Dunia sio Salama

Dunia sio Salama

Yote yanawezekana hakuna kumuamini mmarekani kila taifa linajitegemea lakini pia tunasaidiana kama binadamu. Inawezekana imeanguka kwenye milima ya Uzbekistan au baharini nobody knows kwani ndege nyingi zimepotea bila kujulikana kama ya air India iliyoanguka France ilipatikana baada ya miaka 50. Lakini kwa hali iliyopo sasa na ubabe wa mmarekani anything can happen

Nilisikia kwenye radio jana kwamba miaka ya 70 kuna ndege ndogo ilipotea ikitokea DSM kwenda Zanzibar or vice verse. Mabaki ya ndege hiyo yalipatikana chini ya mlima Kilimanjaro baada ya wiki mbili. Inawezekana wanakoitafuta siko ilikoangukia na rubani mmoja inasadikika alichakachua mawasiliano ya radar.
 
Then heading ya hii habari????

sisi kama binadamu tunafikiri nadhani hata wewe umekiri kuwa binadamu wana akili, lakini linapotokea tatizo kama hili lazima tutumie akili zetu kufikiri, hatuwezi kukaa kimya eti kwa sababu ndege ya Malaysia imepotea.

Kuna changamoto nyingi ambazo zinafanya dunia isiwe salama, mfano magonjwa, terrorism, Vita, Kugombania rasilimali nk.
Nadhani kuzungumza changamoto ni nzuri zaidi kuliko kukaa kimya, au kwa vile Malaysia haituhusu? Au tutabaki tunafikiria tu bila kutoa majibu ya suluhisho....Lets us discuss and see if its relevant to our context especially technologically.
 
Kuna ambao mnakumbuka kimwondo kilichoanguka huko mbeya miaka ya nyuma?
Kwa mfano kimwondo cha jinsi hiyo halafu kiwe kikubwa then kikaigonga ndege na kuizika chini ya bahari ni lini mabaki ya ndege yataonekana?
 
Attachments

  • asteroid-hurtling-towards-earth-640x353.jpg
    asteroid-hurtling-towards-earth-640x353.jpg
    20.3 KB · Views: 149
Wakubwa wamepoteza ndege na abiria zaidi ya 200....wengine tukipoteza simu tunaonekana wazeeeembe.
 
Ni kweli hapo nyuma zimewahi kupotea ndege na hazikuonekana kabisa, au zilikuja kuonekana baada ya muda kupita.

lakini hii ndege ya malaysia ukilinganisha na hizo za zamani kuna tofauti kidogo.

1] dunia ya sasa na huko nyuma ni tofauti kwa maana ya maendeleo ya tekinolojia. maarifa ya dunia ya sasa na hapo nyuma ni tofauti,

2] umuhimu uliyopewa hii ndege wa kuitafuta ni mkubwa sana, na habari zimetangazwa karibu ya dunia nzima.

4] eneo wanalotafuta wanakadiria mafuta yaliyokuwa kwenye ndege na muda wa saa 8 ambao ilionekana angani kabla ya kupotea kwenye rada za kijeshi

5] inatafutwa na nchi zaidi ya 25 pamoja na meli, ndege, viona mbali,

kwa hiyo umakini mkubwa unaotumika kuitafuta hii ndege leo ni siku ya 11 na ukiongezea hawa vijana walioingia kwenye hiyo ndege wakitumia pasipoti za wizi , tena wakitokea kwenye taifa ambalo lina mashaka makubwa, na ambalo hapo nyuma lilishakaririwa likisema linataka kuiondoa israel kwenye uso wa dunia, kusema kweli ni lazima mataifa na hata dunia likiwepo taifa letu tuwe macho sana.

kwa sasa hatuwezi kujua hii ndege iko wapi, ni imetekwa? hakuna anayejua, imeanguka baharini hatujui, imepaa imeishia mawinguni hatuelewi. kwa hiyo chochote kinaweza kutokea sehemu yeyote ambayo hatujui. kwa sababu ndege inaruka juu na inaenda kwa kasi kubwa
 
Hii ni kalii kwelii hivi mkuu wa dunia Obama ameliongeleajee hiliii??
 
Waulize wa IRAN wanaitakia nini Ndege ya watu. Hakika Dunia si salama ukiwa unaishi na watu wenye akili za kiirani.
 
Ni kweli hapo nyuma zimewahi kupotea ndege na hazikuonekana kabisa, au zilikuja kuonekana baada ya muda kupita.

lakini hii ndege ya malaysia ukilinganisha na hizo za zamani kuna tofauti kidogo.

1] dunia ya sasa na huko nyuma ni tofauti kwa maana ya maendeleo ya tekinolojia. maarifa ya dunia ya sasa na hapo nyuma ni tofauti,

2] umuhimu uliyopewa hii ndege wa kuitafuta ni mkubwa sana, na habari zimetangazwa karibu ya dunia nzima.

