EAC bado ipo?Mambo yanayoendelea Mh. Sitta anasemaje?

EAC bado ipo?Mambo yanayoendelea Mh. Sitta anasemaje?

mwene original

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2013
Posts
248
Reaction score
48
Nimekuwa nikijiuliza katika mambo mbalimbali ambayo yamefanyika kwa nchi za Kenya,uganda na Rwanda kukaa vikao vya pamoja kama EAC bila Tanzania kuwepo na jana wamezindua ID itayowafanya watalii kutumia katika nchi zao,na tukumbuke mwezi moja na nusu uliopita hao watu walikutana na kufanya kikao kuhusu kuboresha bandari ya Mombasa bila Tanzania kuwepo.

Sasa nashangaa hadi leo waziri wa Tanzania mwenye dhamana na EA hawaambii wananchi wake kama EAc ipo hai au ilishakufa na kama ilishakufa?

Sitta tunaomba majibu,pamoja na wadau wengine kama mnajua chochote kuhusu hili?
 
Jumuiya ya afrika mashariki ilikufa rasmi baada ya matukio mawili:
1. Baada ya kikao cha siri cha rais kagame, yoweri kaguta mseven(msaba), na uhuru muigai kenyatta
2. Baada ya kagame kuukataa ushauri wa kukaa meza moja na interahammwe ili kujadili amani ya rwanda
tukio hili la pili ni kama lilishika panga la kukata kata jumuiya ya afrika mashariki . Kitendo cha dc kagame kuujibu ushauri wa JK kwa kejeli na matusi si tu umeukasirisha umma wa watatnzania lakini pia umeudhalililisha. Watanzania wanamuona kagame kama jirani ambaye hana shukrani kwa ukarimu ambao tz imekuwa ikitoa kwa wakimbizi toka rwanda kwa miongo mingi sasa.
Kwanza jumuiya hii ilitiliwa shaka kutoka na muelekeo wake hasa mustakhabali WA TANZANIA kutokana ukweli (FACTS) ufuatao;
1. Tamaa ya kaguta msaba na general kagame kufanya fast tracking of east african federation hali yeye akipigia upatu kuchukua uraisi
2. Ukubwa na uwingi wa nchi na raslimali zilizoko tz haukumpa nafasi sana museven kuwa raisi wa KWANZA WA nchi mpya inyoaundwa kwa 60% ya ukubwa wake na Tanzania hali yeye akitoka uganda yenye ukubwa wa 20% wa eneo lote la east africa
3. historia iliyotawaliwa na mapinduzi na umwagaji damu na nchi zote za africa mashariki ispokuwa TANZANIA nA KENYA hadi siku za karibuni.
4. Katika masuala ya biashara kumezwa na wakenya janja ya nyani wa biashara na ujuzi
4. Hofu ya tanzania kuharakishiwa ongezeko na msongamano wa watu.
Angalia viwango hivi vya msongamano wa watu;
- tanzania watu 50 kwa kilometa kilometa ya eneo
- kenya watu >70 kwa kila kilometa ya eneo
- uganda watu 170 kwa kila kilometa ya eneo
- burundi watu 313 kwa kila kilometa ya eneo
- rwanda watu >500 kwa kila kilometa ya eneo( msongamano huu ni mkubwa kuliko ule wa nchi ya ubelegiji ambayo ina watu kama 300 kwa kila kilometa.
Hivyo hali ikiwas ndio hii ndio tanzania inaona shgirikisho hili linalenga zaidi kuganga zaidi njaa za majirani na yenyewe haitafaidika kabisa. Itaichukua takribani miaka 500 hivi kufikia msongamano ulioko rwanda. Sasa ya nini tuanze kuuungana na watu wanaozaliana kama simbilisi?.
TANZANIA KICHWA IPO .ACHA CHEZEA BONGOLAND
 
Tuelekeze nguvu zetu zaidi Sadc ndilo soko kubwa kupita la EAC. Ingawa rais wetu hajasema lolote kuhusu mwenendo huo lakini watanzania tunayo macho na masikio tunaona.

