Dunia ina mambo...

Najarbu kuwaza hvi umri huu ntakuja kumpenda mwanamke kindak ndaki namna hyo daah sjui aisee
Nahis moyo wangu ushaamuwa kuwa mbinafsi
 
What goes around comes around ,baadhi ya wanaume wakikutana na mabinti wanaowapenda kwa dhati upenda kuwanyanyasa na kuona dunia yote wameishikilia ila baadae huja kukiona cha moto ,Karma atamlipia huyo binti msahuri aachane nae aendelee na maisha kwani huyo jamaa sio mwanaume peke yake wapo kibao tu
 
Habarini wadau?
Nimeshuhudia tukio la kusikitisha sana na kila mara ninalifikiria.
Iko hivi, mimi ni mpangaji mmoja wapo kati ya wapangaji watatu.
Kisa hiki ni juu ya mpangaji mwenzangu anayoyafanya wajameni.

Kuna binti mlemavu na pia ni yatima (baada ya kujua story yake ndipo nikajua kuwa ni yatima) Binti huyu mara kadhaa nilimkuta mlangoni kwa mshikaji. Ni sehemu yenye mbu kutokana na mazingira yalivyo lakini binti anamvumilia mshikaji hata saa sita usiku.

Ipo siku ambayo aliwahi kulala hapo nje mshikaji akiwa amelala ndani bila kumjali.
Katika kudodosa ni kwamba msichana alikuwa ni mpenzi wa huyu jamaa kabla ya huyu jamaa kuhamia kwake.

Mwanzo wa mapenzi yao, binti anadai jamaa alimpenda kweli na kumjali kwa kila hali. Kwa kuonyesha mapenzi yake, binti akawa akipata pesa kidogo anagawana sawa na mshikaji. Binti pamoja na ulemavu wake ni shupavu wa kutafuta pesa. Hana wazazi wala walezi wanaojua kula yake.

Huyu jamaa kwao yupo njema lakini bado alimkandamiza binti kwa maneno matamu na kuna muda alimpokonya kila senti aliyokuwa nayo huku yeye akitumia kwa starehe zake. Binti alivumilia na hata kushinda njaa ili huyu jamaa aweze kufurahi.

Jamaa alipotaka kuhama, alimuomba binti pesa za kulipia chumba kwa miezi sita. Binti akahangaika akijua wanayapanga. Jamaa alipopata pesa hizo, alipanga na hakutaka kumwonyesha binti wapi anaishi. Ilipita muda mrefu hadi binti alipopelekwa nyumbani kwa mshikaji tena kwa masimango.

Hapo ndipo akajua wapi mshikaji anaishi. Baada ya muda mfupi tu, mshikaji akamtema binti kwa maneno ya kejeli kuwa "yeye ni mlemavu na hakuna mwanaume atakayemuhitaji. Pia alikuwa nae kipindi ana shida na sio sasa. Hakuwahi kumpenda wala kuwa na ndoto nae." Binti sasa anatia huruma kwani anadai alikuwa akimpenda mshikaji kwa dhati.

Ndugu zangu, kuna watu wa kufanyiwa mabaya na kuchezewa, lakini kwa hawa mabinti ambao wanakuwa na mapenzi ya dhati na kuwasimanga kwa maneno makali, binafsi inaniuma sana. Mkimuona mshikaji ni kama mtu vile.

Kumbe ndani ni shetani. Nae anatuambiaga binti analazimisha upendo naye hamtaki. Hana sababu ya maana ambayo mnaweza kuielewa. Mungu yupo...
Tafuta namna ya kumsaidia hata kwa ushauri tuu utabarikiwa sana kuliko kuendelea kumuona akiteseka.
 
Kweli dunia ina mambo toka kitambo..Binti asife moyo anaweza kupendwa tena na maisha yakaendelea
 
Kwani mwanamke ni wa mtu mmoja? miss chagga

Chibuku ni pombe ambayo walioibuni waliileta wakawa wanaiuza kwa kutumia mavikombe makubwa mapana ya plastiki. Sababu ni kwamba, watu wanyee kikombe kimoja wengi mkiwa mnazungusha kwa wote waliopo hapo.
Lakini, soda kinywaji ambacho ni common kwa watu wote kikaletwa kwenye chupa yenye mdomo mwembamba. Kila chupa kwa mdomo mmoja. Huwezi fungua chupa, uizungushe kwa watu ati kila mtu anywe kidogo kidogo. Huo si ustaarabu wala si vyema kwa afya yako.
Pia, mwanamke alivyo umbwa, aliumbwa kwa ajili ya mtu mmoja tu. Si kwa ajili ya wengi. Hata maandiko yaliwataja wanaume waliokuwa na wanawake wengi kwa kipindi kimoja ila hakuna mwanamke aliyetajwa akiwa na wanaume zaidi ya mmoja.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom