EAC Crisis: Who’s the catalyst?...Pres. Kagame or Kenyatta?

reandle

JF-Expert Member
Joined
May 6, 2009
Posts
11,166
Reaction score
8,152
Si ajabu wengi wetu hatufahamu yale ambayo yalisababisha kuvunjika kwa EAC ya awali; sana sana tunafahamu hayo kupitia maandiko tu. Pamoja na hayo, wengi wetu hapa tunafahamu juu ya kufufuliwa upya kwa jumuiya hiyo. Kwa kurejea tu ni kwamba, EAC ilianza kufufuliwa kipindi ambacho Rais Daniel Arap Moi alishakuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Hali kadhalika, hata Rais Museveni nae alishakuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi vile vile. Kwa upande mwingine, Rais wa Tanzania enzi hizo, Mheshimiwa Benjamini Mkapa alikuwa hajatimiza hata miaka mitano madarakani! Na kama kumbukumbu zangu zipo sawa, ni kwamba harakati za kufufuliwa EAC zilianza ama zilipamba moto miaka michache tu tangu Mkapa aingie madarakani. Hii maana yake ni nini? Akili ya kawaida katika hili inashawishi kwamba, kuna kila dalili kwamba Benjamin Mkapa alikuwa ndie CATALYST ya ufufuliwaji upya wa EAC. Wana Habari na wale watu wa serikalini tangu zamani labda wanaweza kulieleza vizuri jambo hili vinginevyo niatendelea kushawishika kwamba Mkapa ndie ali-push kufufuliwa EAC coz’ Museveni na Moi walishakuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi lakini hapakutokea kitu kama hicho!

Hayo yote kwa sasa ni historia lakini ni muhimu katika kutafuta marejeo. Historia ni mwalimu mzuri. TUENDELEE.
Hivi sasa mtu hahitaji kuwa na shahada ya uhusiano wa kimataifa kufahamu kwamba jumuiya ya Afrika Mashariki ipo mashakani! Wengi wa Watanzania, hususani wana Jamii Forums tumekuwa tukimshutumu sana Kagame kwamba ndie chanzo cha yote haya! Humu jukwaani tumemshambulia sana Kagame kwa lugha mbalimbali; za kiungwana na hata zile za kinyume chake! Niseme wazi, mimi ni miongoni mwa wale ambao nimetupa makombora mazito mazito kwa Kagame! Nimepata kumuita Kagame kwa majina mbalimbali kama vile muuaji na mpenda vita! Nitamke tu kwamba, kwa kawaida akili yangu huwa inakwenda likizo ninapoona kiumbe chochote kinaingilia maslahi ya nchi hii!
Hata hivyo, hatimae akili ikarudi kutoka vacation! Hapo tena nikajiuliza; hivi CATALYST ni KAGAME kweli? Mbona ni kama akili iliyorejea kutoka vacation inanishawishi kwamba CATALYST sio Kagame bali ni KENYATTA?

Kwanza tuwekane sawa, hususani kwa wale ambao walikuwa wanalikimbia somo la Chemistry. WHAT’S A CATALYST?
Kwa kifupi ni kwamba, A Catalyst is a substance which ALTERS the rate of chemical reaction! Ikiwa kumbukumbu zangu zipo sawa, nadhani tafsiri yake inamalizia kwa kusema “but remains unchanged at the end of reaction.”
Ku-alter manake ni kwamba ama ita-speed up the rate of chemical reaction au ita-slow down. Kwa kiswahili chepesi, A Catalyst is like KICHOCHEO! Sasa ni nani basi kati ya Kagame na Kenyatta tunaeweza kumuita a CATALYST/KICHOCHEO? Kama ni Kagame, mbona haya hayakutokea zamani wakati Kagame alishakuwa madarakani tangu enzi hizo? Ni kwanini haya yametokea miezi michache tu tangu Kenyatta aingie madarakani? Is it Kagame or Kenyatta?

Kama mtu atanitaka niwaelezee kwa sentensi fupi sana watu hawa ni kwamba Kagame ni one of the most ambitious leader ever happened in EA history! He’s also The War Monger, hili halina mjadala! Huyo ni Kagame! Lakini kwa upande mwingine, Kenyatta ni one of the Capitalist Leader ever happened in EA history! While Kagame is so ambitious politically and political power, Kenyatta is so ambitious economically and economical power! Kenyatta ni bebari kwa tafsiri zozote zile! Kwa hulka zao, watu wa aina hii wana expansionism motives; however, economical expansionism.
Turudi kwa EAC crisis. Hivi ni nini hasa kinachotafutwa pale kwa hivi sasa? Is it political/power or economical motive? Watu wanazungumzia kuziunganisha nchi zao kwa reli, barabara, bandari and so on! Wanazungumzia ku-speed up suala la kuwa na single currency! Are all those political or economical motives? Sidhani kama panahitajika shahada kufahamu kwamba kinachopiganiwa sana hapo ni maslahi ya kiuchumi; at least kwa sasa! Kama ndivyo, sasa ni nani basi anaweza kuwa the catalyst kati ya Kagame who’s so ambitious for political power au Kenyatta ambae ni so ambitious economically? Huku tukijiuliza hayo, bado tunatakiwa kutojisahaulisha kwamba “mbona haya hayakuwapo huko nyuma?”

WHERE DO I STAND?

