Duuh!, ila wivu!

Duuh!, ila wivu!

Hello! jf members,

Je, ni sahihi kuwa na wivu kwa mpenzi wako akizungumza au kuchart na mtu mwingine ingali kuwa bado hujamuoa?
Kwani wivu unapangwa kwa mafungu kama njugu na kubandikwa lable?

Unaongozwa pa kupita na kuelekea kama misafara ya samuya!

Kwamba hapa panastahili na pale hapana?

Wivu unatokana na hisia za kimapenzi bila kubagua huyu ni mke, hawara au 'mtarajiwa'.

Wivu ni hisia za kimaumbile za wanyama wote chini ya jua.

Kuanza kuujadili wivu ambao humvamia mtu kama yavamiavyo maradhi ni kupoteza muda ama kutaka kuushika upepo kwa mikono mitupu, jambo lililo juu ya uwezo wa kibinadamu.

Shauri namna ya kuucontrol na si pa kuuelekeza, maana wivu ni janga kama yalivyo majanga mengine.
 
kuna jamaa sasa alimpiga demu kisa amemkuta anaongea na mtu mwingine
Huyo alivuka mpaka na huo siyo wivu bali ni unyanyasaji. Alijua wanaongea nini? Na hata kama walikuwa wanaongea mambo ya mapenzi, asingempiga. Kitu ambacho watu wanatakiwa kujua ni kwamba kumpiga mwenza wako siyo wivu bali ni unyanyasaji. BTW huyo aliyepigwa ''ana bahati sana'' kwa sababu ameshajua kama akiolewa na jamaa hataishi kwa amani. Akimbie haraka sana... Siku akiwa mke wake basi atamchinja kama kuku.
 
Back
Top Bottom