WANANCHI MITAANI
WANAYAONA HAWASEMI
Kuna dhana wananchi wa mitaani hawajali na hawaoni yanayoendelea
Ipo dhana wananchi wanaamini kila wanachoelezwa na serikali
Na ipo fikra kuwa ukiwaficha wananchi, umetatua tatizo
Yote si kweli, na hujirudia kwa watu kutojifunza, au kiburi au dharau ya juu
Kiburi, dharau na kutojali ni matokeo ya kuwa na nguvu wasizonazo wananchi.
Kwamba, kikundi cha watu kimedhibiti nchi kiasi cha kufanya watakavyo
Wanatumia maguvu kuminya sauti za wananchi kwa kila hali na mahali.
CCM inafahamu madhara ya hayo. Uchaguzi mkuu makada waliona aibu kunasabishwa na chama. Kilichotokea baada ya hapo ni maguvu tu.
Wananchi walikuwa sababu hizi dhidi ya CCM
1. Dukuduku (reservations) kutokana na yaliyotendwa na CCM kwa miaka mingi
2. Kinyongo (sentiments) wananchi wamebeba hasira mioyoni kwa muda mrefu
3. Chuki (grudge) inakuwepo mioyoni kila siku
Kinyongo na chuki yalitokana na mambo kufanywa kwa utashi wa watu na si umma.
Kuufanya umma wajinga, kuudharau na hata kuudhalilisha.
Kashfa zilifichwa kwa udanganyifu na mbinu chafu, kutumia vyombo vya umma n.k.
Ilifika mahali wananchi wakisema ni afadhali kuchagua shetani kuliko CCM
Hili lilionyesha kiwango cha juu cha dukuduku,chuki na kinyongo kwa CCM/Serikali zake
Hatari kubwa si katika chuki,ni pale chuki, kinyongo na dukuduku vitakapokuwa sababu.
Hili linaweza kuvuruga hali ya uvumilivu waliyo nayo wananchi
Zipo nchi bei ya mkate tu ilileta matatizo makubwa na kuangusha serikali za nchi hizo
Chanzo si bei za mkate bali chuki na dukuduku la muda mrefu liliosubiri sababu
Kwa yanayoendelea, ikitokea sababu tena ya kijinga inaweza kutuletea matatizo.
Wakati wananchi wana maisha magumu, wanafanya kazi na wanalipa kodi
Wapo wanaoiba mabilioni na kulindwa na wale wale wanaokusanya kodi, inafikirisha.
Picha inayojitokeza, ni wananchi kutumika kisiasa 'political expedient'.
Wanaaminishwa ipo nia/dhamira ya kutatua matatizo, kukabiliana na uovu n.k.
Wanaona mambo yale yale waliyozoea yakitendwa kwa mtindo ule ule
Wananchi hawana matumaini, wanakumbatia chuki, kinyongo na dukuduku.
Wanasubiri ili wahalalishe reservations zao.
Ya Bungeni kwa ujumla wake ni ushindi mtamu wa muda mfupi na tatizo chungu muda mrefu. CCM/Serikali wasijidanganye, wananchi wana weledi na ufahamu
Wanaona,wanajua kila mbinu za kulindana.Wana chuki, dukduku na kinyongo
Tusemezane