Dunia haiko Fair na Haijawai kuwa Fair

Dunia haiko Fair na Haijawai kuwa Fair

Dr wa Kaliua

JF-Expert Member
Joined
Sep 20, 2020
Posts
1,634
Reaction score
3,883
Shalom Wana JF
Dunia Ni sehemu salama Sana, Lakini pia ni sehemu hatari Sana!!

Katika maisha yako, usitegemee kufanyiwa Mema hata Kama wewe unafanya Mema(yaani kuwafanyia wema watu wengine sio guarantee ya wewe kutendewa Mema)

Ishi kwa kufuata misingi ya Imani ulionayo lakini pia kufuata Sheria na Taratibu za nchi!!!

Ila usijaribu kuishi kwa kuangalia wengine watazungumzia Nini kuhusu wewe.

Hivyo Basi kuwa makini na watu wafuatao!
1.Mtu ambae anapendekeza pesa kuliko utu,
Ukishagundua rafiki yako au mtu wako wa karibu anapenda sana pesa kuliko utu kaa Nae mbali
Maana IPO siku atatumia pesa kuondoa uwepo wako haijalishi mna uhusiano kiasi gani.

2. Kuwa makini na ndugu zako,
Ni nature ya kila mwanadamu kuchukia maendeleo ya Binadamu mwenzake hivyo hata Kama una ndugu anaekuambia anakupenda na kukuthamini, kaa nae kwa umakini Sana!! (Adui hatoki mbali)) ndugu Ni Miongoni mwa wanaorudisha mipango mingi.

3.Mfanyabiashara.
Hakuna mfanyabiashara ambae Yupo kukupa Faida wewe bila yeye kupata Faida! Hivyo unapoenda dukani au sokoni vaa roho ya paka!! Unaweza kuuziwa vitu kwa gharama ya juu simply because umeendekeza ujamaa.

5. Mtu Yoyote usiemjua.
Tengeneza attention kubwa sana, unapokaaa na mtu usiemjue kwenye usafiri au hata kwenye eneo Lolote la mkusanyiko.
Sio kila anakuja kwako anakuja kwa wema, wengine wanakuja kukusambalatisha.. hivyo kuwa makini na mtu mgeni kwako.

6. Jiepushe na hasira na tamaa.
Miongoni mwa Mambo yanayopeleka watu Jera Ni taama na hasira... Hivyo kaaa mbali na mtu yoyote anaekufanya uwe na hasira, rakini pia kaa mbali na mtu ambae atakufanya uwe na tamaa.

Dunia Ni mahali salama Kama utaaamua kujiepusha na vitu viatakavyo kupotezea dira, Ila Ni sehemu hatari Sana Kama hutozingatia hayo juu.

#nimejifunza kitu hapa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom