Duniani kuna watu sahihi na watu wazuri

Duniani kuna watu sahihi na watu wazuri

JacobMushi

Member
Joined
Sep 18, 2018
Posts
22
Reaction score
30
#usiishienjiani leo: Watu Sahihi, Watu Wazuri.

Kwenye Maisha tunawahitaji watu sahihi. Watu Sahihi sio lazima wawe Wazuri kwetu wanaweza kuwa watu wabaya lakini ni sahihi. Kusudi la hao watu kwenye maisha yetu ndio litaamua usahihi wao.

Unaweza kukutana na mtu anakuchukia bila sababu halafu kwa kukuchukia kwake kukawa sababu ya wewe kusonga mbele Zaidi.
Kuna watu wakikupenda ndio wanakuharibu, badala ya kukusaidia wanakuwa wanakuharibu.

Mfano mtu wa karibu kwako ataumia akiona unateseka kumbe yale mateso yapo kwa kusudi. Yeye anaweza kukuhurumia akakusaidia kukuondoa kwenye mateso kumbe ndio amekuondoa kwenye kufikia mafanikio yako.

Mfano umepanga chumba ukafukuzwa kazi na hela ya kodi ikawa tatizo. Akili yako ikiwa katika kupambana ili upate hela akatokea ndugu yako akakwambia njoo kwangu ukae kwa muda hadi hali itakapokuwa nzuri. Kumbe wakati ule unawaza nini cha kufanya ndio ungepata suluhisho la kudumu la Maisha. Yeye kuja kukupa msaada kidogo ikawa sababu usifikiri tena.

Kuna watu Wazuri kwenye maisha yetu wanaweza kuwa sababu ya sisi kutokujitatulia Matatizo yetu wenyewe. Badala ya kufikiria suluhisho bora na la kudumu unamfikiria mtu ambaye anaweza kukukopesha hela maisha yasogeesogee kidogo.

Ndio maana ukiona watu hawakupi msaada ujue kuna kitu unatakiwa kujifunza. Nacho ni kujifunza Kusimama Mwenyewe.

Watu sahihi wanaweza kuwa watu wabaya kwetu ili kutufundisha vitu mbalimbali. Usimkimbie mtu ambaye hakuoneshi upendo wakati huo huo kuna mengi ya kujifunza kwake. Sio kila bosi atakuwa bosi mzuri.

Muhimu ni kuwa watu hawa makusudi yao kwetu yawe ni kutufanya tuwe bora Zaidi na sio kuanguka.

Unawahitaji watu sahihi na sio watu Wazuri kwako. Sio watu ambao watakuhurumia kila wakati.

Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana.
Rafiki Yako Jacob Mushi
 
Kweli kabisa mkuu mm 2015 nilipata matatizo mfululizo kila ninaye muomba pesa alikuwa anasema hana ata Yule unayeamini anayo anasema hana nilitaabika lakini nilifanikisha kuvuka kile kipindi na nilijifunza kujiwekea akiba ata kwa kidogo nikipatacho kuanzia siku iyoo naamini wakutatua shida zangu ni mm mwenyewe

Sent using Jamii Forums mobile app
 
#usiishienjiani leo: Watu Sahihi, Watu Wazuri.

Kwenye Maisha tunawahitaji watu sahihi. Watu Sahihi sio lazima wawe Wazuri kwetu wanaweza kuwa watu wabaya lakini ni sahihi. Kusudi la hao watu kwenye maisha yetu ndio litaamua usahihi wao.

Unaweza kukutana na mtu anakuchukia bila sababu halafu kwa kukuchukia kwake kukawa sababu ya wewe kusonga mbele Zaidi.
Kuna watu wakikupenda ndio wanakuharibu, badala ya kukusaidia wanakuwa wanakuharibu.

Mfano mtu wa karibu kwako ataumia akiona unateseka kumbe yale mateso yapo kwa kusudi. Yeye anaweza kukuhurumia akakusaidia kukuondoa kwenye mateso kumbe ndio amekuondoa kwenye kufikia mafanikio yako.

Mfano umepanga chumba ukafukuzwa kazi na hela ya kodi ikawa tatizo. Akili yako ikiwa katika kupambana ili upate hela akatokea ndugu yako akakwambia njoo kwangu ukae kwa muda hadi hali itakapokuwa nzuri. Kumbe wakati ule unawaza nini cha kufanya ndio ungepata suluhisho la kudumu la Maisha. Yeye kuja kukupa msaada kidogo ikawa sababu usifikiri tena.

Kuna watu Wazuri kwenye maisha yetu wanaweza kuwa sababu ya sisi kutokujitatulia Matatizo yetu wenyewe. Badala ya kufikiria suluhisho bora na la kudumu unamfikiria mtu ambaye anaweza kukukopesha hela maisha yasogeesogee kidogo.

Ndio maana ukiona watu hawakupi msaada ujue kuna kitu unatakiwa kujifunza. Nacho ni kujifunza Kusimama Mwenyewe.

Watu sahihi wanaweza kuwa watu wabaya kwetu ili kutufundisha vitu mbalimbali. Usimkimbie mtu ambaye hakuoneshi upendo wakati huo huo kuna mengi ya kujifunza kwake. Sio kila bosi atakuwa bosi mzuri.

Muhimu ni kuwa watu hawa makusudi yao kwetu yawe ni kutufanya tuwe bora Zaidi na sio kuanguka.

Unawahitaji watu sahihi na sio watu Wazuri kwako. Sio watu ambao watakuhurumia kila wakati.

Nakutakia Kila la Kheri.
Ubarikiwe sana.
Rafiki Yako Jacob Mushi
Watu sahihi na Wazuri wanahitajika wote katika maisha na ndiyomaana Mungu aliwaumba wote.

"Time is a wealthy when it's timed consecutively"

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fact ...safi sana "

Binafsi naamini mtu yeyote yule mwenye great ambition katika maisha yake anahitaji kuzungukwa na watu wenye mitazamo hasi dhidi yake ....

Watu ambao watakuwa wana mbeza .. watu ambao watakuwa wana mdharau na kumuona si kitu " ... kwanini basi anapaswa kuwa hitaji watu wenye mitazamo ya namna hii katika maisha yake " ....
Sababu ni moja tu " maneno yote hasi ambayo muhusika atakuwa anaambiwa yana paswa kugeuka kuwa hamasa ya kumfanya muhusika aongeze juhudi " maarifa. Shauku na Vitendo vya kupambana ili aweze kufikia malengo yake .na hatimae akifanikiwa aweze kuwa prove wrong wale wote waliokuwa wana mbeza

Hivyo basi mtoa mada upo sahihi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fact ...safi sana "

Binafsi naamini mtu yeyote yule mwenye great ambition katika maisha yake anahitaji kuzungukwa na watu wenye mitazamo hasi dhidi yake ....

Watu ambao watakuwa wana mbeza .. watu ambao watakuwa wana mdharau na kumuona si kitu " ... kwanini basi anapaswa kuwa hitaji watu wenye mitazamo ya namna hii katika maisha yake " ....
Sababu ni moja tu " maneno yote hasi ambayo muhusika atakuwa anaambiwa yana paswa kugeuka kuwa hamasa ya kumfanya muhusika aongeze juhudi " maarifa. Shauku na Vitendo vya kupambana ili aweze kufikia malengo yake ....

Hivyo basi mtoa mada upo sahihi kabisa

Sent using Jamii Forums mobile app
Karibu sana Rafiki Yangu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom