na single currency! Are all those political or economical motives? Sidhani kama panahitajika shahada kufahamu kwamba kinachopiganiwa sana hapo ni maslahi ya kiuchumi; at least kwa sasa! Kama ndivyo, sasa ni nani basi anaweza kuwa the catalyst kati ya Kagame who’s so ambitious for political power au Kenyatta ambae ni so ambitious economically? Huku tukijiuliza hayo, bado tunatakiwa kutojisahaulisha kwamba “mbona haya hayakuwapo huko nyuma?”

WHERE DO I STAND?

I HATE ANY LEADER WHO’S SO AMBITIOUS FOR POWER! Hata hivyo, I’ll always ADORE ANY LEADER WHO’S SO AMBITIOUS FOR ECONOMICAL POWER provided he’s doing so at a national level, meaning kwa ajili ya taifa lake! Kenyatta is one of the Richest Leader in Africa! So, nashawishika kuamini kwamba ambition hii aliyonayo Kenyatta kwa sasa ni kutafuta maslahi makubwa ya kiuchumi kwa nchi yake! BTW, hata harakati zenyewe hazionekani kama ni za personal interest zaidi ya kuonekana kama ni for the national interest. Hata kama roho inanikereketa na kunichonyota lakini lazima niseme wazi kwamba BRAVO KENYATTA! Hao ndio aina ya viongozi wanaotakiwa katika karne hii! We don’t talk of INTERNATIONAL RELATIONS now days but we talk of INTERNATIONAL COOPERATION, no longer INTERNATIONAL DIPLOMACY but ECONOMIC DIPLOMACY! Moyo unaniuma kwelikweli huku ukinikereketa na kumlaani Kenyatta kimoyo moyo kwa kumuona ana-betray EAC! Lakini ukweli utabaki pale pale kwamba sina lolote zaidi ya wivu tu; tena wivu wa kijinga! Wivu wa kijinga wa kuona tunapigwa bao la kisigino huku tukiendelea kuvuta shuka! Matongotongo yakinitoka nitabaini wazi kwamba Kenyatta si rais wa EAC bali ni wa Kenya; so KENYA FIRST, East Africa baadae! Tuache SIASA KALE!

Maana ya yote hayo ni nini? Kulalamika, kunung’unika, ama kupiga kelele katu hakutatusaidia Watanzania! Viongozi wanatakiwa kuamka na kuweka mbele maslahi ya Tanzania. Dunia ya leo ina-operate kwenye soko huru, where market force ndio inayo-determine everything. Kenyatta ni bepari, ameona loophole na hivyo kuamua kuitumia for the interest of Kenya! Loophole kubwa aliyoiona Kenyatta ni miundombinu ya uhakika kwenda land locked areas; PERIOD! Hivi tulitarajia Kenyatta aishirikishe Tanzania katika kuimarisha miundombinu kuelekea Uganda na Rwanda? Unless kama angekuwa ni one of the foolishEST leaders ever happened in African History. Atushirikishe ili iweje? Frankly speaking, nadhani leo hii Mheshimiwa Kikwete akiulizwa achagua moja kati ya kuizamisha Bandari ya Tanga au Mombasa, sina shaka anaweza kuchagua Tanga ili “ndugu zetu” Wakenya wasikose kabisa bandari! Lakini kwa upande mwingine kama Kenyatta ataulizwa izamishwe Bandari ipi kati ya ile ya Dar es salaam au ya Kilwa; haraka haraka atajibu zamisha ya Dar es salaam, ya Kilwa itawatosha! Ukiyasoma haya juu juu, hutanielewa!

Kenyatta na Kenya wameamua kutumia loopholes/opportunities! Nadhani badala ya Watanzania kulalamika sasa tutumie fursa zilizopo! Kwa kuangalia ramani, Biharamulo panaonekana kama ni sehemu ambayo ni rahisi kufikika kutokea Uganda, Rwanda na Burundi; and in fact hata DRC! Sasa kwanini tusiwe na largest Inland Container Terminal pale kisha Biharamulo ikaunganishwa na reli kutokea Dar es salaam ambayo inakuwa chini ya TPA? Kwamba mzigo wa Rwanda, Burundi, Uganda na DRC utakuwa umefika Tanzania pale tu unapokuwa tayari umeshafika Biharamulo. Hii maana yake ni kwamba, Importers kutoka mataifa hayo badala ya kuja Dar, wanafuata mizigo yao Biharumlo na Exportes badala ya kuleta mzigo Dar, wanafikisha Biharamulo au popote pale patakapoonekana ni very strategic! Hili likifanyika, hata kama kutakuwa na reli za vioo kutoka Mombasa hadi Kigali/Kampala/Bujumbura bado wafanyabiashara wa huko wata-opt kwenda kutumia Dar Via Biharamulo unless tushindwe kuwa efficient! Efficient kubwa ninayozungumzia hapa ni rate at which mizigo itakuwa evacuated. Kwanini tusiwe na a very large TPA’s Inland Container Terminal sehemu kama Tunduma ambayo ita-cater wafanyabiashara wa Zambia, South and South East DRC, Zimbabwe na Malawi?

Kwanini tusiwe na mpango wa makusudi kufanikisha haya? Tukisubiri Mchina, imekula kwetu; isitoshe Mchina anataka Bandari ya Bagamoyo wakati hata hiyo ya Dar hakuna efficiency! Why don’t we have something like SAVINGS BEFORE BUDGET SCHEMES (SBBS)? Hata kama hakuna kitu kama hicho duniani; si dhambi sisi tukiwa wa kwanza! Kwamba, tunaweka sheria kabisa before anything, 10% ya mapato ghafi ya TRA ya kila mwezi, yanaenda moja kwa moja SBBS FUND na hiyo 90% inayobaki ndiyo inaenda kwenye mzunguko wa kawaida! Isitoshe, nadhani SBBS inaweza kusababisha uwepo wa matumizi mazuri ya serikali. Si ajabu haya matumizi yasiyo na maana wakati mwingine yanatokea kwavile watu wanaona kuna fedha nyingi; kwanini wasinunue magari ya fahari wakati wanaona fedha ipo?!
NAWAKILISHA!
Jamaa umeshusha nondo za maana. International diplomacy ifike ukomo. Habari ya kunywa chai na Zimbabwe, S.A, Mozambique etc tukizungumzia ukomredi; halaf Kenya ndio inakua the 2nd largest exporter in Comesa: zifike mwisho


tragedy of the commons
 
Da !!!kichwa kinauma nimesoma nimeelewa ,,,

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Back
Top Bottom