SALAMU ZA MWAKA MPYA ZA RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA MHESHIMIWA DKT. JAKAYA MRISHO KIKWETE KWA WATANZANIA,
TAREHE 31 DESEMBA, 2013
Ndugu wanajamvi, kipande hicho ni sehemu ya hotuba ya rais. Ningependa tukiangalie kipande kuhusiana na mada iliyopo.Ujangili wa Wanyamapori
Ndugu Wananchi;
Mwaka huu tuliongeza nguvu katika kupambana na ujangili wa wanyamapori na uvunaji haramu wa rasilimali za misitu. Hili ni tatizo la siku nyingi lakini katika miaka ya hivi karibuni limekuwa kubwa mno na kuwazidi nguvu Askari wa Wanyamapori na Maafisa Misitu.
Kwa nia ya kuwaongezea nguvu, mwaka 2010 niliagiza Jeshi la Polisi lisaidie Idara ya Wanyamapori na Idara ya Misitu katika kupambana na uhalifu huo. Operesheni kadhaa ziliendeshwa maeneo mbalimbali nchini na mafanikio ya kutia moyo yalipatikana. Lakini, kwa kutambua ukubwa wa tatizo na hasa kwa upande wa aina ya silaha na mbinu zinazotumiwa na majangili niliamua kuhusisha vyombo vingine vya usalama likiwemo Jeshi la Ulinzi. Nia ni kuongeza nguvu ya mapambano. Ndipo ilipoanzishwa "OPERESHENI TOKOMEZA".
Ndugu Wananchi;
Kazi nzuri imefanyika chini ya Operesheni hiyo. Mafanikio ya kuleta matumaini yameweza kupatikana. Mitandao ya ujangili imeweza kutambulika na wahusika wake kadhaa wametiwa nguvuni. Mitandao hiyo inahusisha watu wa aina mbalimbali. Wamo raia wa kawaida, wapo watu maarufu, wapo watumishi wa idara mbalimbali za Serikali wakiwamo wa Idara za Wanyamapori na Misitu. Watu 1,030 walikamatwa pamoja na silaha za kijeshi 18, za kiraia 1,579 na shehena kubwa za meno ya ndovu na nyara nyingine navyo vilikamatwa.Watu kadhaa tayari wameshafikishwa mahakamani.
Ndugu Wananchi;
Wahenga wamesema "kwenye wengi pana mengi". Katika utekelezaji wa Operesheni hii kumekuwepo na taarifa za kufanyika makosa kinyume na malengo na madhumuni ya Operesheni. Niliagiza baada ya kumalizika kwa awamu ya kwanza, zoezi lisitishwe kwa muda ili uchunguzi ufanyike, kasoro zitambuliwe na waliofanya makosa wachukuliwe hatua zipasazo. Wakati kazi hiyo inafanyika suala hilo lilijadiliwa Bungeni na Kamati Teule kuundwa. Matokeo yake sote tunayajua. Mawaziri wanne wamewajibika kisiasa.
Ndugu Wananchi;
Napenda kutumia nafasi hii kuwapa pole Mawaziri wetu hao kwa matatizo yaliyowakuta. Nawapongeza kwa uamuzi wa kukubali kuwajibika kwa makosa yaliyofanywa na maofisa wa chini yao. Wameonesha ukomavu wa kisiasa na kiuongozi wa hali ya juu na moyo wa uzalendo.
Kama mlivyosikia nitaunda Kamisheni ya Uchunguzi itakayoongozwa na Jaji wa Mahakama Kuu. Uchunguzi wa kina utafanywa kuhusu kadhia yote hiyo. Makosa yaliyofanyika yataainishwa na waliofanya kutambuliwa ili wachukuliwe hatua zipasazo kwa mujibu wa sheria na kwa mujibu wa kanuni za utumishi wa umma.
