DW radio yamkaanga rais Magufuli

DW radio yamkaanga rais Magufuli

bne

JF-Expert Member
Joined
Oct 11, 2016
Posts
1,686
Reaction score
2,023
Katika taarifa ya habari ya Leo jioni redio DW Deutsche Welle, imetoa tahariri ndefu inayoonesha jinsi serikali ya Tanzania ilivyoshindwa kuendesha nchi badala yake serikali hiyo kutumia nguvu kubwa kulazimisha watu kukubali matakwa yake.

Wameendelea kuonanga serikali ya Tanzania kuwa ni serikali isiyofwata sheria na hata polisi nao wameshindwa kufwata sheria ktk kutimiza majukumu yao badala yake wanafanya kazi kulingana na matamko yanayotolewa na viongozi wa serikali.

Wametolea mfano jinsi wanasiasa wa wapinzani wanavyo kamatwa na kufunguliwa kesi zisizo na kichwa wala miguu ambazo kisheria hazina mashiko.

Wameonyesha wasiwasi mkubwa kuwa kwa sasa nchi inakoelekea siko kwani hata vyombo vya habari, mahakama na bunge vimekuwa passive isipokuwa mhimili mmoja tu wenye nguvu.

Pia wameonyesha kuwa serikali ya sasa kutokana na udhaifu wake imekuwa tayari kuhakikisha migogoro ndani ya vyama vya siasa ili kuvipunguza nguvu na wakatolea mfano CUF

Mwisho walimnukuu mh Tundu Lissu kuwa kwasasa nchi iko stage ya kwanza ya udikteta yaani u dikteta uchwara.
 
Ni bahati mbaya kelele zao haziwezi kumumfanya Mh. Rais aache kuinyoosha nchi. Wanapowaangalia akina Lissu basi wangekuwa wanawaangalia na wakulima pia. Lissu ni mpayukaji kukamatwa ni hadhi yake anayostahili.
 
Tuwekee sauti mkuu angalau

An ant on the move does more than a dozing ox.
 
Back
Top Bottom