Asante Mkuu
Nguruvi3 kwa kuendeleza uzi huu...
Kujiuzulu kwa Papa ni kitu ambacho hakijazoeleka kabisa hasa ukizingatia kuwa mara ya mwisho hilo kutokea ilikuwa miaka 600 iliyopita hivyo ni kitu kigeni mno...Lakini kwa kuwa utaratibu wa kujiuzulu upo na unakubalika kwa mujibu wa kanuni za Vatican, na kwa kuwa ametoa sababu za kiafya ambazo hazipingiki kutokana na umri wake mkubwa then suala hili mwishowe litakuja kukubalika na wengi na hatimaye kuzoeleka hata kwa viongozi watakaofuatia.
Kuhusu vurugu zinazoendelea hapa nyumbani niseme tu kwamba Serikali inaposhindwa kusimama katika nafasi yake. Inaposhindwa kusimamia sheria na taratibu kwa ukamilifu na ujasiri bila kujali nani anavunja sheria na anatoka wapi na anasali wapi ndiyo inatufikisha hapa. Mungu atusaidie kwa kweli!
Ni kweli kuwa hakuna papa katika kipindi cha karne 6 aliyewahi kufanya hivyo.
Hata hivyo Benedict alifanya kazi na John Paul ambaye siku za mwisho za uhai wake kanisa liliongozwa na ''inner circle'' ya Vatican akiwemo Benedict. Nadhani kwa kuona hilo yeye ameamua ku-set a platform kwa wajao ili isifike mahali Papa anakuwa hana uwezo lakini bado anaongoza kwa kutumia jina.
Kuna hili la kashfa za ngono ambalo limeitafuna sana kanisa.
Siku chache zilizopita kadinali mmoja ametuhumiwa katika kashfa kama hiyo na leo conclave ikikaa yeye hayumo.
Uzito wa madai hayo umeifanya kazi ya papa kuwa ngumu sana kwani kila mahali alipozuru ilibidi atangulize samahani kwa makosa ya watu walio chini yake tena kwa kashfa za ngono.
Dunia inabadilika sana, hili suala la yeye kuhojiwa kwa kujua uchafu na kuufunika chini ya kapeti nalo halipaswi kupewa kisogo. Kashfa nyingi zilijulikana lakini katika kulinda hadhi ya Vatican zilifichwa.
Zimeandikwa sana na jinsi mawasiliano yalivyokuwa yanafanyika na makao makuu.
Wakati huo Ratsinger alikuwa mshauri mkuu ndani ya st Peter.
Pengine hofu ya kuitwa kuhojiwa nayo yaweza kuwa ni sababu.
Swali linalosumbua akili yangu ni kuwa kwanini hawa watawa, walei, mapadri na maaskofu wanaingia katika kashfa za ulawiti na si ngono kama ya mume na mke?
Tunafahamu wao ni binadam na ni dhaifu tu kimaumbile, lakini basi ingetokea wao kuwa na mahusiano, mathalani mapadri na watawa, au viongozi na wanawawke pengine lingeleeweka japo kwa taabu.
Kiichoeleweka na hasa upande wangu ni wao kuwalawiti vijana wadogo. Kwanini kuwalawiti na si kufanya ngono na wanawake? Sijui kama nitaeleweka lakini ndivyo ninavyojiuliza.
Kwanini weakness yao iwe katika vitoto vidogo vya kiume na si watawa, wanawake, machangudoa?
Ikumbukwe kuwa sasa hivi kanisa katoliki duniani linaongozwa na college of Cardinals ambao wapo Vatican katika kikao cha Conclave kitakachomchagua papa ajaye. Hili litatokea kabla ya pasaka.
TANZANIA
Kuhusu yanayotokea hapa nyumbani, nakubaliana nawe kuwa serikali imechangia sana katika kuzorota kwa hali.
Haiwezekani mtu auze DVD za kuhamasisha mauaji aachwe tu aendelee kusambaza sumu hiyo.
Tumeona kule Zanzibar Watu wakichomwa moto na vibanda vyao kwa kisingizio cha muungano.
Hiki tulionya kuwa ni kisingizio tu kwani wakati wanafanya hivyo lengo lilikuwa Mtanganyika kwa jina na mkristo kwa lengo.Wote waliofanya ujinga ule waliachiwa huru.
Likaja la kunusurika Padri kuuawa, hadi leo hakuna aliyefikishwa mbele ya sheria bali ni zuga za uchunguzi.
Limefika la Padre kuuawa sasa.
Nasema huu ni ugaidi kwasababu lengo ni kuwatisha waumini wa dini nyingine au kuweka shinikizo ili serikali ikubaliane na madai ya kuwaachia huru masheikh walioko magereza.
Serikali ingefuatilia kwa umakini tahadhari za watu na makundi mbAli mbali tusingefika hapa tulipo.