I HATE ANY LEADER WHO’S SO AMBITIOUS FOR POWER! Hata hivyo, I’ll always ADORE ANY LEADER WHO’S SO AMBITIOUS FOR ECONOMICAL POWER provided he’s doing so at a national level, meaning kwa ajili ya taifa lake! Kenyatta is one of the Richest Leader in Africa! So, nashawishika kuamini kwamba ambition hii aliyonayo Kenyatta kwa sasa ni kutafuta maslahi makubwa ya kiuchumi kwa nchi yake! BTW, hata harakati zenyewe hazionekani kama ni za personal interest zaidi ya kuonekana kama ni for the national interest. Hata kama roho inanikereketa na kunichonyota lakini lazima niseme wazi kwamba BRAVO KENYATTA! Hao ndio aina ya viongozi wanaotakiwa katika karne hii! We don’t talk of INTERNATIONAL RELATIONS now days but we talk of INTERNATIONAL COOPERATION, no longer INTERNATIONAL DIPLOMACY but ECONOMIC DIPLOMACY! Moyo unaniuma kwelikweli huku ukinikereketa na kumlaani Kenyatta kimoyo moyo kwa kumuona ana-betray EAC! Lakini ukweli utabaki pale pale kwamba sina lolote zaidi ya wivu tu; tena wivu wa kijinga! Wivu wa kijinga wa kuona tunapigwa bao la kisigino huku tukiendelea kuvuta shuka! Matongotongo yakinitoka nitabaini wazi kwamba Kenyatta si rais wa EAC bali ni wa Kenya; so KENYA FIRST, East Africa baadae! Tuache SIASA KALE!

Maana ya yote hayo ni nini? Kulalamika, kunung’unika, ama kupiga kelele katu hakutatusaidia Watanzania! Viongozi wanatakiwa kuamka na kuweka mbele maslahi ya Tanzania. Dunia ya leo ina-operate kwenye soko huru, where market force ndio inayo-determine everything. Kenyatta ni bepari, ameona loophole na hivyo kuamua kuitumia for the interest of Kenya! Loophole kubwa aliyoiona Kenyatta ni miundombinu ya uhakika kwenda land locked areas; PERIOD! Hivi tulitarajia Kenyatta aishirikishe Tanzania katika kuimarisha miundombinu kuelekea Uganda na Rwanda? Unless kama angekuwa ni one of the foolishEST leaders ever happened in African History. Atushirikishe ili iweje? Frankly speaking, nadhani leo hii Mheshimiwa Kikwete akiulizwa achagua moja kati ya kuizamisha Bandari ya Tanga au Mombasa, sina shaka anaweza kuchagua Tanga ili “ndugu zetu” Wakenya wasikose kabisa bandari! Lakini kwa upande mwingine kama Kenyatta ataulizwa izamishwe Bandari ipi kati ya ile ya Dar es salaam au ya Kilwa; haraka haraka atajibu zamisha ya Dar es salaam, ya Kilwa itawatosha! Ukiyasoma haya juu juu, hutanielewa!

Kenyatta na Kenya wameamua kutumia loopholes/opportunities! Nadhani badala ya Watanzania kulalamika sasa tutumie fursa zilizopo! Kwa kuangalia ramani, Biharamulo panaonekana kama ni sehemu ambayo ni rahisi kufikika kutokea Uganda, Rwanda na Burundi; and in fact hata DRC! Sasa kwanini tusiwe na largest Inland Container Terminal pale kisha Biharamulo ikaunganishwa na reli kutokea Dar es salaam ambayo inakuwa chini ya TPA? Kwamba mzigo wa Rwanda, Burundi, Uganda na DRC utakuwa umefika Tanzania pale tu unapokuwa tayari umeshafika Biharamulo. Hii maana yake ni kwamba, Importers kutoka mataifa hayo badala ya kuja Dar, wanafuata mizigo yao Biharumlo na Exportes badala ya kuleta mzigo Dar, wanafikisha Biharamulo au popote pale patakapoonekana ni very strategic! Hili likifanyika, hata kama kutakuwa na reli za vioo kutoka Mombasa hadi Kigali/Kampala/Bujumbura bado wafanyabiashara wa huko wata-opt kwenda kutumia Dar Via Biharamulo unless tushindwe kuwa efficient! Efficient kubwa ninayozungumzia hapa ni rate at which mizigo itakuwa evacuated. Kwanini tusiwe na a very large TPA’s Inland Container Terminal sehemu kama Tunduma ambayo ita-cater wafanyabiashara wa Zambia, South and South East DRC, Zimbabwe na Malawi?

Kwanini tusiwe na mpango wa makusudi kufanikisha haya? Tukisubiri Mchina, imekula kwetu; isitoshe Mchina anataka Bandari ya Bagamoyo wakati hata hiyo ya Dar hakuna efficiency! Why don’t we have something like SAVINGS BEFORE BUDGET SCHEMES (SBBS)? Hata kama hakuna kitu kama hicho duniani; si dhambi sisi tukiwa wa kwanza! Kwamba, tunaweka sheria kabisa before anything, 10% ya mapato ghafi ya TRA ya kila mwezi, yanaenda moja kwa moja SBBS FUND na hiyo 90% inayobaki ndiyo inaenda kwenye mzunguko wa kawaida! Isitoshe, nadhani SBBS inaweza kusababisha uwepo wa matumizi mazuri ya serikali. Si ajabu haya matumizi yasiyo na maana wakati mwingine yanatokea kwavile watu wanaona kuna fedha nyingi; kwanini wasinunue magari ya fahari wakati wanaona fedha ipo?! UKishakuwa na SBBS, vipaumbele vitazingatiwa coz’ budget itakuwa ishafinywa in advance! I hope, hili likifanyika basi after 5 years SBBS inaweza kuwa na at least TSh. 2 Trillions ambazo zinaweza kuanzia kwenye program za makusudi kama hizo za ujengwaji wa njia za reli na program zingine zote.

