Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Duru za Siasa: 'Safari ya Dodoma'

Discussion in 'Great Thinkers' started by Nguruvi3, Sep 11, 2016.

 1. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #1
  Sep 11, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,168
  Likes Received: 4,726
  Trophy Points: 280
  SAFARI YA DODOMA

  Uamuzi wa kuhamia Dodoma ni tukio la 'kushtukiza' lililopokelewa kwa mshawasha na hisia

  Ni tukio lilozua taharuki kwa taasisi, watendaji ,wafanyakazi na jamii kwa ujumla

  Kadri siku zinavyosonga mbele mengi tuliyojadili yanajitokeza kwa sura tofauti

  Hoja kubwa si kuhamia Dodoma, bali utaratibu wa kuhamia Dodoma

  Wengi wanadhani ni suala jepesi kuhamisha makao makuu ya nchi

  Kuna kuchanganya mambo kati ya kuhamia Dodoma kama makao makuu ya nchi/serikali
  Halafu kuna kuhamia Dodoma kama kitovu cha shughuli za nchi ikiwemo biashara

  Makao makuu ya nchi na serikali ni sehemu maamuzi mengi ya kisera na utekelezaji hufanywa.

  Ndio msingi wa kuhamisha wizara na idara za serikali pamoja na mihimili mingine ya dola

  Haina maana ya kuhamisha shughuli za biashara. Dar es Salaam itabaki kuwa kitovu cha biashara kutokana na miundo mbinu yake na hata nafasi yake kijiografia ua idadi ya watu

  Tunaanza kuona ugumu wa kuhamia Dodoma kwa namna tofauti

  Maswali yanayojitokeza;
  Je, maamuzi ya kuhamia Dodoma yalifanyiwa marejeo na kuhakiwa kabla ya kutangazwa?
  Je, vyombo husika vilishirikishwa katika kupanga au kuonyesha 'concern' zao
  Je, ilikuwa suala la kuhamia Dodoma kwa haraka, au lilikuwa na plan za muda mrefu?
  Je, Mji wa Dodoma upo tayari kupokea ugeni utakaoongeza 'strain' huduma za umma?

  Kwa umuhimu wa suala hili, uzi utakuwa endelevu kujadili nini kinachoendelea

  Kwa kuanzia, tutarejea tuliyowahi kuyajadili nyuma

  Tusemezane
   
 2. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #2
  Sep 11, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,168
  Likes Received: 4,726
  Trophy Points: 280
  KULIKUWA NA MAREJEO KABLA YA KUPANGA SAFARI?

  Uamuzi wa kuhamia Dodoma ulifanywa miaka karibu ya 40 iliyopita na awamu ya kwanza

  Kwa mujibu wa wazee waliokuwepo, mpango huo ulikamwa kutokana na kuingilia na masuala mengine ya kipaumbele kwa Taifa kama uwepo wa vita ya Kagera

  Kutokana na hyo, uwezo wa kiuchumi ukawa tatizo na kila awamu ilikwepa jambo hilo

  Miaka 30+ ni mingi sana katika dunia hii inayokwenda kasi.
  Yapo mabadiliko ya kicuhumi, kisiasa na kijamii ambayo hayakuwepo uamuzi unatolewa

  Hii ni pamoja na mabadiliko katika eneo la teknolojia ambalo limekuwa na athari chanya au hasi katika sekta zote, iwe ujenzi, afya, mawasiliano, elimu n.k.

  Urefu wa muda na mabadiliko yaliyotokea yanatueleza jambo muhimu.
  Kwamba, tulitakiwa kufanyia marejeo hoja kujiridhisha uwepo wa umuhimu au la

  Tulipaswa tuwe na mjadala mpana wa Kitaifa kwa haraka ili kutupa mwanga kama bado tupo katika njia sahihi au tunahitaji marekebisho au mpango mzima hauna tija

  Tuna uhakika suala lisingekuwa na urasimu kwani ni kwa masilahi ya kila mmoja

  Taharuki iliyowakumba watendaji, tunahoji kama ngazi za juu zilishiriki mjadala mfupi?

