Siku wakisema kila nchi itumie vitu ilivyotengeneza yenyewe hata sipati picha! msafara wa rais utakuwa na lundo la mikokoteni,kuhamia Dodoma ndo itakuwa basi tena,wali tutalia vidole,kuangalia Tv na kusikiliza redio ndo kwaheri,show za fiesta hazitakuwa na maiki wala spika,fikiria nguo za mitumba zote,majinsi makali,makadeti,viatu vyote vya wazungu vikachukuliwa...ndio utajuwa waafrika tuko nyuma kiasi gani,Tujenge viwanda tuache utani.