NAWAKILISHA!
 
Mchakato unaendelea kama ulivopangwa , tatizo ni inhibitor(negative catalyst) TZ-ccm(s) inapunguza overall reaction rate.
 
Unless kama uliwataka hao TZ-CCM wa-participate kwenye movement inayoendelea....kwamba nao wawe ni part and parcel ya harakati ambazo Uganda, Kenya na Rwanda wanafanya! Kwa mtazamo wangu, hadi sasa Tanzania wapo sahihi! Huwezi kushiriki mchakato ambao utatuua wenyewe! Hapa nawaunga mkono kwa 100% isipokuwa wanatakiwa kujipanga ili kukabiliana na threat hiyo na sio kumlaumu Kenyatta wala Kagame. Kagame nae ni lazima aangalie maslahi ya Rwanda yake kabla ya EAC; so kama anaona ni much better kwao kuungana na Kenya na Uganda basi yupo sahihi! Sisi tunatakiwa kufanya vitendo vitakavyo-prove otherwise. Hata kama Kagame atakuwa na chuki zake binafsi kuhusu TZ; tukijizatiti chuki zake atabaki nazo mwenyewe na roho yake!! Hatuna shida na mizigo ya serikali ya Rwanda tuna shida na mizigo ya Rwanda! Akisusa kupitisha mizigo ya serikali, wafanyabiashara wa huko watapitisha tu ikiwa huku kutakuwa mazingira mazingira nafuu kwao kibiashara! Anaweza ku-impose tax ku-discourage lakini Kagame au Museveni hawatakuwa madarakani milele; obvious watakuja viongozi ambao ni rational decision makers.
 
Nimekusoma na kukuelewa vyema mkuu,adui wa Tanzania katika shirikisho hili si Kagame kama wengi tunavyodhani bali ni Kenyatta.Nakuunga mkono mbandika mada hii,kwamba kenyatta ni kiongozi
mtaifa,anayeiangalia kenya kwanza na wengine baadae,hili nililishuhudia dhahiri wakati wa kampeni zake alipokuwa akitumia maneno ya kebei dhidi ya Tanzania,pale alipoiambia hadhara kuwa kama angelikuwa na shida ya kuwa kiongozi wa kawaida,asingeshindwa kuwa ata balozi wa Tanzania awatafutie wakenya kazi na mabiashara,hii kauli hili ni bugudhi na kunifanya kumchukia huyu jamaa,kuona kana kwamba atafanya juu chini kuiona nguvu ya Tanzania inayoendelea kuimarika katika kanda hii ikififia hili Kenya iendelee kuwa taifa linaloongoza daima kiuchumi katika jumuiya hii.

Minajiri tumeshamjua mchochezi wa ndoa yetu,hatuna budi kuangalia ni jinsi gani tunaweza kudili naye.Mapendekezo uliyoyatoa yanamanufaa makubwa kwa taifa letu kama yakifanyiwa kazi,nacho ogopa mie ni utashi wa viongozi wetu katika mambo haya.jeografia yetu inaturuhusu kuneemeka na kustawi kiuchumi kama tukiboresha miundombinu na mifumo ya uchukuzi.

Ubinafisi wa serikali ya Kenya na viongozi wake ndio utaolimaliza hili shirikisho.Museveni,Kikwete,Kibaki na Kagame wote walikuwepo,lakini hawajai kuishi na figisufigisu ya namna yoyote hile.Lakini bwana mdogo alipotinga ikulu ya Nairobi akaona yeye ndo mwenye kujua zaidi.Kama nilivyoeleza awali chuki zake na Tanzania azikuanza leo.Sometimes I wish Odinga had been elected not this hypocrite who manipulates other member states for his country solo interests,I call this one street relationship.
 
Acheni longolongo hakuna uadui wala chuki watu wanataka maendeleo tuu,Rwanda ilikuwa ya kwanza kuwa na deal na TZ kujenga Reli all the way to Kigali lakini kilichotokea ni unseriousness na usanii wa TZ project ikaishia kwenye makaratasi na siasa nyingi ambazo hazina mpango,leo wameamua ku7fanya projects kupitia Uganda/Kenya mnawaita maadui?mnacheza nyie na mtakaa na majungu tuu na kuongea nonsense huku Reli za watu zikijengwa,TZ kwa vitendo vyake ndio mvunjaji wa EA na wala asimlaumu mwingine na EA haitavunjika ila TZ ikiendelea hivi itawekwa pembeni tuu
 
Si ajabu wengi wetu hatufahamu yale ambayo yalisababisha kuvunjika kwa EAC ya awali; sana sana tunafahamu hayo kupitia maandiko tu. Pamoja na hayo, wengi wetu hapa tunafahamu juu ya kufufuliwa upya kwa jumuiya hiyo. Kwa kurejea tu ni kwamba, EAC ilianza kufufuliwa kipindi ambacho Rais Daniel Arap Moi alishakuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi. Hali kadhalika, hata Rais Museveni nae alishakuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi vile vile. Kwa upande mwingine, Rais wa Tanzania enzi hizo, Mheshimiwa Benjamini Mkapa alikuwa hajatimiza hata miaka mitano madarakani! Na kama kumbukumbu zangu zipo sawa, ni kwamba harakati za kufufuliwa EAC zilianza ama zilipamba moto miaka michache tu tangu Mkapa aingie madarakani. Hii maana yake ni nini? Akili ya kawaida katika hili inashawishi kwamba, kuna kila dalili kwamba Benjamin Mkapa alikuwa ndie CATALYST ya ufufuliwaji upya wa EAC. Wana Habari na wale watu wa serikalini tangu zamani labda wanaweza kulieleza vizuri jambo hili vinginevyo niatendelea kushawishika kwamba Mkapa ndie ali-push kufufuliwa EAC coz’ Museveni na Moi walishakuwa madarakani kwa zaidi ya miaka kumi lakini hapakutokea kitu kama hicho!

Hayo yote kwa sasa ni historia lakini ni muhimu katika kutafuta marejeo. Historia ni mwalimu mzuri. TUENDELEE.
Hivi sasa mtu hahitaji kuwa na shahada ya uhusiano wa kimataifa kufahamu kwamba jumuiya ya Afrika Mashariki ipo mashakani! Wengi wa Watanzania, hususani wana Jamii Forums tumekuwa tukimshutumu sana Kagame kwamba ndie chanzo cha yote haya! Humu jukwaani tumemshambulia sana Kagame kwa lugha mbalimbali; za kiungwana na hata zile za kinyume chake! Niseme wazi, mimi ni miongoni mwa wale ambao nimetupa makombora mazito mazito kwa Kagame! Nimepata kumuita Kagame kwa majina mbalimbali kama vile muuaji na mpenda vita! Nitamke tu kwamba, kwa kawaida akili yangu huwa inakwenda likizo ninapoona kiumbe chochote kinaingilia maslahi ya nchi hii!
Hata hivyo, hatimae akili ikarudi kutoka vacation! Hapo tena nikajiuliza; hivi CATALYST ni KAGAME kweli? Mbona ni kama akili iliyorejea kutoka vacation inanishawishi kwamba CATALYST sio Kagame bali ni KENYATTA?

Kwanza tuwekane sawa, hususani kwa wale ambao walikuwa wanalikimbia somo la Chemistry. WHAT’S A CATALYST?
Kwa kifupi ni kwamba, A Catalyst is a substance which ALTERS the rate of chemical reaction! Ikiwa kumbukumbu zangu zipo sawa, nadhani tafsiri yake inamalizia kwa kusema “but remains unchanged at the end of reaction.”
Ku-alter manake ni kwamba ama ita-speed up the rate of chemical reaction au ita-slow down. Kwa kiswahili chepesi, A Catalyst is like KICHOCHEO! Sasa ni nani basi kati ya Kagame na Kenyatta tunaeweza kumuita a CATALYST/KICHOCHEO? Kama ni Kagame, mbona haya hayakutokea zamani wakati Kagame alishakuwa madarakani tangu enzi hizo? Ni kwanini haya yametokea miezi michache tu tangu Kenyatta aingie madarakani? Is it Kagame or Kenyatta?

Kama mtu atanitaka niwaelezee kwa sentensi fupi sana watu hawa ni kwamba Kagame ni one of the most ambitious leader ever happened in EA history! He’s also The War Monger, hili halina mjadala! Huyo ni Kagame! Lakini kwa upande mwingine, Kenyatta ni one of the Capitalist Leader ever happened in EA history! While Kagame is so ambitious politically and political power, Kenyatta is so ambitious economically and economical power! Kenyatta ni bebari kwa tafsiri zozote zile! Kwa hulka zao, watu wa aina hii wana expansionism motives; however, economical expansionism.
Turudi kwa EAC crisis. Hivi ni nini hasa kinachotafutwa pale kwa hivi sasa? Is it political/power or economical motive? Watu wanazungumzia kuziunganisha nchi zao kwa reli, barabara, bandari and so on! Wanazungumzia ku-speed up suala la kuwa na single currency! Are all those political or economical motives? Sidhani kama panahitajika shahada kufahamu kwamba kinachopiganiwa sana hapo ni maslahi ya kiuchumi; at least kwa sasa! Kama ndivyo, sasa ni nani basi anaweza kuwa the catalyst kati ya Kagame who’s so ambitious for political power au Kenyatta ambae ni so ambitious economically? Huku tukijiuliza hayo, bado tunatakiwa kutojisahaulisha kwamba “mbona haya hayakuwapo huko nyuma?”

WHERE DO I STAND?

I HATE ANY LEADER WHO’S SO AMBITIOUS FOR POWER! Hata hivyo, I’ll always ADORE ANY LEADER WHO’S SO AMBITIOUS FOR ECONOMICAL POWER provided he’s doing so at a national level, meaning kwa ajili ya taifa lake! Kenyatta is one of the Richest Leader in Africa! So, nashawishika kuamini kwamba ambition hii aliyonayo Kenyatta kwa sasa ni kutafuta maslahi makubwa ya kiuchumi kwa nchi yake! BTW, hata harakati zenyewe hazionekani kama ni za personal interest zaidi ya kuonekana kama ni for the national interest. Hata kama roho inanikereketa na kunichonyota lakini lazima niseme wazi kwamba BRAVO KENYATTA! Hao ndio aina ya viongozi wanaotakiwa katika karne hii! We don’t talk of INTERNATIONAL RELATIONS now days but we talk of INTERNATIONAL COOPERATION, no longer INTERNATIONAL DIPLOMACY but ECONOMIC DIPLOMACY! Moyo unaniuma kwelikweli huku ukinikereketa na kumlaani Kenyatta kimoyo moyo kwa kumuona ana-betray EAC! Lakini ukweli utabaki pale pale kwamba sina lolote zaidi ya wivu tu; tena wivu wa kijinga! Wivu wa kijinga wa kuona tunapigwa bao la kisigino huku tukiendelea kuvuta shuka! Matongotongo yakinitoka nitabaini wazi kwamba Kenyatta si rais wa EAC bali ni wa Kenya; so KENYA FIRST, East Africa baadae! Tuache SIASA KALE!

Maana ya yote hayo ni nini? Kulalamika, kunung’unika, ama kupiga kelele katu hakutatusaidia Watanzania! Viongozi wanatakiwa kuamka na kuweka mbele maslahi ya Tanzania. Dunia ya leo ina-operate kwenye soko huru, where market force ndio inayo-determine everything. Kenyatta ni bepari, ameona loophole na hivyo kuamua kuitumia for the interest of Kenya! Loophole kubwa aliyoiona Kenyatta ni miundombinu ya uhakika kwenda land locked areas; PERIOD! Hivi tulitarajia Kenyatta aishirikishe Tanzania katika kuimarisha miundombinu kuelekea Uganda na Rwanda? Unless kama angekuwa ni one of the foolishEST leaders ever happened in African History. Atushirikishe ili iweje? Frankly speaking, nadhani leo hii Mheshimiwa Kikwete akiulizwa achagua moja kati ya kuizamisha Bandari ya Tanga au Mombasa, sina shaka anaweza kuchagua Tanga ili “ndugu zetu” Wakenya wasikose kabisa bandari! Lakini kwa upande mwingine kama Kenyatta ataulizwa izamishwe Bandari ipi kati ya ile ya Dar es salaam au ya Kilwa; haraka haraka atajibu zamisha ya Dar es salaam, ya Kilwa itawatosha! Ukiyasoma haya juu juu, hutanielewa!

Kenyatta na Kenya wameamua kutumia loopholes/opportunities! Nadhani badala ya Watanzania kulalamika sasa tutumie fursa zilizopo! Kwa kuangalia ramani, Biharamulo panaonekana kama ni sehemu ambayo ni rahisi kufikika kutokea Uganda, Rwanda na Burundi; and in fact hata DRC! Sasa kwanini tusiwe na largest Inland Container Terminal pale kisha Biharamulo ikaunganishwa na reli kutokea Dar es salaam ambayo inakuwa chini ya TPA? Kwamba mzigo wa Rwanda, Burundi, Uganda na DRC utakuwa umefika Tanzania pale tu unapokuwa tayari umeshafika Biharamulo. Hii maana yake ni kwamba, Importers kutoka mataifa hayo badala ya kuja Dar, wanafuata mizigo yao Biharumlo na Exportes badala ya kuleta mzigo Dar, wanafikisha Biharamulo au popote pale patakapoonekana ni very strategic! Hili likifanyika, hata kama kutakuwa na reli za vioo kutoka Mombasa hadi Kigali/Kampala/Bujumbura bado wafanyabiashara wa huko wata-opt kwenda kutumia Dar Via Biharamulo unless tushindwe kuwa efficient! Efficient kubwa ninayozungumzia hapa ni rate at which mizigo itakuwa evacuated. Kwanini tusiwe na a very large TPA’s Inland Container Terminal sehemu kama Tunduma ambayo ita-cater wafanyabiashara wa Zambia, South and South East DRC, Zimbabwe na Malawi?

Kwanini tusiwe na mpango wa makusudi kufanikisha haya? Tukisubiri Mchina, imekula kwetu; isitoshe Mchina anataka Bandari ya Bagamoyo wakati hata hiyo ya Dar hakuna efficiency! Why don’t we have something like SAVINGS BEFORE BUDGET SCHEMES (SBBS)? Hata kama hakuna kitu kama hicho duniani; si dhambi sisi tukiwa wa kwanza! Kwamba, tunaweka sheria kabisa before anything, 10% ya mapato ghafi ya TRA ya kila mwezi, yanaenda moja kwa moja SBBS FUND na hiyo 90% inayobaki ndiyo inaenda kwenye mzunguko wa kawaida! Isitoshe, nadhani SBBS inaweza kusababisha uwepo wa matumizi mazuri ya serikali. Si ajabu haya matumizi yasiyo na maana wakati mwingine yanatokea kwavile watu wanaona kuna fedha nyingi; kwanini wasinunue magari ya fahari wakati wanaona fedha ipo?! UKishakuwa na SBBS, vipaumbele vitazingatiwa coz’ budget itakuwa ishafinywa in advance! I hope, hili likifanyika basi after 5 years SBBS inaweza kuwa na at least TSh. 2 Trillions ambazo zinaweza kuanzia kwenye program za makusudi kama hizo za ujengwaji wa njia za reli na program zingine zote.

NAWAKILISHA!

NasDaz; umemaliza yote!! Kwa kuwa wahusika wanapita sana hapa..hata mzee wa Magogoni nae hupita sana hapa, hivyo habari hizi zimefika! Asante mzalendo mwenzangu!
 