  Tunauliza kulikuwa na marejeo au tulikwenda na maamuzi ya miaka 30 iliyopita?

  Na je, hakukuwepo haja ya mjadala wa kitaifa au kupitia wawakilishi kufikia uamuzi?

  Tusemezane
   
 3. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #3
  Sep 11, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,168
  Likes Received: 4,726
  Trophy Points: 280
  JE, KULIKUWA NA USHIRIKISHWAJI WA VYOMBO VINGINE

  Tarehe 31 JULY 2016
  Tuliandika kuwa CDA imekuwepo kisheria kwa muda wa uhai wa tangazo la kuhamia Dodoma. Jukumu kubwa lilikuwa kuandaa mji kwa ajili ya kupokea serikali

  CDA ilipata fungu la kazi ya kuendeleza makao makuu.
  Katika kipindi hicho hatuoni ufanisi kwa taharuki iliyotokea baada ya tangazo kutolewa

  Tukauliza, kama CDA haikuweza kufanya maandalizi ni muujiza gani unaooweza kusaidia serikali kuhamia huko mwezi huu ?

  Swali hilo limepata jibu karibuni kwa ofisi ya waziri mkuu kushindwa kuhamia kama ilivyosemwa

  Makazi ya waziri mkuu hayajakamilika, na kwa mujibu wa gazeti moja la Sept 10 2016 waziri mkuu amesema uhamaiaji utakuwa wa awamu tofauti na haraka iliyokuwepo

  Wakati huo huo, taasisi za huduma za jamii kama Hospitali na idara ya maji zimeonyesha wasi wasi kuhusu ujio, kwamba huduma hazitakidhi mahitaji

  Hatuna uhakika maeneo ya huduma za miundo mbinu (sewerage) barabara, masoko, makazi ya wananchi , shule n.k. yapo tayari kwa ugeni tarajiwa

  Hili linatueleza jambo moja, kwamba hakukuwa na ushirikishwaji wa vyombo vingine na hivyo kujikuta katika hali ya ''kufumaniwa' kama lugha ni sahihi au 'off guard' kwa lugha zao

  Kutangaza kuhamia, kisha kubadili ratiba ni dalili kuwa ''mkokoteni umewekwa mbele ya farasi'' (Cart in front of the hose)

  Pengine kungekuwa na mjadala japo kidogo, ushirikishwaji wa taasisi na idara na upangaji wa mipango ya kuhamia ungekuwa katika ratiba inayoeleweka ukiwa na rasilimali

  Hili linaleta hoja nyingine

  SHERIA
  Kwamba kuhamia Dodoma ni sera tu au ni sera yenye sheria? Tunauliza hivi kwasababu wakati wa kuomba rasilimali fedha, suala litatinga bungeni. Fungu linatokaje? Ni swali tu wajuzi watusaidie
   
 4. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #4
  Sep 11, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,168
  Likes Received: 4,726
  Trophy Points: 280
  JE, LILIKUWA NI SUALA LA HARAKA AU LILILOHITAJI MIPANGO?

  Tunaendelea kupitia hoja za bandiko la kwanza

  Kuhamia Dodoma limekuwa suala la haraka, hata hivyo linahitaji mipango ya muda mrefu

  July 31 2016 tulisema, ni bora serikali kutoa muda kwa mashirika/taasis zinayohusiana na shughuli za jamii kutengeneza mazingira ya ' ugeni' kutopata mawaa wakti ukifika

  Serikali ingeliagiza CDA kuhakikisha miundo mbinu inakamilika, makazi na huduma
  Shirika la nyumba lisitishe miradi mingine ili kuongeza nguvu kwa CDA kwa lengo hilo

  Mifuko ya jamii iombwe kushirikiana na mashirika kama CDA na NHC kutengeneza miundo mbinu na hasa suala la makazi na ofisi za umma

  Ujenzi wa reli ya SGR upewe kipaumbele kuunga Dar es Salaama na Dodoma.
  Hii ni kwasababu shughuli nyingi ikiwemo familia zitabaki Dar es Salaam kwa muda

  Wizara zihamie kwa nafasi ili kutoa muda kwa Mji wa Dodoma kuji 'adjust' kwa utaratibu
  Yote yanahitaji muda uliopangwai. Msingi wa hoja ni kuwa na ratiba na taratibu

