KING MIDAS
JF-Expert Member
- Dec 1, 2010
- 10,569
- 21,075
DUNIA NA ULIMWENGU ULITOKEA WAPI?
BIG BANG ni mlipuko mkubwa ajabu sana ambao ulitokea hapo kale ikihusisha dark energy/nishati nyeusi au nishati ya kiza na chanzo cha nishati hiyo ya giza haijulikani ni nini wana sayansi wanadai ndani ya hiyo nishati ya kiza ilizaa kila kitu unachokiona kulitokea au ilizaa mlipuko mdogo sana na ndani ya sekunde likawa ni limlipuko likubwa ajabu ambapo hatujawahi shuhudia na ndipo kukazaliwa solar nebula, pembezoni mwa ulimwengu utashuhudia hizi solar nebula hivyo ulimwengu inakuwa siku hadi siku na haina mwisho wake
SOLAR NEBULA ni gesi na mavumbi yanayoekea angani baada ya dark energy/nishati ya giza kufanya kazi yake, haya magesi na mavumbi huwa ndiyo hugeuka baadae na kuwa kama vimawe vidogo vidogo sana na gesi
Basi SOLAR SYSTEM yetu tuliyomo ilianzaje???? Inasemekana miaka billion 4.7 iliyopita jirani kulikuwa na supernova mlipuko wa nyota kongwe sana na hapo ukubwa wa mawimbi yake ulipelekea baadhi ya vipande visambae hadi huku kwenye solar nebula yetu huku yale mawimbi yakapekea mavumbi na gesi yaanze kuzunguka kwa spidi kubwa sana chukua sahani uiweke chin kisha izungushe na hapo ndipo chemical reaction iliongezeka metals zilizaliwa na helium pia
Basi zile matals nzito zilikaa katikati na JUA likazaliwa na nyepesi pembezoni kidogo na nyepesi zaidi pembeni kabisa kiufupi maada nzito zilikaa kati kwa mpangilio kwenda nyepesi zilikaa pembezoni, mfano Terrestrial planets kama Mercury, Venus, Earth na Mars zina metals nzito zaidi tofaut na zile zilizopo nyuma ya uwanda wa asteroid belt ambazo nyingi zimeundwa kwa gases au liquids (mfno Maji)
Kiufupi Muda ulivyosogea mbele solar system ilianza kupoa taratibu jambo ambalo lilipelekea vigimba kuanza kuungana na kuunda magimba madogo na hatimae makubwa zaidi na zaidi hadi baadae kuwa SAYARI, SATELLITES, ASTEROIDS NA METEOROIDS ( niachie hapa nitakuja endelea ikiwa kuna uhitaji)
Dunia, ni sphere (tufe) na kuanzia ndani kati kilomita 3200au 6000 matabaka mbalimbali likianza na core(inner & outer) ambalo ni uji wa moto wa chuma, mantle(lower and upper)uji moto wa mawe,lava, crust, mawe, udongo na maji
Sasa THEIA lisayari lingingine likiwa na ukubwa karibia sawa na dunia kwa spidi iliingia kwenye orbit ya dunia na kuigonga dunia badala ya kuungana ikafanya kama vitenes vigonganapo na kuancha sehemu yake hapa duniani na kwa kuwa imemgawia nguvu dunia basi ilimbidi dunia imkokote nae akaitwa moon(mbalamwezi au mwezi)
Basi hapo vumbi lilikuwa limejaa anga zima na joto lilikuwa ni kali sana kadiria 200°C hadi 600°C na hakukuwa na hata tone la maji dunia nzima wala udongo mzuri, basi anga lilipoa zaid na zaid na vumbi la anga likaanza kutua juu ya ardhi likitengeneza kama utepe wa udongo laini huku volcano nazo zikiendelea kupoa hapo ni kadri ya miaka milion 1.5 iliyopita, vimondo (asteroids, comets na meteoroids ziliendelea kurindima kama kawaida kwenye anga la dunia), inaminika anga lilivyopoa basi ilikuwa zamu ya vimondo vilivyokuwa vimejaa mabarafu ya maji yenye chemikali mbalimbali na mara vilipoingia anga la dunia(atmosphere) viliyeyuka na kupelekea mvua kubwa kunyesha pande zote na kuijaza dunia nzima bahari hata baadae nchi kavu ilianza kuibuka ndani ya maji nchi hiyo ilikua ni moja kubwa ulimwengu mzima lililoitwa Pangea, pangea nayo ilikuja kuvunjika kutokana na mitetemeko na kutokea vipande vipande vya nchi na mabara hadi leo.