Sehemu ya II
'VITA' MASHARIKI YA KATI
HAMAS WASHAMBULIA ISRAEL, NA ISRAEL YASEMA ITAJIBU MAPIGO
Inaendelea..
Shambuli la HAMAS lilipangwa kwa muda mrefu na kwa utalaam kwa maana kwamba walishambulia kutoka angani, majini na ardhini wakitumia makombora , drone na utekaji wa askari wa Israel.
Ni kundi la makomandoo waliofanya utafiti wa kutosha hata kuishtukiza idara ya usalama ya Israel MOSAD na CIA.
Swali linaloumiza wadadisi wa habari ni, kwanini, shambulio lililohusisha watu wengi namna hiyo halikuweza kuvuja?
Katika kuonyesha umahiri, HAMAS wamerusha makombora zaidi ya 5000. Wengi wanajiuliza ni kwanini.
Jibu ni kwamba Israel ina makombora ya 'Iron dome' yanayozuia makombora ya Wapalestina.
HAMAS walirusha makombora mengi ili ku 'overpower iron domes' na hilo limefanikiwa sana
Pili, makombora ya HAMAS kwa mara ya kwanza yamefika Tel Aviv, ikiashiria utaalam zaidi wa kuyatengeneza kutoka nje ya GAZA. Tayari vidole vinanyooshwa kuelekea Tehran, Iran kama mshirika mkuu wa HAMAS
Katika uzi huu mabandiko #39,40,41 tumeeleza kifo cha Kamanda wa kijeshi wa Iran Bw. Qasem Suleiman kilichofanywa na Marekani kule Iraq.
Tulieleza kwamba aliyefanya shambulio ni Marekani kwa niaba ya Israel, ili kutotibua nchi za Kiarabu
Iran ilijibu pigo kwa kushambulia ngome ya Marekani IRAQ na kuumiza askari wengi, ikiapa kulipiza kisasa mbeleni
Mwaka 2020 Israel alimuua mwanasayansi wa IRAN aliyekuwa kiongozi wa mpango wa kutengeneza Nuklia Bw Mohsen Fakhrizadeh , mauaji yaliyowauma sana Iran.
Baada ya shambulio la jana, Bunge la Iran lilipitisha kauli ya kuunga mkono shambulizi la HAMAS.
Pamoja na Iran, kuna maandamano sehemu mbali mbali za Dunia katika kuunga mkono shambuli la HAMAS
Kwa mantiki, Iran imeweza kulipa kisasi ingawa GAZA italipa gharama kwa mashambulio ya Israel.
Sahambulio la HAMAS linakumbusha jinsi Israel ilivyoshindwa vita dhidi ya HEZBOLLAH ya Imam Nasrallah.
Vikosi vya Marekani vimeelekea Israel na Rais wa Marekani akisema wataisaidia Israel kwa kila msaada wanaoutaka
Hii maana yake ni kwamba Israel kwa ushirika na Marekani inapigana vita na kundi la HAMAS.
Hali ya usaidizi kutoka Marekani inaeleza udhaifu wa Israel kama yenyewe ni dhaifu kusimama yenyewe.
Ugomvi uliopo kati ya ISRAEL na HAMAS unaweza kusambaa mashariki ya kati kama hautatafutiwa ufumbuzi
HAMASA wamefanikiwa sana katika kupanga mkakati wa kuiunganisha Mashariki ya kati kwa kutumia dini.
HAMAS wanatumia makosa ya Israel ya kuuvamia Msikiti Maarufu wa Al-Aqssa pale Jerusalem, moja ya shemu muhimu sana katika Ibada ya Waislam wakihusisha Msikiti na Ziara ya Mtume Muhammad S.A.W kwenda Mbinguni.
Katika mashambulizi, HAMAS wanatumia kikosi cha kijeshi kinachoitwa Al-Qasam kwa maana wapiganaji waKiislam wakichukua jina kutoka kwa mwanazuon Izza -Din na kuyafanya mapambano yao ni dhidi ya eneo la Waislam
Pili, HAMAS wanasema shambulio lao ni kulinda Msikiti wa Al-Aqsa ulioingiliwa na Israel. Haya yamewaunganisha Waislam mashariki ya kati dhidi ya Israel
Tumeona maandamano Tehran, Istambul, Kuwait, Sanaa Yemen na yatapamba zaidi hadi kufikia Jumatatu.
Hata Mahasimu wa HAMAS kule WEST BANK nao wameandamana kuwaunga mkono HAMAS
Mzozo huu unaziweka nchi zifuatazo katika wakati mgumu; Marekani, Israel, na Saudi Arabia. Tutajadili sehemu ya III
Tutafafanua
Charles kilian