Kuna msomaji wa safu hii kaniuliza kuna tofauti gani ya yale ya Mwanza, Geita na Zanzibar? Kama ni ugaidi kwanini isiwe kote iwe Zanzibar.
Jibu langu ni kuwa wote ni uovu tu lakini uovu unatofautiana.
Kule Mwanza na Geita kunajulikana ni suala la kuchinja nyama. Kwamba tatizo linafahamika na limekuzwa kijinga na watu wasio na uelewa au pengine tu kwa kuchochewa.Pande zote zimekosa busara na kupelekea yaliyotokea.
Zanzibar ni Ugaidi kwa sababu tafsiri ya ugaiDi ni tisho (terror) na tendo ni kutishia (terrorism) na afanyaye ni gaidi(terrorist). Gaidi siku zote hujificha na hata sababu zake huzificha. Anachotaka ni kufikia lengo lake la kutishia.
Zanzibar wanaua ili kuwatisha Watanganyika na hasa Wakristo ima kuhama Zanzibar au kuacha kazi zao.
Kwa uelewa mdogo hili ni jambo la hatari sana kwa mustakabali wa Zanzibar.
Sifa ya Zanzibar mbali na nyingine nzuri nyingi ni kuwa Kiota cha kuzalishia watu wenye misimamo mikali kisiasa.
Sifa hii imeondoa sifa ya Zanzibar kuwa sehemu ya ustaraabu wa kale katika pwani ya Afrika mashariki.
Hivi sasa Zan inaangaliwa kwa jicho kali na mataifa mengine hasa ya maghAribi.
Mataifa hayo yangependa kuona Zanzibar inadhibitiwa ili isije ikawa Somalia au Mali nyingine.
Kwa haya yanayotokea ndio kwanza yanashadidia hoja ya mataifa haya.
Kuna mambo mengi yatatokea. Kwanza ni kuzuia sekta ya utalii kukua kwa kuonya watalii kutozuru Zanz.
Uchumi wa Zanz unatEgemea sana utalii. Hapo kutakuwa na hali ngumu sana na huenda wawekezaji wakakimbia kama si kuishi kwa machale.
Pili, Tanzania itashinikizwa kuhakikisha kuwa muungano hauvunjiki ili kuweza kudhibiti Zanzibar kwa ukaribu.
Wakati mchakato wA katiba ukiendelea tuataona nguvu ya kuzuia hilo ikijitokeza.
Kwa kuanzia tu vitambulisho vya taifa la Tanzania vimetolewa. Hii maana yake ni kuwa iwe iwavyo muungano utakuwepo
Miongoni mwa waliochukua ni Maalim Seif. Hii ilifanywa makusudi ili kuonyesha kuwa hata Seif anaunga mkono muungano.
Maana yake ni nini? Ni kuwa zile ndoto za Zanzibar huru haZitatimia kwasababu uwepo mkataba au serikali 3 , 4 au 5 bado kuna mambo ambayo Zanz itabaki katika udhibiti.
Hii haitokani na Tanganyika bali shinikizo la mataifa makubwa kuhakikisha kuwa kisiwa hiki kinapewa ukaribu katika uangalizi.
Lingine linaloweza kutokea ni kuwaunga mkono wajitenge kabisa katika mambo yao.
Mataifa ya magharibi yatafanya hivyo ili kuweza kutoa msaada na huenda kuifanya Zanzibar ijione kuwa bora zaidi kuliko ndani ya muungao.
Hata hivyo misaada hiyo itakuwa na masharti na si aghalabu tutasikia Zan huru ikishinikizwa kukubali matakwa kama kuheshimu haki za binadamu katika imani na pengine kukubali mambo kama ya ndoa za jinsia moja, ushoga n.k.
Yote hayo yatafanywa ili kuhakikisha kuwa nchi hizo zina uakribu sana na Zanz ili kujua na kudhibiti hali itakayojitokeza.
Hivyo mauaji ya kigaidi kama yanayoendelea hayaisaidii Zanz hata kidogo.
Yanazidi kuiweka katika ramani ya dunia kwa alama mbaya sana.
Twende mbele na nyuma lakini lawama zinabaki kwa serikali. Serikali zilizopita ziliweza kudhibiti hali kabla ya uharibifu,
Kutoa uhuru wa kuabudu bila bughudha, kuweka mipaka ya dini na siasa na hata kuwashughulikia wakorofi mapema.
Udhaifu wa kiongozi wa serikali ya leo ndio umetufikisha hapa. Hata baada ya maonyo ya kila aina serikali hiyo haikuchukua hatua na sasa inapigana kujenga ukuta na si kuziba ufa.
Hili liwe fundisho kwa Watanzania, wakikaa na kujua kuwa kiongozi wa nchi si mcheza mpira au mpiga zumari.
Ni mtu muhimu sana katika mustakabali wa taifa na upatikanaji wake ni lazima uzingatie, uwezo, uadilifu na maono ya kiongozi na siyo ucheshi,tabasamu au undumila kuwili.
Tusemezane