Dunia ipo katika process ya kujiangamiza? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Dunia ipo katika process ya kujiangamiza?

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Lukwangule, Feb 28, 2010.

 1. L

  Lukwangule Senior Member

  #1
  Feb 28, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna majanga mengi yanatokea duniani hasa yanayohusiana na mabadiliko ya tabia nchi, matetemeko na milipuko ya volkano.Maelezo haya yanayokuja chini ni matokeo ya maneno na maulizo niliyokutana nayo na washiriki wenzangu ndani ya JF wakizungumzia Haiti na Chile na Japan pia. lakini kuna tetemeko kubw ala China na nikasema ngoja namie niwapatie watu mambo niliyosoma katika kitabu kimoja kilichopandikwa 2004 Hercolubus or Red Planet.
  Kitabu hiki niliomba niletewe baada ya kukisoma katika mtandao na kweli watu hao waliniletea. Ukikisoma kitabu hiki walahi unaweza kupatwa na wazimu.
  Lakini siku zote wanadamu ndio chanzo cha wazimu wa wanadamu wenzao. Kitabu hiki hakiingiliani na imani zako ingawa unatakiwa kwenda na akili katika kukisoma.
  Ni kitabu ambacho kinaelezea kinagaubaga kwa mfumo wa akili tambuzi kuhusu maangamizi ya dunia hii.
  Kitabu hiki hakina uhusiano wa wazi na Biblia ambayo ninajenga mazoea ya kuisoma.Lakini ndani ya kitabu neno upendo na utunzaji wa mazingira ni kitu kinachozungumzwa sana. Kitabu hiki kinaitwa Hercolubus or Red Planet.
  Kwa mujibu wa mwandishi, kitabu hiki ni onyo kwa wanadamu kuhusu maangamizi ya dunia wanaoishi kutokana na kuwa sayari Hercolubus kuendelea kuikaribia dunia.
  Imeelezwa kuwa sayari hii kubwa ina nguvu kubwa ya mvutano ambayo itasababisha matetemeko ya ghafla yaliyo makubwa na yanayoweza kutokea kwa mkupuo mmoja pamoja, mawimbi makubwa ya bahari, milipuko ya volkano na mambo mengine ambayo ni tishio kubwa kwa sayari hii ya wanadamu.
  Kitabu kimeelezwa kuwa matukio yatazidi ukubwa na ukali wake kwa jinsi sayari hiyo inavyozidi kuiakribia dunia na hali itaendelea mpaka dunia itakapomezwa na kuangamizwa kabisa.
  Mwandishi V.M. RabolĂș anaelea kwa undani majanga yanayoikabiuri dunia ikiwa na pamoja na yale ambayo tayari yameshaanza kutokea yakiwa ni ishara ya uharibifu mkubwa duniani.
  Pia katika kitabu chake kuna kitu alichodai ni fomula ya kuepuka maangamizi.
  kwa maelezo zaidi ingia http:lukwangule.blogspot.com
   
 2. K

  Kidatu JF-Expert Member

  #2
  Feb 28, 2010
  Joined: Jun 11, 2008
  Messages: 1,494
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 145
  Asante mkuu kwa kutupa habari hii. Ngoja nami niingia katika blog hiyo ili nipate copy ya kitabu hicho.
   
 3. Pape

  Pape JF-Expert Member

  #3
  Feb 28, 2010
  Joined: Dec 11, 2008
  Messages: 5,513
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  lol 4 pages pdf
   
 4. C

  Cotan Member

  #4
  Feb 28, 2010
  Joined: Feb 11, 2010
  Messages: 72
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  asante mkuu
   
 5. Kituko

  Kituko JF-Expert Member

  #5
  Feb 28, 2010
  Joined: Jan 12, 2009
  Messages: 9,517
  Likes Received: 7,271
  Trophy Points: 280
  lakini pamoja na hayo maelezo ukweli unabaki palepale kwamba hayo matetemeko na volcano eruption ni matokeo ya Geological internal proces, na sio kweli kwamba sasa yamezidi kuliko hapo zamani, kuna uwezekano kwamba sasa yamepungua kwa sababu kwa asilimia kubwa dunia ilifikia katika kiwango chake cha kujibalance,
  Mfano chukulia pale Ngorongoro Crater, ule ulikuwa ni mlima mkubwa labda zaidi hata ya kilimanjaro lakini kwa sababu ya eruprtion ya volcano kutoka huo mlima ndio hiyo crater ika form (Crater formation)

  kweli nakubliana na wewe kuwa shughuli za kibinadamu zinaweza kwa kiasi kikubwa kutokea kwa haya matetemeko
  chukua mfano wa bara la Africa, kwa hapa lilipo linaonekana kama liko sattled na limejibalance vizuri kutokana na uzito wake relative to the entire Earth (Isostance), sasa imagine madini yote yanayochimbwa Africa millions of tons (Iron, Copper,gold, nickel, diamond, caco3 ect), na kumbuka hizi tani zinaenda out of Africa say europe or America, sasa Automatically Bara la Africa litakuwa linaloose weight na same time Europe ina gain weight, sasa katika kujibalance na kucompersent weight loss na weight gain lazima haya mambo yatokee na yatatokea sana
   
 6. L

  Lukwangule Senior Member

  #6
  Mar 11, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 150
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nataka kusema kwamba maelezo ya kituko ni bomba na yalienda shule thanks kwa kunielimisha. this is what i call knowledge beyond what what, thanks man I apprecciate
   
 7. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #7
  Mar 11, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 15,241
  Likes Received: 2,328
  Trophy Points: 280
  Kwakuwa kitabu hicho kina ukaribu na Bible nitakitafuta nikisome, nashukuru
   
 8. Isimilo

  Isimilo JF-Expert Member

  #8
  Mar 11, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 219
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  hiyo sayari kwa jina inaitwa Nibiru au Planet X.
  imekua ikija karibu na dunia kwa interval ya muda mrefu sana. sio lazima iimeze ila kile kitendo cha kuikaribia tu ndicho kinachofanya uharibifu huo.
   
 9. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #9
  Mar 11, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,891
  Likes Received: 181
  Trophy Points: 160
  kwangu maisha ni "Ni ubatili, ni ubatili!...ubatili mtupu! Kila kitu ni ubatili.
  Dunia iwepo ama isiwepo, ni ubatili.
   
 10. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #10
  Mar 11, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,382
  Likes Received: 1,200
  Trophy Points: 280
  Haya yote yametabiriwa ndani ya kitabu cha biblia. Tofauti pekee nninayoweza kuiona ni lugha ya kitaalamu iliyopo kwenye kitabu cha Red planet ya kuweza kuufikisha ujumbe kwa lugha ya kueleweka kwa waliowengi ambapo lugha ya nabii zilizopo ndani ya biblia ni ngumu kwao kuzitafsiri.
   
 11. Isimilo

  Isimilo JF-Expert Member

  #11
  Mar 11, 2010
  Joined: Aug 16, 2007
  Messages: 219
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  ukitaka kujua ugumu ulioko kwenye kutafasiri unabii ndani ya biblia- ingia kichwakichwa kwenye daniel chapter 11. utapata habari yake.
  inadaiwa hiyo sura imebeba unabii mgumu kuliko nabii zote kueleweka ndani ya biblia na unabii mrefu ulioanzia tangu babylonia ya zamani hadi siku ya mwisho wa dunia
   
 12. FirstLady1

  FirstLady1 JF-Expert Member

  #12
  Mar 11, 2010
  Joined: Jul 29, 2009
  Messages: 16,640
  Likes Received: 625
  Trophy Points: 280
  thanx Lukwangule
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...