Ndugu Wananchi;
Ni muhimu kufanya hivi ili haki itendeke ipasavyo. Mtindo wa mzigo wa makosa ya watumishi wa umma kubebwa na viongozi wa kisiasa pekee, tena wasiokuwa na hatia ya moja kwa moja, siyo sahihi. Lazima kila mtu abebe mzigo wake inavyostahili. Ni matumaini yangu pia kwamba katika siku za usoni kunapotokea matatizo ya namna hii uchunguzi uwe wa kina ili wale hasa waliohusika na kutenda makosa wawajibishwe. Uwajibikaji wa wana-siasa peke yao hautoshi, kwani huwaacha waharibifu waendelee na kazi isivyostahili. Mtindo huu utawafanya watumishi wasione umuhimu wa kutokurudia makosa. Hata hivyo, pale kwenye ushahidi wa wazi kwamba kiongozi wa kisiasa angeweza kuchukua hatua za kuzuia madhara lakini hakufanya hivyo lazima kiongozi huyo awajibike.
Ogah, tatizo la viongozi waliopo ni kubwa kulikotunavyoliona.Hivi kuna ugumu gani wa kuwafahamu watendaji wa serikali wanaohujumu maliasili zetu.....mbona Dr. Mwakyembe kaingia Wizara ya Transport na kukuta uozo na kuchukua hatua....ingawa sio very effective.......atleast tunaweza kusema Mwakyembe amejaribu........
Hivi kweli Rais na Mawaziri wetu pamoja na vyombo vyote vilivyo chini yao anashindwa kuwa na taarifa za nani anahusika na ujangili au uhujumu wa maliasili zetu na kuchukua hatua?...........mpaka kila wakati tume ziundwe?.....I really miss Sokoine.........Hivi kwenye issue kama ya KIA......hivi kuna haja kweli ya kungoja tume iundwe ili watu wawajibishwe.....au kumuwajibisha mtu ni lazima umfukuze?.......
Inasikitisha sana unapoona Rais wa nchi anakubali kushindwa na wahujumu uchumu wa nchi yetu.....hiyo quote inaonyesha ni jinsi gani.....viongozi wetu ambavyo hawajui jinsi ya kutatua matatizo.....
Tatizo jingine walilonalo viongozi wetu ni kuwa....wanaposoma critics ndani ya JF wanakuwa offended......na kuanza kuleta kejeli kuwa watu wa JF......
Mkuu hapa umeleta point muhimu sana. Hakuna chochote kipya kama watendaji ni hao waliopo katika mtandao. Mh Rais anajua hilo lakini ujanja ujanja tu kwasababu wale watendaji hawapo kwa merit wapo kwa kufahamiana.Najaribu sana kujiuliza hivi hiyo kabineti mpya ya Mawaziri watakuwa na tofauti gani ktk wajibu wa kazi zao tofauti na hawa waloachishwa madaraka? Jamani ukweli tuuzungumze huyo waziri mpya atafanya nini kuzuia Mjangili ama mauaji ikiwa watendaji wetu ni wale wale walokuwa ktk mtandao wa Ujangili na mauaji?
........Kwamba tatizo la Tanzania si upungufu wa rasilimali watu au vinginevyo ni upungufu mkubwa wa utashi wa viongozi kusimamia kampeni dhidi ya Tembo. Ni kukosa dhamira ya kweli moyoni, na ni kukosa uchungu wa rasilimali ya nchi yetu
Ni ushiriki wa mtandao mkubwa uliopo serikali jambo lililosemwa na waziri aliyejiuzulu............
Ogah waziri Kagasheki aliposema majangili watandikwe risasi ile ilikuwa ni frustration ya kuona wanyama wanakwisha na jitihada zake zinakwamishwa na wanamtandao kwa kutumia serikali.Mkuu...huo ndio ukweli wenyewe.....wale wazalendo wachache waliopo wanapigwa vita......iweje Waziri awajibishwe Naibu wake abaki?......tena akapandishwa ngazi na kuwa Waziri kamili!!.......haya mambo ya urafiki rafiki na kuendekeza siasa kwenye mambo muhimu ya Kitaifa ndiyo yanayotu-cost kweli kweli.......
Ni kweli Majangili wanatumia udhaifu wetu kuhujumu maliasili zetu....period!