Muda mfupi tu ambao Rwanda imekaribishwa EAC tayari wanachama hawaaminiani. Tulilijadili mapema kabisa hapa JF kuwa kuingia kwa nchi hizo kutayumbisha EAC . Ilikuwa ni mapema sana kuwaingiza kwenye umoja kabla hawajaachana na ile sumu yao ya ubaguzi wao wa asili.
 
Napenda sana ushirikiano wa SADC hauna kulazimisha mambo kwa nguvu kama ilivyo jumuia ya Afrika mashariki. Hawa wenzetu wa Afrika mashariki wanataka tuungane chapuchapu/haraka haraka bila kufuata hatua.
 
Endapo Rais Kikwete angeitisha kura ya maoni leo ya kututaka tuendelee na EAC au tujitoe naamini watanzania wengi watasema tujitoe. Hii ina maana moja tu kuwa ni Rais kikwete ambaye ameshikiria hatima yetu kwenye jumuia hiyo.
 
Nilishawahi kupost siku za nyuma kuwa ndugu zetu ni SADC na sio EAC. Leo yanaanza kudhihirika.
 
Asili ya Jumuia ya Afrika Mashariki ni Nchi tatu tu, Tanzania,Kenya na Uganda huu muongezeko wa hizi Nchi mbili Rwanda na Burundi umefanyika kwa kuwa Nchi hizi tuko nazo karibu sana Kijiografia lakini siyo Kijamii. Nchi yetu Tanzania tumekuwa wahanga wa Wakimbizi kwa miongo kadhaa sasa na tumejitahidi sana kuwavumilia ndugu zetu hawa kwa kipindi hiko chote,lakini ninaamini kuwa kama matatizo ya ukimbizi yangekuwa yanatukuta sisi Watanzania basi hawa jirani zetu wangetunyanyasa sana! tumuombe Mungu na sisi wenyewe Watanzania tuilinde amani yetu kwa jinsi yoyote ile.

Nimesoma matusi na kejeli nyingi zilizotolewa na Rais wa Rwanda kwa Rais wetu wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kweli yamenisikitisha sana kwanza Kagame hana shukrani pili si mstaarabu na tatu ni Muuaji tena siyo wa kufikirika bali ni muuaji wa dhahiri! Kejeli za Kagame hazina kichwa wala miguu anashindwa kukumbuka nani waliomfikisha hapo alipo kama Rais.Tanzania ina mchango mkubwa sana kwa nafasi yake aliyokuwa nayo amepata mafunzo yake ya awali ya kijeshi pale Monduli ameishi Tanzania kama nyumbani kwake kwa miongo kadhaa kabla ya kujiunga na Museveni wakiwa na Meja Jenerali Fredy Rwejiema,mim naamini kuwa ushauri aliokuwa anaupata Kagame toka kwa Viongozi wa Tanzania wakati huo na mpaka sasa bado haujabadirika ni uleule,tuna msisitiza akae kwa amani na wale wote raia wenzake wa Rwanda,nchi ile si ya kwake pekee bali ni nchi ya wote raia wa Rwanda.

Dharau za Kagame ni matokeo ya tabia zake mbovu alizokuwa nazo toka yuko Tanzania.Mwalimu Nyerere alikuwa anamvumilia tu lakini alishindwa kufahamu kuwa huyu kijana atakuja kuwa msumbufu baadae matokeo yake ndiyo haya sasa sisi Watanzania tunapenda kuishi vizuri na majirani zetu kwa sababu hivi sasa tumeshachoka kuwapokea wakimbizi kila kunapokucha,kama wanashindwa kuishi vizuri nyumbani kwao basi wajue nasi hatutakuwa radhi kuwapokea tena ingawa tumesaini mkataba wa Kimataifa kuhusu Wakimbizi.
 
Sitta anahangaika kumtukana Lowassa kwamba anapitapita makanisani na misikitini, wakati huo huo na yeye akienda kanisani kuendesha harambee yenye ukomo wa Sh milioni 3 tu!!! Kwake Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kama anamkomoa aliyemteua!
 
Kagame sema suuu tuifute historia ya hiyo tarafa yako ndani ya dakika 10.
 
Back
Top Bottom