Acheni longolongo hakuna uadui wala chuki watu wanataka maendeleo tuu,Rwanda ilikuwa ya kwanza kuwa na deal na TZ kujenga Reli all the way to Kigali lakini kilichotokea ni unseriousness na usanii wa TZ project ikaishia kwenye makaratasi na siasa nyingi ambazo hazina mpango,leo wameamua ku7fanya projects kupitia Uganda/Kenya mnawaita maadui?mnacheza nyie na mtakaa na majungu tuu na kuongea nonsense huku Reli za watu zikijengwa,TZ kwa vitendo vyake ndio mvunjaji wa EA na wala asimlaumu mwingine na EA haitavunjika ila TZ ikiendelea hivi itawekwa pembeni tuu
Achana na mawazo mfu wewe! Nani amezungumzia suala la uadui hapa? Yaani wewe kwa ufahamu wako unaona hii mada inajadili chuki za Kagame?!Hivi huwa unaelewa unaposoma au unakurupuka tu ku-post kabla hujasoma? Binafsi nimesema wazi kwamba kama ni tatizo si Kagame bali ni Kenyatta....hata hivyo, nikaenda mbele zaidi na kusema kwamba hata huyo Kenyatta huwezi kumlaumu coz' anachofanya ni right for the interest of his country na hata Kagame yupo right for the interest of Rwanda yake! Good enough, hata hapo kabla ya post yako, Mkuu Van persie nae ameunga mkono kwamba tatizo sio Kagame!! Sasa wewe unaemtolea mapovu nani? Au umekariri....kwamba ukiona thread inayozungumzia EAC au imetaja Kagame basi thread hiyo inaelezea maovu ya Kagame?! Uwe unaanza kusoma kabla hujakurupuka ku-post ndugu vinginevyo utapatwa na ugonjwa wa moyo coz' I know kila inapotokea thread kuhusu Kagame lazima uingie kum-defend!!
 
Pamoja sana, sina shaka kwamba tutafika tu mkuu wangu!
 
Nimekusoma na kukuelewa vyema mkuu,adui wa Tanzania katika shirikisho hili si Kagame kama wengi tunavyodhani bali ni Kenyatta.Nakuunga mkono mbandika mada hii,kwamba kenyatta ni kiongozi
mtaifa,anayeiangalia kenya kwanza na wengine baadae,hili nililishuhudia dhahiri wakati wa kampeni zake alipokuwa akitumia maneno ya kebei dhidi ya Tanzania,pale alipoiambia hadhara kuwa kama angelikuwa na shida ya kuwa kiongozi wa kawaida,asingeshindwa kuwa ata balozi wa Tanzania awatafutie wakenya kazi na mabiashara,hii kauli hili ni bugudhi na kunifanya kumchukia huyu jamaa,kuona kana kwamba atafanya juu chini kuiona nguvu ya Tanzania inayoendelea kuimarika katika kanda hii ikififia hili Kenya iendelee kuwa taifa linaloongoza daima kiuchumi katika jumuiya hii.

Minajiri tumeshamjua mchochezi wa ndoa yetu,hatuna budi kuangalia ni jinsi gani tunaweza kudili naye.Mapendekezo uliyoyatoa yanamanufaa makubwa kwa taifa letu kama yakifanyiwa kazi,nacho ogopa mie ni utashi wa viongozi wetu katika mambo haya.jeografia yetu inaturuhusu kuneemeka na kustawi kiuchumi kama tukiboresha miundombinu na mifumo ya uchukuzi.

Ubinafisi wa serikali ya Kenya na viongozi wake ndio utaolimaliza hili shirikisho.Museveni,Kikwete,Kibaki na Kagame wote walikuwepo,lakini hawajai kuishi na figisufigisu ya namna yoyote hile.Lakini bwana mdogo alipotinga ikulu ya Nairobi akaona yeye ndo mwenye kujua zaidi.Kama nilivyoeleza awali chuki zake na Tanzania azikuanza leo.Sometimes I wish Odinga had been elected not this hypocrite who manipulates other member states for his country solo interests,I call this one street relationship.
Mkuu,
uliyoeleza yote ni sahihi kwa 100%.....kwa hakika ndiyo yanayotakiwa kufahamika na viongozi wetu! Kenya ni ndugu zetu lakini si washirika wetu, hili ni muhimu sana viongozi wetu wakalifahamu! Kenya wanaweza kuwa washirika wazuri kwa kutuuzia chao lakini si kwa wao kununua chetu; wao watanunua chetu si kwa kutaka bali kwa shingo upande! Wakikumbwa na baa la njaa, watanunua tu mahindi yetu kwani ndiyo option rahisi! Hili ni muhimu sana wengi tukilifahamu! Hata hivyo, siwalaumu....any country should do what's best for her country; PERIOD!
 
Good thoughts on how to beat the competition., lakini labda niulize kwa mtazamo wako unadhani tunauhitaji muungano huu ( EAC)
Economically, BIG YES! EAC is ready our market! IN a simple Customer Management Principle; don' ever do anything that might cause you loose even a single customer! The hardest part in customer management is how to retain your customers but the most important part is to retain them! EAC is our market, means is our customer! No matter how many customers we have, we shouldn't get prepared to loose even a single from millions of customers you have!
 
Achana na mawazo mfu wewe! Nani amezungumzia suala la uadui hapa? Yaani wewe kwa ufahamu wako unaona hii mada inajadili chuki za Kagame?!Hivi huwa unaelewa unaposoma au unakurupuka tu ku-post kabla hujasoma? Binafsi nimesema wazi kwamba kama ni tatizo si Kagame bali ni Kenyatta....hata hivyo, nikaenda mbele zaidi na kusema kwamba hata huyo Kenyatta huwezi kumlaumu coz' anachofanya ni right for the interest of his country na hata Kagame yupo right for the interest of Rwanda yake! Good enough, hata hapo kabla ya post yako, Mkuu Van persie nae ameunga mkono kwamba tatizo sio Kagame!! Sasa wewe unaemtolea mapovu nani? Au umekariri....kwamba ukiona thread inayozungumzia EAC au imetaja Kagame basi thread hiyo inaelezea maovu ya Kagame?! Uwe unaanza kusoma kabla hujakurupuka ku-post ndugu vinginevyo utapatwa na ugonjwa wa moyo coz' I know kila inapotokea thread kuhusu Kagame lazima uingie kum-defend!!
Wee ----- usiharibu hii topic ingawaje umeileta mwenyewe na kila mtu anaweza kuandika upuuzi ujue so don't be a smartazz,msome van Persie anaongelea uadui ambao naona ndio longolongo tuu...anyway move on!!!
 
Safi sana mkuu..

Wazo kama hili la inland port nimewahi kulitoa hapa lakini nilitumia mji wa Kahama badala ya Biharamulo,

Lakini nafikiri kama wahusika wanasoma watakua wameelewa nini cha kufanya

Naunga mkono hoja

mawazo yangu yalikua haya

quote_icon.png
By asigwa

Hii ni move nzuri sana kwa viongozi wetu kama wana busara.

Kwa kuwa tayari DRC wameonesha nia ya kuingia EAC lakini mpaka Tanzania iwepo na kwa kuwa BURUNDI wanakuwa nyuma ya mgongo wa Tanzania, hapa ndipo pa kucheza karata yetu.

Kwamba wao wamemwaga ugali sisi tumwage mboga, tusitoke EAC lakini tuanzishe TANZANIAN BUSSINESS PARTNERS ambapo tutawachukua CONGO na BURUNDI kwa kuwa wote ni locked countries na matatizo yao yanafanana(vita vya ndani).Halafu tuingie mikataba na CONGO ya kiuchumi kabla ya kuipigia debe iingie EAC.

Sisi tunachotakiwa kufanya CONGO ikishaingia kule ni kujenga kituo cha kibiashara kikubwa sana pale KAHAMA na hii inakua strategically kwa ajili ya ku-connect biashara ya Burundi na CONGO kupitia bandari ya Tanga huku tukianza ku-destabilize biashara ya Rwanda na Uganda kupitia Mombasa.
Kama CONGO na Burundi zikiwa na amani na zikfanya biashara kupitia KAHAMA obvious kukua kwao kiuchumi kutaanza kuizorotesha RWANDA na UGANDA ambazo itabidi zinunue baadhi ya bidhaaa toka CONGO na BURUNDI ambazo zimepita Tanzania(KAHAMA). Na kwa vyovyote kwa mfumo wa free market hawawezi kundelea kupitisha bidhaa zao KENYA kwa kuwa ni gharama na chumi za nchi zinazowazunguka zimeshakua hivyo hawana jinsi isipokua kurudi KAHAMA.

Wakija huku tunawa-force waingie mikataba ya kibiashara na TANZANIA BUSSINES PARTNERS wasipotaka waondoke, Lazima wataingia ili kunusuru chumi zao na hapa Tanzania itakua imewini game ya kutengwa na kuwa na sauti kubwa ya kiuchumi katika ukanda huu..
 
Wee ----- usiharibu hii topic ingawaje umeileta mwenyewe na kila mtu anaweza kuandika upuuzi ujue so don't be a smartazz,msome van Persie anaongelea uadui ambao naona ndio longolongo tuu...anyway move on!!!
Koba mi nakufahamu wewe unavyomtetea Kagame, sikulaumu coz' it's none of my business lakini katika mada hii hakuna popote Kagame aliposemwa! Hebu msome vizuri Van persie, namnukuu "Nimekusoma na kukuelewa vyema mkuu,adui wa Tanzania katika shirikisho hili si Kagame kama wengi tunavyodhani bali ni Kenyatta.Nakuunga mkono mbandika mada hii,kwamba kenyatta ni kiongozi" BInafsi, wala sifichi na isitoshe nimeshasema kabla kwamba I've problem with Kagame lakini katika hili wala sina tatizo na Kagame zaidi ya kumuunga mkono; kwamba he's right kwani akiwa kama Rais wa Rwanda hana budi kuangalia maslahi ya Rwanda!

Hata hivyo, kuna jambo lingine la msingi ambalo kwa member mkongwe kama wewe ulitakiwa kulifahamu! Kwamba, usipo-quote post yoyote, by default utakuwa unaizungumzia the main post/thread ikiwa uta-comment anything! Tuachane na hayo, tuendelee!
 
Mkuu asigwa nilikuwa sijaona hiyo kitu yako before; probably kv hivi sasa nimeadimika sana hapa jamvini! It's very interesting kwamba wakati watu tunayaona haya lakini bado wengine wamebaki kulalamika tu!
 
Last edited by a moderator:
Acheni longolongo hakuna uadui wala chuki watu wanataka maendeleo tuu,Rwanda ilikuwa ya kwanza kuwa na deal na TZ kujenga Reli all the way to Kigali lakini kilichotokea ni unseriousness na usanii wa TZ project ikaishia kwenye makaratasi na siasa nyingi ambazo hazina mpango,leo wameamua ku7fanya projects kupitia Uganda/Kenya mnawaita maadui?mnacheza nyie na mtakaa na majungu tuu na kuongea nonsense huku Reli za watu zikijengwa,TZ kwa vitendo vyake ndio mvunjaji wa EA na wala asimlaumu mwingine na EA haitavunjika ila TZ ikiendelea hivi itawekwa pembeni tuu

Ngoja uone hizo projects zinakuja kuwa blocked mahakamani, tena waambie waende taratibu wasipate hasara kubwa!
 
