Dunia tambala bovu

Tetengo

Member
Joined
Jan 21, 2023
Posts
50
Reaction score
23
Ama kweli dunia tambala bovu na maisha hayana formula.

Namshukuru Mungu kwa maana hata ktk miiba huwa kuna maua.Matumaini yapo hata ktk shida,hata ktk changamoto lipo jamb zur utakalowez kujfunz ama kupata.Jifunze kumtazama na kumwona Yesu katikati ya changamoto.

Maisha hay ni kuw makin kwan uzur wa mkakas ndan kipande cha mti.Si salam sana kutumia kiatu cha baniani mbaya kumtibu ila cha msingi usiache mbachao kwa msala upitao.

Cku zote heri kenda shika kulko kumi nenda uje na kuna wakati utapulza kuwasha ama kuzima.Japo dau La mnyonge haliend Joshi,zingatia fimbo ya mnyonge ni umoja.Usije hat cku moj ukamchanganya Lila na fira kwani hazitangamani.

Hakikisha kabla hujaruka uagane na nyonga na hauwez fika mahala bila ya kamba ndefu isiyofunga kuni.Kamwe usitaman miwan ya baa.Kuwa makin na anayekumulika mchana maana atakuchoma ucku.

Yote kwa yote mcheza kwao hutunzwa,jikabidhi kikamilifu kwa Mungu wako,mtumaini na kumtanguliza yeye tu kwa kila jambo kwani cku zote ckio haliwezi kurefuka na kuzidi kichwa labda cyo mwanadamu.


131-Baba Anilinda
I Trust In God

Namtegemea Mungu niwapo
Humo barani na baharini,
Yeye wa mbinguni anilinda.
Baba wa mbinguni anilinda.

CHORUS
Namwamini, Mungu anitunza (anitunza)
Milimani (milimani) au baharini (baharini), baharini
Moyo wangu (moyo wangu) aulinda (aulinda),
Baba wa mbinguni anilinda.

La Waridi alinawirisha,
Na huyo tai juu angani,
Nami kweli anilinda,
Baba wa mbinguni anilinda.

Tunduni mwa simba namwamini,
Kwenye vita ama gerezani,
Motoni na furikoni,
Baba wa mbinguni anilinda.

Bondeni mwa giza na upweke,
Mchunga wangu yuanilinda,
Kwa upole aniongoza.
Baba wa mbinguni anilinda.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…