  UHARAKA

  Uharaka una madhara makubwa kwa serikali na wananchi kwa ujumla wake

  Tulinukuu gazeti lililokuwa na kichwa cha habari ' Urahisi kuhamia Dodoma'
  Gazeti lilitoa takwimu za NBS zikionyesha nyumba katika baadhi ya maeneo ni za udongo

  Gharama ni kati ya 15,000-20,000 za kupnga kwa kuchangia huduma kama vyoo
  Kwingineko kama Area C na Uzunguni ni 300,000+

  Athari za uharaka zipo katika maeneo mengi

  1. Kuongezeka kwa gharama za kuendesha serikali. Dar itabaki kitovu cha biashara, kuna ofisi zitalazimika kuwa na ofisi ndogo ili kukidhi haja za kibiashara, kikazi n.k.

  Kwa mfano, hatutegemei Wanadiplomasia kuhamia Dodoma ambako makazi ya waziri mkuu yamekuwa tatizo na nyumba zinazoelezwa ni hizo za udongo huko Mlimwa

  Usafiri wa anga utabaki Dar es Salaam ukiakisi uwepo wa ofisi za kidilomasia, mashirika ya biashara, ofisi za umma zenye mahusiano na biashara kubwa n.k.

  Serikali haiwezi kujitenga na 'network' hiyo.

  2. Mji wa Dodoma utakabiliwa na ongezeko la ghafla la wakazi.
  Huduma za afya, elimu, miundo mbinu n.k. zitaathirika. Haya yatachangia kuongezeka ghafla kwa gharama za maisha kwa wakazi wa Dodoma bila kutarajia

  3. Wafanyakazi watakaohama wataathirika kisaikolojia.
  Wengi wana makazi ya kudumua Dar ambayo ni sehemu ya maandalizi ya kustaafu.
  Kuwahamisha katika mwendo wa haraka kama ilivyo kuna maanisha mambo mawili

  a) Wachague kwenda na ongezeko la gharama za maisha kwa familia mbili, au kuacha familia wakiwajibika kwa familia hizo wakiwa Dodoma au kuacha kazi

  b) Baadhi wapo hatua za mwisho za utumishi. Mstaafu mtarajiwa miaka 1, 2, 3, 4 ijayo anapoambiwa achague kwenda au kuacha kazi ni 'teso' la kisaikolojia bila sababu

  Haya yanajibu swali, uharaka uliopo umezingatia hali halisi au ni kuhamia kwa haraka?

  Inaendelea
   
 5. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #5
  Sep 11, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,168
  Likes Received: 4,726
  Trophy Points: 280
  JE ,DODOMA IPO TAYARI KWA 'UGENI'

  Ipo dhana hafifu kuwa uwepo wa Bunge Dodoma na mikutano mikubwa ni ishara za utayari wa Dodoma kupokea ujio. Ipo dhana Dodoma ikiunganisha mikoa mingi ipo tayari kimiundo mbinu

  Dhana hizi ni potofu kwa kuzingatia kuwa uwepo wa Wabunge na watumishi ni wa muda tu.

  Wabunge na familia zao wanaishi nje ya Dodoma, kilichopo ni makazi au ofisi za muda

  Hili linathibitika kwa ukweli kuwa makazi ya waziri mkuu hayajakamilika, kwa maana kuwa uwepo wake Dodoma ni kwa nyakati tu na hivyo anahitaji makazi ya kudumu

  Wageni wanaofika Dodoma ni wa muda tu ambao huenda kwa shughuli maalum kwa muda maalum na hivyo hawawezi kueleza utayari wa mji kupokea wakazi wa kudumu.

  Ongezeko la watu linatarajiwa kuwa kubwa zikiwemo familia za watumishi, familia za wafanya biashara na family za watu wengine wanaohusiana na mzunguko wa jamii.

  Kwa muda mfupi Dodoma itakuwa na ongezeko la ghafla la wakazi

  Hii maana yake, mji unatakiwa uwe na miundo mbinu ya kutosheleza ongezeko hilo

  Idara ya maji imeonyesha wasi wasi wa ongezeko na upatikanaji wa maji
  Hospitali ya mkoa nayo imeonyesha wasi wasi katika huduma zikiwem o za kuhifadhi wafu

  Dodoma inahitaji mfumo wa majitaka(sewerage) ambao si kuwa unatakiwa kujengwa katika mabomba bali katika kupokea tofauti na Dar ambako sehemu kubwa huishia baharini

  Miundo mbinu ya barabara , mashule itakuwa na msongamano mkubwa

  Tukiuangalia Mji wa Dodoma, wasi wasi wa upatikanaji maji safi, usafirishaji maji taka na overcrowding katika huduma kama za shule na hospitali hizo ni precursor kwa maradhi ya milipuko

  Kushindwa kwa ofisi ya waziri mkuu kuhamia sept mosi kama ilivyokuwa kunaeleza ukubwa wa tatizo na changamoto zake. Kwa bahati mbaya haionekani kama kuna 'organization' katika hili

  Kusipokuwa na plan nzuri, kushirikisha wadau, kutoa vipaumbele na kupanga kwa pamoja, tutahamia Dodoma kwa kuzua matatizo makubwa mbele ya safari

  Ili kufanikiwa katika uratibu wa shughuli ni lazima yawepo mamlaka ya kushughulikia.
  Kwasasa hilo ni jukumu la CDA, kwa jinsi CDA ilivyofeli kwa miaka mingi hatutarajii mapya.

  Kwa kuanzia ni kuifumua CDA, kuweka watu wenye uwezo na maono ya kukabiliana changamoto
   
 6. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #6
  Sep 15, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,168
  Likes Received: 4,726
  Trophy Points: 280
  SAFARI YA DODOMA NA 'TETEMEKO'

  Dodoma ni eneo linalojulikana kuwa katika ukanda wa bonde la ufa

  Kumekuwa na matukio ya tetemeko la ardhi mara kwa mara

  Tunakumbuka tetemeko la kuahirisha bunge wakati wa Spika Msekwa

  Hatujui ni lini au wakati gani, tunachojua eneo hilo lipo 'prone' kwa tetemeko

  Ongezeko la watu halina uhusiano na tetemeko la ardhi

  Hata hivyo,madhara ya tetemeko kwenye wengi ni tofauti na kwenye wachache

  Je, miundo mbinu ya Dodoma imetengenzwa kukabiliana na hali kama hiyo?

  Je, majengo yaliyopo na yajayo yapo katika hali ya tahadhari?

  Tetemeko lililoikumba Kagera limetufundisha mengi

  Kwanza, utayari kwa majanga ya asili ni mdogo sana kama upo

  Pili, uwezo wetu unatia shaka

  Juzi waziri mkuu alikutana na wafanyabaiashara na mabalozi kuchangia maafa

  Kiasi kilichokusanywa na ahadi ni chini ya Bilioni 5 kwa taarifa za awali

  Je, ipo haja ya michango ikishirikisha nchi, mashirika na wafanyabiashara?

  Ikiwa ofisi ya bunge ilirudisha bilioni 6 serikali, tume ya uchaguzi bilion takribani 12, kulikuwa na sababu zipi za kutafuta michango kutoka kwingineko?

  Hii ni kuonyesha tu kuwa tuna rasilimali zilizokolewa za kutosha ikiwemo watumishi hewa n.k. Kwanini hatukuwa tayari kabla na wakati wa tukio?

  Hatumaanishi michango haikuwa mizuri, la hasa, hilo ni jukumu letu wananchi

  Lakini madhara yanayohitaji uharaka yakisubiri michango ya wafanyabishara na mabalozi inatia shaka na kwa kiasi kinachosemwa kilichangwa inafikirisha

  Hapa ndipo tujiulize tena, je, safari ya Dodoma ityakayohitaji rasilimali zaidi itakuwa katika hali tarajiwa au itakuwa bora twende?

  Je, mji upo tayari ku handle majanga kama ya Kagera kwa kuangalia jiografia?