Achana na mawazo mfu wewe! Nani amezungumzia suala la uadui hapa? Yaani wewe kwa ufahamu wako unaona hii mada inajadili chuki za Kagame?!Hivi huwa unaelewa unaposoma au unakurupuka tu ku-post kabla hujasoma? Binafsi nimesema wazi kwamba kama ni tatizo si Kagame bali ni Kenyatta....hata hivyo, nikaenda mbele zaidi na kusema kwamba hata huyo Kenyatta huwezi kumlaumu coz' anachofanya ni right for the interest of his country na hata Kagame yupo right for the interest of Rwanda yake! Good enough, hata hapo kabla ya post yako, Mkuu Van persie nae ameunga mkono kwamba tatizo sio Kagame!! Sasa wewe unaemtolea mapovu nani? Au umekariri....kwamba ukiona thread inayozungumzia EAC au imetaja Kagame basi thread hiyo inaelezea maovu ya Kagame?! Uwe unaanza kusoma kabla hujakurupuka ku-post ndugu vinginevyo utapatwa na ugonjwa wa moyo coz' I know kila inapotokea thread kuhusu Kagame lazima uingie kum-defend!!

Mkuu naomba Usibishane na huyu,hawa ndio wabongo halisia,waliojaa madarakani ambao hawana mipango mirefu ya kiuchumi na Nchi Yao,hasa linapokuja suala la mahusiano ya kimataifa,wamekalia kutafuta sifa kwa kuingilia vitu visivyo na manufaa kwa taifa ili jamii ya kimataifa iwasifie,lakini badala ya kisifiwa wanachekwa na kung'ong'wa na wenzao wanappwageuzia migongo,hii uliyotoa ni analysis nzuri sana na ingeweza kusaidia wale wa Foreign affairs kubadilisha Foreign Policies zao,Leo kukiwa na ugomvi Kenya tutakuwa wa kwanza kurukia huo ugomvi ili tuusuruhishe,ila Kama kuna opportunity ya kufanya biashara na Rwanda na Nchi nyingine hakuna atakayefatilia jinsi ya kuwavutia wanyarwanda kufanya biashara na sisi,ni muda sasa umefika wa hizi bongo zetu zilizolala kuamka na kufanya vitu in our NATIONAL'S BEST INTEREST!
 
Watu wanaongelea Congo kujiunga na EAC, wakati huo huo, hao Congo waliingizwa kwa haraka haraka kule SADC kwa sababu Mugabe alitaka kuchuma rasilimali za Congo zikamtokea puani. Nchi haiendelei ati kwa sababu imeungana na nchi flani. Mipango ya serikali kuwakwamua raia wake kwenye uchovu na umasikini uliokubuhu ndio unaweza kuwaendeleza wananchi. (Tofauti tunayoiona ni viongozi kujilimbikizia mali baada ya kuuza mashirika ya uma kwa bei ya peremende na kuhakikisha hata yale yaliyokuwa yanafanya vizuri kuwekewa komeo yasifanye kazi zake kama vile NIC, shirika la simu reli nk.)

Sio siri Kenya wanahaha hivi sasa kutokana na mambo mawili makubwa uchumi wao ambao kwa kiasi kikubwa unashikiliwa na wageni ambao wanamkakati wa kuongeza wigo ili waendelee kutapika maslahi yao. Pili ni ukosefu wa ardhi ambayo inamilikiwa na wachache ambao wanaishi Ulaya. (Rejea machafuko baada ya uchaguzi uliopita ... .... ICC inawangoja) Rwanda na Burundi waliingizwa kwenye shirikisho haraka haraka vile vile wana tatizo la ardhi kutokana na population yao kuwa kubwa. Uchu wao ni kuona wanateka ardhi ya Tanzania na kuja kuneemeka kwenye rasilimali zetu. Ikumbukwe ni nchi hizi hizi ndizo zinaendelea kutubeza ati hatuna cha kujivunia lakini hawaishi kutamani kumiliki vipande vya ardhi na kuleta bidhaa zao zisizo na viwango kwa raia wetu.

Hatuwezi kuingia kwenye miungano bandia ati kwa sababu M7 au Kagame wanataka iwe hivyo. Viongozi tulionao ndio chimbuko la wizi wa rasilimali na utajiri wa nchi yetu. Tumeona jinsi Mkapa, na sasa Jakaya jinsi walivyojitajirisha kwa muda mfupi tangu waingie madarakani, tunaona jinsi wanavyotaka kujihami ili baadaye wasiweze kushitakiwa ati kwa sababu tu wanataka kuwa na ushirikiano haramu na kuwa na njia ya kujificha.

Je, Jakaya au Mkapa wanaweza kweli Kutueleza kwa nini hadi leo hii tunakuwa na mijadala ya raia wa Tanzania kuficha pesa Switzerland? Au kwa nini hadi leo hii watanzania hawaelewi kwa nini Loliondo iliuzwa kwa siri na rais Mwinyi? Kikwete hawezi kusema lolote kwa sababu Mwinyi ndiye aliyemleta na udhaifu wa Mkapa ndio uliomletea neema. Ndio sababu hadi leo hii rasilimali za madini zinachotwa bila wanaochimba kulipa kodi inayotakiwa kwa sababu tu Jakaya anamiliki hisa kule Byankulu.

Maendeleo hayataletwa na wageni ambao wanafikiria jinsi ya kutatua matatizo yao, maendeleo yataletwa na chimbuko la ndani la mikakati, mipango bora pamoja na kuondoa viongozi wezi ambao tunao hivi sasa hayo yakuwa CHACHU YA KULIONDOA TAIFA HILI KWENYE UVUNDO WA DARK AGES.
 
Back
Top Bottom