4] eneo wanalotafuta wanakadiria mafuta yaliyokuwa kwenye ndege na muda wa saa 8 ambao ilionekana angani kabla ya kupotea kwenye rada za kijeshi

5] inatafutwa na nchi zaidi ya 25 pamoja na meli, ndege, viona mbali,

kwa hiyo umakini mkubwa unaotumika kuitafuta hii ndege leo ni siku ya 11 na ukiongezea hawa vijana walioingia kwenye hiyo ndege wakitumia pasipoti za wizi , tena wakitokea kwenye taifa ambalo lina mashaka makubwa, na ambalo hapo nyuma lilishakaririwa likisema linataka kuiondoa israel kwenye uso wa dunia, kusema kweli ni lazima mataifa na hata dunia likiwepo taifa letu tuwe macho sana.

kwa sasa hatuwezi kujua hii ndege iko wapi, ni imetekwa? hakuna anayejua, imeanguka baharini hatujui, imepaa imeishia mawinguni hatuelewi. kwa hiyo chochote kinaweza kutokea sehemu yeyote ambayo hatujui. kwa sababu ndege inaruka juu na inaenda kwa kasi kubwa
hapo umenena .sasa hawa wanaosema dunia si salama wanataka twende wapi.dunia ni dunia tu na ndio ilivyoumbwa ,tatizo likitokea ndio mwanzo wa kugundua teknolojia ya juu zaidi
 
Wote tunajua kwamba ndege ya Malaysia imepotea takrabani wiki mbili sasa na wala haijulikani mahali ilipo. Kuna juhudi mbalimbali za mataifa ya magharibi na mashariki yanaangaika kuitafuta lakini bila mafanikio. Kwa sasa mimi kama mwananchi wa dunia ya tatu au nchi zinazoendelea nimejiuliza maswali mengi sana;

  • 1. Kama nchi zilizoendelea zimeshindwa kuipata hiyo ndege duniani kuna usalama gani? Hapa ina maana kwamba nchi zilizoendelea zimejiimarisha zaidi kiteknolojia, wameweka rada na setelaiti kila mahali hasa kwenye anga za juu ili waone kila kitu kinachoendelea duniani.
  • 2. Sasa dunia tujue lipi? Abiria wapo hai au wamekufa? Kama wamekufa maiti zao ziko wapi?
  • 3. Malaysia ni nchi ambayo imepiga hatua sana katika maendeleo ijapokuwa kwenye miaka ya 1960 ilikuwa karibu sawa na Tanzania, hata matokeo makubwa sasa (the big results now) Tanzania iliiga kwao, sasa na wao walifanya juhudi gani kuhakikisha usalama wa abiria na mali zake? Kwani hawakujua hujuma zilizokuwepo kabla (if any)? Au wanategemea mataifa ya magharibi yaangalie usalama wao?
  • 4. Nchi za dunia ya tatu ikiwemo Tanzania tumejifunza nini kutokana na mkasi huu? Kuna haja ya kuendelea kuzitegemea tena nchi za magharibi kwenye maswala yetu mbalimbali ikiwamo maswala ya ulizi na usalama?
  • 5. Je Tanzania ni salama kwa Utegemezi wa Marekani?
Naomba sana Moods msiondoe Uzi huu au kuuhamisha, uzi huu kwa mtazamo mfupi inaweza isionekana ya kisiasa lakini ukweli ni kwamba ni siasa tupu. Nchi zilizoendelea zinatumia technolojia zao kututisha na hata kutulazimisha tufuate siasa wanazo zitaka, wote tunajua yaliyomkuta Ghadafi , Sadam na wengineo. Hapa sio kwamba ninabeza technolojia ya nchi za magharibi bali tafakari pana kama technolojia zao zinaweza kukabiliana na changamoto za sasa. Yaani kwa mshangao wangu ni kuwa wao wana masetilite kila mahali mpaka kwenye mwezi wameshindwaje kuiona hii ndge ilipoelekea? Technolojia zao ni chui la makaratasi? Yaani technolojia zao zilitufanya tufikirie kwamba hata tukilala usiku na wake zetu hawa wajamaa huwa wanatuona. Naomba kuwasilisha

Long ago Marekani waliamua ku-abandon research zao kuhusu UFOs baada ya kuwa wamejiridhisha kuwa UFOs hawapose any threat kwa maisha ya viumbe waliopo duniani. Nadhani kuna haja sasa wa-revisit decision yao kuhusu swala hili. Wasiendelee ku-rule out kuwa siyo threat rather watumie hypothesis ya kuonyesha kuwa hawajui kama UFOs ni threat ama siyo threat na hivyo waingie kazini tena wakishirikiana na mataifa mengine yenye uwezo wa kufanya hivyo. Still, mimi naamini kabisa kuwa bado tuko salama, na tutazidi kuendelea kuwa salama kadri siku zinavyozidi kwenda mbele kwa sababu only the living God rules the world, no more no less, hiyo ndiyo an undeniable fact ya kwanza na ya mwisho hapa duniani!
 
Back
Top Bottom