  Tusemezane
   
 7. Nguruvi3

  Nguruvi3 Platinum Member

  #7
  Sep 17, 2016
  Joined: Jun 21, 2010
  Messages: 11,168
  Likes Received: 4,726
  Trophy Points: 280
  KAULI YA WAZIRI MKUU

  TANGAZO LILIVYOPOKELEWA NDIVYO SIVYO

  Waziri mkuu(PM) ameeleza mpango wa serikali kuhamia Dodoma

  Kwanza, ameeleza jambo moja muhimu 'kwamba miundo mbinu iliyopo Dodoma inatosheleza mahitaji ya serikali kwa kuhamia kwa awamu''

  Kwa lugha hiyo PM anasema, haiwezekani kuhamia Dodoma kwa mkupuo.
  Hili tumelijadili katika hapa tukisisitiza kuwa si suala la kuhamia tu bali utaratibu na miundo mbinu

  PM akasema kuna master plan inayopitiwa ili kuifanya Dodoma ikidhi vigezo vya kimataifa

  Kwa maneno hayo, master plan haikuwa imepitiwa kwanza kabla ya kutangaza kuhamia

  Akasema zimeundwa kamati za kitaifa kama ile ya makatibu wakuu, na kwa kushirikiana na CDA na ofisi za mkoa kuratibu shughuli nzima

  Kwa maneno mengine, kamati hazikuwepo kwanza, tangazo lilipotoka

  PM- shughuli ya kuhamia itashirikisha sekta binafsi na jamii.
  Hii ni pamoja na kuhakikisha Dodoma inakuwa na miundo mbinu kama bandari kavu, mahoteli mazuri na makazi ya kuishi

  Hapa PM ameliona tatizo la makazi tuliloongea siku za nyuma.
  Kwamba Dodoma haikuwa tayari kupokea wageni kwa miundo mbinu yake, na hilo lingeumiza sana wafanyakazi . Lingeongeza gharama za maisha kutokana na demand and supply n.k.

  Kilichoshangaza ni ujenzi wa bandari kavu. Tunadhani haikuwa sahihi kusema 'ujenzi' wa bandari kavu. Dodoma ni mji wa serikali na si biashara, kwanini kuwepo na bandari kavu?

  Hapa kunaonyesha kuwa wataalam bado wanatakiwa kushauri ili kuepuka maamuzi ya wanasiasa

  HARAKA YA NINI?
  Baada ya tangazo la Rais tuliona viongozi wakihaha na mikakati ya kuhamia Dodoma.
  Ilikuwa vurugu , vikao , matamako n.k. bila chembe ya tathmini kutoka kwa viongozi

  Zoezi la kwanza kushindwa ni ofisi ya PM kuhamia sept 1. Hili ndilo limeamsha viongozi 'wape up call' kuwa tatizo lipo mbeleni

  Hakuna aliyejiuliza kama kweli tupo tayari, sababu zile za 1973 zipo na kama tuna rasilimali

  HARAKA ZA TAASISI BILA TATHMINI. NI KATIKA KU 'IMPRESS'?

  Mfano mzuri ni tume ya uchaguzi. Hii ilitangaza kutafuta eneo la kiwanja na kuanza ujenzi wa ofisi

  Tume ya uchaguzi ni ofisi ndogo tu ambayo shughuli nyingi huratibiwa wilayani na mikoani

  Inaweza kukodi jingo zuri na kuendesha shughuli zake

  Muda utakavyosonga mbele ndipo inaweza kujenga makao yake ya kudumu

  Huu ni mfano tu wa viongozi waliopokea tamko kwa kulitafisiri vibaya na bila kulifanyia tathimini

  Kazi ya tume si kujenga majumba, inaweza kukodi ofisi kutoka taasisi za umma kama NHC, Mifuko ya umma n.k. ambazo zitajenga majengo kadri muda unavyosonga mbele

  Haraka ya kutafuta viwanja kukiwa hakuna ratiba ilikuwa ya nini? Kwani ni lazima wajenge ofisi?

  Wizara nyingi zinatumia majengo ya mashirika, je, NEC walifanya tathmini kati ya umiliki na kukodi majengo kipi ni bora? Ilifanyika tathmini?

  Inaendelea
   
Loading...